Mambo ya kuzingatia kabla ya kugawanya urithi
Kabla mali ya marehemu haijagawanywa kwa warihi wake, hapana budi kuzingatia yafuatayo:
(a)Haki zilizofungana na mali ya urithi:
Mali ya marehemu haitakuwa halali kwa warithi wake mpaka zitolewe haki zifuatazo:
(i)Madeni.
(ii)Zakat.
(iii)Gharama za makazi ya mkewe katika kipindi cha eda.
(iv)Usia ambao hauzidi theluthi moja (1/3) ya mali yote iliyobakia.
(b)Sharti Ia kurithi:
Kurithi kuna sharti tatu:
(i)Kufa yule mwenye kurithiwa (Si halali kurithi mali ya mtu aliye hai).
(ii)Kuwepo hai mrithi wakati akifa mrithiwa. Kwa mfano, kama wawili wanaorithiana mathalani baba na mtoto wote wamekufa. Aliyekufa nyuma (au aliyeshuhudia kifo cha mwenzie) atakuwa mrithi wa yule aliyetangulia kufa.
(iii)Kukosekana mambo yenye kumzuilia mtu kurithi.
(c)Mambo yanayomzuilia mtu kurithi
Mrithi huzuilika kurithi itakapopatikana na moja kati ya sababu zifuatazo:
(i)Kumuua amrithiye: Yaani mtu hatamrithi aliyemuua ijapokuwa kwa bahati mbaya.
Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema Mwenye kuua hapati chochote katika mirathi. (Tirmidh, Ibn Majah).
(ii)Kuhitalifiana katika dini:
Muislamu hamrithi kafiri, mshirikina, mkristo au myahudi na wala kafiri, mshirikina, mkristo au myahudi hatamrithi Muislamu hata akiwa karibu naye kiasi gani katika nasaba.
Usama bin Zaid (r.a)ameeleza kuwa mtume wa Allah amesema: Muislamu hamrithi mshirikina wala mshirikina hamrithi Muislamu. (Bukhari na Muslim)
Pia Mtume (s.a.w) amesema katika Hadithi iliyosimuliwa na Abdullah bin Amri(r.a) kuwa: Watu wa dini mbili tofauti hawatarithiana. (Abu Dauwd, Ibn Majah, Tirmidh).
(iii)Mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa hana haki ya kumrithi baba aliyemzaa na baba hana haki katika mirathi yake, kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:
Amri bin Shuab(r.a) ameeleza kutoka kwa baba yake naye kutoka kwa babu yake kuwa Mtume wa Allah amesema: "Atakayezini na mwanamke muungwana au na mjakazi, mtoto atakayepatikana humo hana haki naye. Hatomrithi na wala hatarithiwa naye ". (Tirmidh)
(d)Sababu za Kurithi:
Mtu hurithi kwa sababu moja katika hizi:
(i)Kuwa na nasaba na marehemu (baba, mama, mtoto, ndugu, n.k.). (ii)Kuoana kwa ndoa halali (yaani mume humrithi mke na mke humrithi mumewe).
(iii)Kuacha huru, yaani mwenye kumpa uhuru mtumwa humrithi huru wake.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Wajibu wa KufanyakaziUislamu siyo tu unawahimiza watu kufanya kazi na kutokuwa wavivu bali kufanya kazi ni Ibada.
Soma Zaidi...Udhaifu wa Hoja za Kudhibiti Uzazi:Hoja nyingi zinazotolewa kuunga mkono udhibiti wa uzazi zimejengwa juu ya hali na mazingira ya maisha yaliyoletwa na utamaduni na maendeleo ya nchi za Ulaya na Marekani.
Soma Zaidi...Kuzika Kuzika ni kitendo cha nne cha faradh tunacho lazimika kumfanyia ndugu yetu aliyetutangulia kufa.
Soma Zaidi...Hii ni hutuba ya ndoa kwa ufupi, Imekusanya mambo ya msingi yanayohitajika katika hutuba ya ndoa
Soma Zaidi...