Faida za uzazi wa mpango kwa watoto.

Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa uzazi wa mpango kwa watoto, sio akina Mama peke yao wanaofaidika na uzazi wa mpango vile vile na watoto wanafaidika na uzazi wa mpango kama ifuatavyo.

Faida za uzazi wa mpango kwa watoto.

1.kwanza kabisa tunajua lengo kuu la uzazi wa mpango ni kupata namba ya watoto wanaohitajika na kuwapa nafasi ya kutosha kutoka kwa mtoto mmoja kwenda kwa mwingine, kwa hiyo na watoto wanapata faida ya uzazi wa mpango kama ifuatavyo.

 

2.uzazi wa mpango ukitumiwa ipasavyo unawapa watoto nafasi ya kupendwa na wazazi wao kwa mfano watoto wakizidiana miaka minne kwa vyovyote yule mtoto atainja mapenzi ya wazazi wake kuliko wale watoto wanaozidiana mwaka mmoja mmoja kwa hiyo tuwape watoto nafasi kati ya mtoto mmoja kwenda mwingine ili waweze kuonja mapenzi ya kweli kutoka kwa wazazi wao.

 

3.Pia uzazi wa mpango unawapa watoto nafasi ya kunyonya kwa mda mrefu , tunajua wazi kubwa mtoto alinyonya kwa mda unaofaa anakuwa na afya nzuri pia anaweza kukingwa dhidi ya magonjwa kuna  wataalamu wanasema mtoto alkinyonya kwa mda wa kutosha anakuwa na akili za kufikiria kwa hiyo tuwape watoto mda waweze kunyonya kwa mda wa kutosha.

 

4.Uzazi wa mpango inawasaidia watoto wapate elimu ya kutosha kwa sababu mtoto akikaa na Wazazi kwa mda anajifunza mambo mengi kuliko wakiwa wengi na pia wazazi wataweza kupata Ela na kumpeleka mtoto wao shule nzuri kuliko kama wangekuwa wengi.

 

5.Pia uzazi wa mpango unasaidia kupunguza vifo vya watoto wakiwa wadogo , kwa sababu ya kukosa mahitaji muhimu au kuzaliwa wakiwa hawajafikishwa umri au na uzito mdogo kwa hiyo tunapaswa kujua kuwa hata watoto wenyewe ikiwa wazazi wakitumia njia ya uzazi wa mpango nao wanapata faida kwa hiyo wazazi na jamii kwa ujumla mnaalikwa kutumia njia za uzazi wa mpango ili kuyafanya maisha ya watoto yapendezeJe! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/02/21/Monday - 03:20:06 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 805


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-