Nini maana ya asaba katika mirathi ya kiislamu

Nini maana ya asaba katika mirathi ya kiislamu

Asaba - Warithi wasio na mafungu maalum



Asaba ni warithi wasiowekewa fungu maalum na hustahiki kupata mali yote ikiwa hapana wenye mafungu au kupata kilichobakia baada ya wenye mafungu kuchukua haki yao. Asaba wenyewe wako wa ama tatu:
(a)Asaba kwa nafsi yake.
(b)Asaba wa pamoja na mtu mwingine.
(c)Asaba kwa sababu ya mtu mwingine.
(a)Asaba kwa nafsi yake


(a)Asaba kwa nafsi yake
Ni wale wanaume tu ambao uhusiano wao na huyu marehemu haukuingiliwa na mwanamke. Nao ni hawa wafuatao:
I .Mtoto mwanamume.
2.Mjukuu (mwanamume).
3. Baba.
4.Babu (baba yake baba).
5.Ndugu wa kwa baba na mama.
6.Ndugu wa kwa baba.
7.Mtoto mwanamume wa ndugu wa kwa baba na mama.
8.Mtoto mwanamume wa ndugu wa kwa baba.
9.Ami wa kwa baba na mama.
1O.Ami wa kwa baba.
11.Mtoto mwanamume waAmi wa kwa baba na mama.
12.Mtoto mwanamume waAmi wa kwa baba.
13.Bwana na bibi mwenye kumuacha mtumwa huru.
14.Asaba wa mwenye kuacha huru mtumwa.



(b)Asaba wa Pamoja na mtu mwingine:
I .Binti akiwa pamoja na kijana mwanamume.
2.Binti wa mtoto wa kiume (mjukuu) akiwa pamoja na mtoto
mwanamume wa mtoto mwanamume (mjukuu wa kiume).
3. Dada wa kwa baba na mama akiwa pamoja na ndugu wa kwa
baba na mama.
4.Dada wa kwa baba akiwa pamoja na ndugu wa kwa baba.
5.Dada wa kwa baba na mama au wa kwa baba akiwa pamoja na babu.



(c) Asaba kwa sababu ya mtu mwingine:
Ni dada wa kwa baba na mama au wa kwa baba tu atakapokuwa pamoja na binti au binti wa mtoto wa kiume au wote wawili.



Musharakah - Kushirikiana fungu:
Ingawa asaba wote utaratibu wao wa kurithi ni mmoja lakini nani kati yao mwenye haki zaidi ya kurithi pindi wakitokea pamoja itategemea na uzawa wa karibu na uwiano wa uhusiano na maiti. Kwa mfano, uhusiano wa kwa baba na mama una nguvu zaidi kuliko uhusiano wa kwa baba tu, kwa hiyo, asaba wa kwa baba na mama ana haki ya kurithi kuliko asaba wa kwa baba tu.



Tumefahamu kwamba asaba hana fungu, bali huchukua urithi wote kama hakuna mwenye fungu, au huchukua kilicho bakia baada ya wenye mafungu kuchukua chao au hukosa kabisa kama hakuna kilicho bakia au wakati mwingine asaba wenye daraja sawa na mwenye fungu, watashirikiana fungu hilo. Kwa mfano: Amekufa mtu akaacha mume, mama, ndugu wa kwa mama zaidi ya mmoja na ndugu wa kwa baba na mam




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 2288

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani    👉2 Kitabu cha Afya    👉3 Bongolite - Game zone - Play free game    👉4 Simulizi za Hadithi Audio    👉5 Dua za Mitume na Manabii    👉6 web hosting   

Post zinazofanana:

Maana ya mirathi katika uislamu

Post hii itakufundishabkuhusu mirathi ya kiislamu, maana yake.

Soma Zaidi...
Tarstibu za kulipa swaumu ya Ramadhani

Hapa utajifunza namna ambayo utatakiwa kulipa funga ya Ramadhani kwa siku ambazo hukufunga

Soma Zaidi...
Nini kifanyike baada ya mazishi ya kiislamu

Huu ni utaratibu unaotakiwa kufanyika baada ya kuzika.

Soma Zaidi...
Sunnah za swaumu, sunnah ambazo zinaambatans ns kufungabmwezi wa Ramadhani

Yajuwe mambo ambayo yanapendeza kuyafanya wakati ukiwa umefunga Ramadhani.

Soma Zaidi...
Maana ya uadilifu na usawa na tofauti zao

Posti hii itakwenda kukufunza utofauti kati ya uadilifu na usawa

Soma Zaidi...
Namna ya kuosha maiti hatua kwa hatua

Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...