picha

Faida za vitamin C mwilini

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za vitamini C mwilini

FAIDA ZA VITAMINI C MWILINI

 

Kama tulivyokwisha kuona vyakula vya vitamini C kama vile papai, machungwa, mananasi, maembe, malimao na ndimu. Pia tuliona baadhi ya kazi za vitamini C ambazo ni kusaidia katika kuuwa kemikali mbaya mwilini, kuipa nguvu miili yetu ya kupambana na maradhi. Katika makala hii nitakwenda kukujuza umuhimu wa vitamin C katuka mwili wa kila kiumbe akiwemo binadamu.

 

Faida na umuhimu wa vitamini C

1.Hulinda mwili dhidi ya maradhi ya kiseyeye (scurvy): Haya ni maradhi ambayo hufanya mwili uweze kutoa damu kwenye mafinzi, mwili kuchubuka kwa urahisi, kuchelewa kupona kwa majeraha. Kusoma zaidi kuhusu ugonjwa huu pitia zaidi makala zetu.

 

2.Kulinda mwili zidi ya maambukizi na mashambulizi:

Tafiti mbalimbali zilizofanya zinaonesha kuwa vitamini C inaweza kusaidia kupunguza nguvu za virusi waletao mafua na homa ya mafua. Baadhi ya tafiti zinadiriki kusema kuwa vitamini hivi kuponyesha mafua yaa kwa haraka, lakini ambalo halina shaka ni kuwa vitamini c vinaweza kupunguza kupata mafua ya mara kwa mara au kufanya mafua yaondoke kwa haraka.

 

3.Vitamini C ni muhimu sana katika mfumo wa kinga mwilini. Kwani vitamini C husaidia katika Antimicrobial yaani katika kuzuia vijidudu shambulizi mwilini kama bakteria na virusi, pia vitamini C husaidia katika Natural killer cell yaani katika kuuwa vijidudu shambulizi ama kuvizuia visiendelee kukua mwilini, pia vitamini C husaidia katika kuimarisha mfumo wa kinga kwa kuimarisha seli hai nyeupe ziitwazo lymphocyte hizi ndizo seli ambazo askari mkuu wa mwili dhidi ya vimelea vya maradhi kama virisi, fangasi, protozoa na bakteria.

 

4.Kulinda miili yetu dhidi ya saratani (cancer):

Tafiti mbalimbali zimefanywa kuhusu aina ya saratani na zinavyohusiana na vitamini C kama saratani ya matiti na mapafu. Ijapokuwa tafiti hizi hazikuweza kuthibitisha moja kwa moja kuwa vitamini C vinasaidia kuondoa saratani hizi kalaki kuna mambo ambayo tafiti hizi yametufungua mawazo:

A. Vitamini C husaidia kuborsha afya na kuishi vyema kwa wagonjwa wa saratani

B. Vitamini C inaweza kuuwa seli zinazotengeneza uvimbe wa saratani

 

5.Husaidia kulind miili yetu dhidi ya maradhi yanayohusu mishipa ya damu na moyo (cardiovascular)

 

6.Husaidia kulinda miili yetu dhidi ya maradhi ya ubongo na kusahasahau

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Vyakula Main: Post File: Download PDF Views 9154

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉4 web hosting     👉5 Kitau cha Fiqh     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zinazofanana:

Vyakula na vinywaji hatari na vilivyo salama kwa mgonjwa wa kisukari

Hapa utajifunza vyakula hatari kwa mgonjwa wa kisukari, pia utajifunza vyakula salama anavyotakiwa ale mgonjwa wa kisukari, Pia ujajifunza njia za kujikinga na kisukari

Soma Zaidi...
Kazi za madini ya Shaba mwilini.

Post hii inahusu zaidi madini ya Shaba mwilini,ni madini ambayo ufanya kazi mbalimbali mwilini, kama ifuatavyo

Soma Zaidi...
FAIDA ZA MAJI MWILINI

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...
Zijuwe faida za kiafya za kula nanasi

Je umeshawahi kula nanasi kwa wingi.

Soma Zaidi...
Vyakula Vya vitamini B, kazi za Vitamini B na dalili za Upungufu wa Vitamini B mwilini

hapa Tutakwenda kuona Vyakula Vya vitamini B, kazi za Vitamini B na dalili za Upungufu wa Vitamini B mwilini

Soma Zaidi...
Faida za kiafya za viazi vitamu

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula viazi vitamin

Soma Zaidi...