Haki na wajibu kwa jirani
Wajibu kwa Jirani
Pamoja na kuwajibika kutekeleza haki mbali mbali kwa wanafamilia tunawajibika vile vile kuwatendea wema majirani zetu wakiwa waislamu au katika dini nyingine. Qur-an inasisitiza:
"... Na wafanyieni ihsani wazazi wawili, jamaa, yatima, maskini najirani waliokaribu najirani walio mbali na rafiki walio ubavuni mwenu..." (4:36)
Mtume wa Allah (s.w) ametuusia juu ya suala Ia kuwafanyia ihsani jirani kwa uzito mkubwa kama tunavyojifunza katika Hadith zifuatazo:
"Anas(r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: "Yule ambayejirani yake hasalimiki kutokana na ukorofi wake, hataingia peponi." (Muslim)
Aysha na Ibn 'Umar (r. a) wameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: "Jibril hakuacha kunihimiza juu ya jirani mpaka nikahisi kuwa si muda mrefujirani atafanywa kuwa mrithi." (Bukhari na Muslim)
Katika hadith iliyosimuliwa na lbn Mas'ud (r.a) Mtume (s.a.w) amesikika akisisitiza:
"... Naapa kwa yule aliyeshikilia maisha yangu mkononi mwake, mtu hatakuwa Muislamu wa kweli mpaka moyo wake na ulimi wake viukiri Uislamu, na hatakuwa muumini wa kweli mapaka jirani yake asalimike na kero zake." (Ahmad)
Pia Mtume (s.a.w) anatufahamisha kuwa kipimo cha mtu kuwa ni mwema au ni mbaya ni jirani zake kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:
Ibn Mas 'ud (r.a) ameeleza kuwa mtu mmoja alimuuliza Mtume wa Allah: "Ee Mtume wa Allah! Nitatambuaje kuwa nimefanya mazuri na nitajuaje kuwa nimefanya mabaya?" Mtume (s.a.w) alimjibu: "Utakapowasikia majirani zako wakisema umefanya vizuri," basi umefanya vizuri na utakapowasikia wakisema - umefanya vibaya basi umefanya vibaya. Huu ndio ukweli kwa sababu majirani wako karibu sana na wewe na kwa hiyo wanaijua vema tabia yako.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitabu cha Afya 👉2 Dua za Mitume na Manabii 👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉4 Bongolite - Game zone - Play free game 👉5 kitabu cha Simulizi 👉6 Kitau cha Fiqh
Post zinazofanana:
Hawa ndio wanaoruhusiwa kurithi
Hii ni orodha ya watu ambao wanaweza kurithi malibya marehrmu.
Soma Zaidi...Mwenendo wa mwenye kunuia hijjah na umrah
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Zijuwe aina kuu 6 za talaka katika uislamu
Talaka zimegawanyika katika makundi mengi. Katika somo hili utakwenda kukifunza aina kuu za talaka katika uislamu.
Soma Zaidi...Ni nini maana ya uchumi katika uislamu
Katikabuislamu dhana ya uchumi imetofautiana na dhana ya kidunia hivi leo ambapo kamari na riba ni moja ya vitu muhimu katika uchumi.
Soma Zaidi...Hizi ndio nyakati za swala tano na jinsi ya kuchunga nyakati za swala.
Posti hii inakwenda kukufundisha kuhusu jinsi yavkuchunga nyakatibza swala tano.
Soma Zaidi...