FAIDA ZA UKWAJU (TAMARIND)


image


Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za ukwaju


. Faida za ukwaju (Tamarind)

Ukwajju ni katika mimea ambayo matunda yake yanatumika katika kutengenezea madawa ya hospitali. Kinywaji cha ukwaju hutumika katika kutibu kuharisha, kukosa choo, homa na aina za vidonda vya tumbo. Tofauti na matunda pia majani na maganda ya mti huu pia hutumika katika kutibu vidonda. Wataalamu wa afya bado wanaendelea kuuchunguza mti huu kwa ajili ya kupata tiba zaidi.

 

Antioxidant ambayo ipo kwenye ukwaju husaidia katika kudhibiti na kulinda mwili dhidi ya maradhi ya moyo, saratani na kisukari. Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa ukwaju husaidia katika kushusha kiwango cha sukari kwenye damu. Pia kwa watu wenye kutaka kupunguza uzito, ukwaju pia husaidia.

 

Ukwaju una virutubisho vingi sana kama vile:- madini ya magnesium, potassium, chuma, calcium na phosphorous. Pia kuna vitamin B1 (thiamin), vitamin B2 (riboflavin), vitamin B3 (niacin). pia kuna vitamin C, k na B6 na B5. kwa ufupi ukwaju ni katika matunda ya asili yalotumiwa na watu toka zamani sana.

 

Katika ukwaju kuna polyphenols kama vile flavonoids ambayo husaidia katika kudhibiti kiwango cha cholesterol na triglycerides. Antioxidant zilizomo kwenye tunda hili husaidia katika kulinda mwili dhidi ya maradhi ya moyo. Pia ukwaju husaidia katika kutengeneza dawa za malaria.

 

Tafiti za kisayansi zinaonesha kuwa ukwaju husaidia katika kupunguza uzito. Itambulike kuwa kuzidi uzito mwilini kunahusianishwa sana na maradhi ya moyo, ini, na figo. Hivyo ukwaju husaidia katika kupunguza choloesterol mbaya (LDL) na husaidia katika kuongeza cholesterol nzuri (HDL).

 

Ukwaju una potassium bitartipate ambayo hii husaidia katika upatikanaji wa choo na kuzuia kuganda kwa choo. Mizizi na maganda ya mkwaju husaidia sana kwa maumivu ya tumbo. Uw.epo wa procyanidins kwenye ukwaju husaidia katika kulinda ini dhidi ya uharibifu. Pia ukwaju hutumika katika kutibu along’atwa na nyoka



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Hadiythi za alif lela u lela       ðŸ‘‰    2 Jifunze fiqh       ðŸ‘‰    3 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    4 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    5 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    6 Mafunzo ya html kwa kiswahili    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Karanga (groundnuts)
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula karanga Soma Zaidi...

image Faida za kiafya za kula kisamvu
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kisamvu Soma Zaidi...

image Uyoga (mushrooms)
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula uyoga Soma Zaidi...

image Faida kula fenesi
Somo hili linakwenda kukuletea faida za kiafya za kula fenesi Soma Zaidi...

image Faida za kiafya za kitunguu maji
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kitunguu maji Soma Zaidi...

image Faida za kula stafeli/soursop
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za stafel/soursop Soma Zaidi...

image Faida za kiafya za kula fyulisi/ peach
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula fyulisi/peach Soma Zaidi...

image Naomba mnielekeze jinsi ya matayarisho ya Mbegu za papai mpaka nianze kuzitumia kama tiba
Mbegu za papai ni katika baadhi ya mbegu ambazo hutumika kama dawa, na tunda lake ni katika matunda yenyevirutubisho vingi sana. Mbegu za papai zinatumka kwa matumizi mengi sana kiafya. Je ungependa kujuwa faida za papai na jinsi ya kuandaa mbegu zake kama tiba? endelea na makala hii Soma Zaidi...

image Limao (lemon)
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula limao Soma Zaidi...

image Faida za mbegu za papai
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za mbegu za papai na umuhimu wake kiafya Soma Zaidi...