Kondomu ni mpira ambao uwekwa kwenye uke au uume kwa ajili ya kuzuia mimba wakati wa kujamiiana
Mtazamo juu ya matumizi ya kondonu umekuwa ukikabiliwa na imani za kidini. Zipo dini ambazo zinakataza kabisa, lakini zipo ambazo zinakubali endapo kutakuwa na haja ya kiulazima za kiafya. Kwa vyovyote itakavyokuwa haja ya kutumia kondomu ipo kulingana na sababu mbalimbali. Sababu nyingine zinakubaliwa na dini zote kwa mfano kuzuia kizazi endapo itaonekana ni hatari kwa mwanamke huwenda akapoteza maisha pindi akipata ujauzito, ama kulinda ndoa ambazo mmoja wao ameathirika. Zipo sababu nyingine ambazo zinaweza kukubalika katika dini zote.
Sasa kwa kuwa hali ya matumizi ya kondomu yapo kama hivyo basi ipo haja ya watu kuelezwa faida na hasara ambazo unaweza kuzipata kama utaamuwa kutumia kondomu. Faida hizi na hasara zitasaidia kukukumbusha kuendelea kuwa makini hata ukiwa unatumia kondomu.
Aina za kondomu
1. Kondomu ya kike ambayo huvaliwa na mwanamke wakati wa kujamiiana
2. Kondomu ya kiume, hii ni Aina ya kondomu inayovaliwa na mwanaume wakati wa kujamiiana
Faida za kutumia kondomu
1. Kuzuia kuongezeka kwa mimba zisizotarajiwa
2. Kuzuia magonjwa ya ngono
3. Kuzuia kuambukizwa kwa ugonjwa wa Ukimwi
Kati ya njia za uzazi wa mpango kondomu ndiyo njia pekee inayosaidia kupunguza kusambaa kwa magonjwa ya ngono na Ukimwi
Hasara za kutumia kondomu
1. Kondomu hukinga maambukizi ya magonjwa ya ngono, yanayoingia kwa njia ya ngono, lakini upo uwezekano wa kupata endapo kindomu itapasuka, ama itavuka wakati wa tendo. Pia kama kuna mikato iliyosababishwa na kunyoa na ikawa ipo wazi kuruhusu vijidudu kupendya kwa wawili hawa upo uwezekano wa kupata magonjwa. Ama kuvuka kwa kondomu au kupasuka upo uwezekano wa kupata ujauzito. Ijapokuwa hali hizi ni mara chache sana kutokea. hii inakuwa hasara endapo mtu atajiamini kwa asilimoa 100 kuwa yupo salama anapotumia kondomu bila ya kuchukuwa tahadhari nyingine.
2. kondomu kwa baadhi ya watu inawaletea allegi kama miwasho na mapele. Hii inatokana na mafuta yanayowekwa. Kwa baadhi ya watu miili yao haiendani na mafuta hayohivyo kuwasababishia aleji kila wanapotumia. Zungumza na daktari endapo una tatizo hili la aleji unapotumia kondomu.
3. kuna baadhi ya kondomu zinawekwa vilainishi vya Nonoxynol-9 kwa ajili ya kuuwa mbegu za kiume. Vilainishi hivi vinaweza kusababisha madhara kwenye uke kama kuwashwa hivyo kupelekea kuongezeka kwa hatari ya kupata maradhi ya ngono.
Kuwepo kwa hasara hizi inamaanisha kuwa watumiaji wa kondomu wawe makini wasijipe matumaini ya kuwa salama kwa asilimia 100, kwani chochote kinaweza kutokea.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi madhara ya kutumia madawa ya kupunguza maumivu,ni madhara ambayo utokea kwa mtu anayetumia madawa ya kupunguza maumivu.
Soma Zaidi...Tezidume ni moja ya magonjwa hayari yanayotokea katika mwili wa mwanaume.Hapa nimekuandalia sababu za kutokea kwa tezi dume.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na hatua za kujikinga na Maambukizi ya Uvimbe kwenye ovari na kwenye mirija ya uzazi
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea hatua za ukuaji mimba na dalili zake
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za maumivu ya uume baada ya tendo la ndoa
Soma Zaidi...Swali langi ni hiliMama mjamzito anapo hisi uchungu je mtoto huendelea kucheza tumboni?
Soma Zaidi...Je, unafahamu dalili za mwanzo za ujauzito? Kutoka kwa kichefuchefu hadi uchovu, ujue nini cha kutarajia.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia Faida za Uzazi wa mpango kwa watoto, mama, wanandoa, na jamii au JUMUIYA.
Soma Zaidi...KubaleheΓΒ ni wakati mwili wa mtoto unapoanza kubadilika na kuwa wa mtu mzima (balehe) hivi karibuni. Kubalehe ambao huanza kabla ya umri wa miaka 8 kwa wasichana na kabla ya umri wa miaka 9 kwa wavulana.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza baadhi ya dalili za mimba kuanzia week mbili Hadi mwezi
Soma Zaidi...