Haki na wajibu kwa mayatima

Haki na wajibu kwa mayatima

Wajibu kwa Mayatima



Yatima ni mtoto aliyefiwa na wazazi wake, hasa baba, kabla ya kufikia baleghe. Uislamu unatuhimiza kuwatendea wema yatima na kuwatunzia urithi wao kwa uadilifu mpaka wafikie baleghe yao na kuwa na akili ya kutunza mali.


"... Na wanakuulizajuu ya mayatima: Sema: Kuwatendea mema ndivyo vizuri. Na kama mkichanganyika nao (ndivyo vyema vile vile) ,kwani ni ndugu zenu..." (2:220)
Tunajifunza kutokana na aya hii kuwa tunatakiwa tuwatendee wema mayatima na tuishi nao katika familia kama tunavyoishi na watoto wetu. Kukaa nao pamoja kwa huruma na mapenzi kutawafariji na kuziba pengo Ia kufiwa na mzazi au wazazi wao. Si katika mwenendo wa Kiislamu kuwatenga mayatima kwenye makazi maalumu. Tuishi nao katika familia zetu na tuwasomeshe katika shule wanazosoma watoto wetu.



Kuwanyanyasa mayatima ni katika madhambi makubwa mbele ya Allah (s.w). Si muumini wa kweli yule anayemnyanyasa yatima kama tunavyojifunza katika Qur-an:


".Je, umemuona yule anayekadhibisha dini (asiyeamini malipo ya akhera)? Huyo ni yule anayemsukuma (anayemnyanyasa) yatima." (107:1-2)



Msisitizo wa kuwatendea wema mayatima pia tunaupata katika hadith zifuatazo:
Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: "Kaya (familia) bora kuliko zote ni ile ambamo anatendewa wema yatima; na kaya mbovu kuliko zote ni ile ambamo ananyanyaswa yatima." (Ibn Majah)



Sahl bin Sa 'ad (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: 'Mimi na yule anayemlea yatima (kwa wema), akiwa wa kwake au kwa wengine, tutakuwa naye peponi kama hivi - akionyesha kidole cha mwanzo (cha shahada) na kinachofuatia (cha kati) huku vikiwa vimeshikamana bila ya kuachana mwanya wowote ". (Bukhari)
Kuwatendea wema mayatima ni pamoja na kuwatunzia mali zao za urithi kwa uadilifu kama inavyosisitizwa katika Qur-an:


"Na wapeni mayatima mali zao. Wala msibadilishe kibaya kwa kizuri. Wala msile mali zao pamoja na mali zenu. Hakika (yote) hayo nijukumu kubwa." (4:2)



Na wajaribuni mayatima (wanapokuwa karibu ya kubaleghe kama wataweza kutumia fedha zao vizuri wakati watakapobaleghe. Wajaribuni kidogo kidogo) mpaka wafike wakati wa kuoa (kubaleghe). Kama mkiwaona wana akili njema, wapeni mali zao. Wala msizile kwa fujo na kwa haraka ya kwamba watakua (wazitake; hebu tuzile upesi). Na mwenye kuwa tajiri basi ajiepushe (na kuchukua ujira katika kuwafanyia kazi zao). Na atakayekuwa mhitaji basi ale kwa namna inayokubaliwa na Sharia. Na mtakapowapa mali zao, basi wawekeeni mashahidi (/uu ya kuwa Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi. (4:6)


Hakika wale ambao wanakula mali ya mayatima kwa dhuluma, bila shaka wanakula moto matumboni mwao; na wataungua katika huo Moto (wa Jahannam) uwakao. (4:10)
Kutokana na aya hizi tunahimizwa kutunza mali za mayatima mpaka watakapofikia umri stahiki ndio tuwakabidhi. Kama tuna uwezo tusitumie chochote kutokana na mali hiyo katika kuwalea. Kama hatuna uwezo tunaruhusiwa tuitumie katika kuwapa mahitaji ya lazima kama vile Elimu, mavazi, n.k; lakini vile vile kwa tahadhari na ungalifu.




                   




Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 176


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

hizi ndio nguzo za swala, swala za faradhi na suna
Soma Zaidi...

ihram na nia ya Hija na Umra
1. Soma Zaidi...

DUA 85 - 93
SWALA YA MTUME 85. Soma Zaidi...

BAADHI YA DUA ZA KILA SIKU
BAADHI YA DUA ZA KILA SIKU. Soma Zaidi...

TAREKH, HISTORIA NA SIRA YA UISLAMU NA MTUME MUHAMMAD KUTOKA KUZALIWA MPAKA KUFARIKI NA HARAKATI ZAKE
1. Soma Zaidi...

jamii
Soma Zaidi...

Kuamini siku ya mwiho: Pia utajifunza kuhusu maisha ya barzakh (kaburini), siku ya qiyama
Soma Zaidi...

Kwa Nini Mwanaadamu Hawezi Kuunda Dini Sahihi ?
1. Soma Zaidi...

HARUSI YA ALADINI NA BINTI SULTANI
Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII SHUAIB
Soma Zaidi...

Sababu za kushuka kwa surat al-Fiil
SURAT AL-FIILSura hii imeteremshwa Makkah na ina Aya Sita pamoja na Basmallah. Soma Zaidi...

Kushuka na kuhifadhiwa kwa quran, hatua kwa hatua: mafunzo ya baadhi ya sura za quran
QUR'AN 5. Soma Zaidi...