Taratibu na namna ya kutafuta mchumba na sifa za mchumba

Taratibu na namna ya kutafuta mchumba na sifa za mchumba

Kuchagua Mchumba



Jambo Ia kwanza katika kuendea taratibu za kukamilisha ndoa ya Kiislamu ni kuchagua mchumba. Katika kuchagua mchumba, Mtume (s.a.w) anatunasihi katika hadithi ifuatayo:



Abu Hurairah amesimulia kuwa: Mtume (s.a.w) amesema: 'Mwanamke anaolewa kwa vitu vine: kwa utajiri wake, hadhi yake, uzuri wake wa sura na kwa dini yake (Uchaji-Mungu wake). Mchague yule mwenye msimamo mzuri wa dini " (Bukhari na Muslimu)



Hadithi hii inatufahamisha kuwa vitu vinavyoweza kuwa vichocheo vya mtu kumchagua mchumba ni hivyo vinne vilivyotajwa, lakini Mtume (s.a.w) anatusisitizia tukifanye kichocheo cha dini kiwe namba moja kisha ndio vifuatie hivyo vingine. Ukweli ni kwamba mke mcha-Mungu atatii amri za AIIah(sw) na Mtume wake ambazo zitampelekea kumtii na kumheshimu mumewe. Halikadhalika, mume mcha-Mungu, atamtii Allah (s.w) na huchunga mipaka aliyomuwekea, jambo litakalompelekea kumhurumia mkewe na kumtendea haki inavyostahiki. Hivyo, maisha ya wacha-Mungu hawa katika familia yatakuwa ni yale ya kuhurumiana, kusaidiana na kushirikiana katika kuilea na kuiendeleza familia katika misingi ya ucha-Mungu.



Pia katika suala Ia kuchagua mchumba mtume (s.a.w) anazidi kutuasa katika hadithi ifuatayo:
Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) amesema "Utakapochumbiwa na mwanamume unayempenda kwa dini (ucha-Mungu wake) basi kubali uolewe naye. Kama hutafanya hivyo patakuwa na huzuni na vurugu katika ulimwengu.


Msisitizo wa kuwaoa wanawake wacha-Mungu au kuolewa na wanaume wacha-Mungu uko bayana katika Qur-an kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:


Wala msiwaoe wanawake makafiri mpaka waamini. Na mjakazi mwenye kuamini ni bora kuliko muungwana kafiri, hata ingawa kakupendezeni. Wala msiwaoze wanaume makafiri (wanawake Waislamu) mpaka waamini. Na mtumwa mwenye kuamini ni bora kuliko muungwana kafiri, hata akikupendezeni. Hao makafiri wanaitia kwenye moto. Na Mwenyezi Mungu anaitia kwenye Pepo na Samahani, kwa amri yake. Naye hueleza aya zake kwa watu iii wapate kukumbuka." (2:221)


Wanawake wabaya ni wa wanaume wabaya; na wanaume wabaya ni wa wanawake wabaya; na wanawake wema ni wa wanaume wema; na wanaume wema ni wa wanawake wema " (24:26)



Mwanamume mzinfu hafungamani ila na mwanamke mzinfu au mwanamke mshirikina; na mwanamke mzinfu hafungamani ila na mwanamume mzinfu au mwanamume mshirikina, na hayo yam eharamishwa kwa waislamu." (24:3)



Kutokana na aya hizi tunajifunza kuwa waislamu si tu wameharamishiwa kuwaoa au kuoelewa na makafiri na washirikina bali pia wameharamishiwa kuwaoa au kuolewa na watu wazinifu na waliozama katika maasi mengineyo hata kama watadai kuwa ni waislamu.La muhimu tunalopata hapa ni kuwa waumini wanatakiwa wawe makini katika kuchagua wachumba. Wazingatie wema na ucha-Mungu wa hao wanaowatarajia wawe wake au waume zao.



Na (mmehalalishiwa kuwaoa) wanawake wema wa Kiislamu na wanawake wema katika wale waliopewa kitabu kabla yenu, mtakapo wapa mahari yao na kufunga nao ndoa, bila ya kufanya uzinfu au kuwaweka vimada " (5:5)



Katika aya hii inatolewa ruhusa kwa wanaume wa Kiislamu kuwaoa wanawake wema wa ah-lal-kitaab ambao ni wanawake wema wa Kiyahudi na Kikristo kama inavyofafanuliwa katika Qur-an. Pametokea kutofautiana miongoni mwa wanazuoni wa Kiislamu juu ya ruhusa hii ya kuoa Ahlal-kitaab.



Kulingana na Sheikh Abdallah Saleh Alfarsy katika sherehe ya aya hii (5:5) ameeleza kuwa Mkristo aliyeruhusiwa kuoelewa na Muislamu ni yule tu ambaye ukoo wake umeingia katika dini hiyo kabla ya Uislamu haujaja.Amezidi kusisitiza Sheikh "Ama hawa wanaoitwa Misheni wanaoingia katika Ukristo sasa Si halali kuwaoa. ni haram wala ndoa haisihi".



Kulingana na maoni ya lbn Abbas (r.a), Muislamu anaweza kumuoa mwanamke wa Ahlal-Kitaabi aliye katika himaya ya Dola ya Kiislamu tu, na haruhusiwi kumuoa mwanamke wa Ahlal-Kitaabi ambaye yuko katika dola ambazo ni maadui wa Dola ya Kiislamu au yuko katika dola za Kikafiri. Tofauti na maoni haya ya lbn Abbas, Said bin Masayyab na Hassan Basri wanasema kuwa ruhusa hii ya kuwaoa wanawake wema wa Ahial-Kitabi imetolewa kwa ujumla.



leleweke kuwa kuwaoa Ahlal-Kitaabi si amri bali ni ruhusa kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w) kama ruhusa nyingine zilizotolewa katika Qur-an. Kuitumia ruhusa hii pasina haja na pasina kuzingatia malezi ya watoto katika misingi ya Uislamu ni hatari kubwa. Ikitokea mtu anaishi katika nchi ya Ahial-Kitabi na hana namna ya kumpata mwanamke mwema wa Kiislamu wa kumuoa, itakuwa kwake vyema kumuoa mwanamke mwema miongoni mwa hao Ahlal-Kitaabi badala ya kufanya uzinifu au kukaa na mwanamke bila ndoa. Ama pale ambapo kuna mabinti wema wa Kiislamu kuna haja gani ya kumuoa binti wa Kikristo? Jambo Ia msingi Ia kusisitiza hapa ni kwamba, aliyetoa ruhusa hii ni Mwenyezi Mungu (s.w), Mjuzi mwenye Hekima. Hivyo, kwa vyovyote vile kuna hekima kubwa katika ruhusa hii.



Ni haramu kwa wanawake wa Kiislamu kuoelewa na wanaume Wakristo au Mayahudi. Hivyo kwa mtazamo wa Kiislamu hapana ndoa kati ya mwanamume Mkristo au Myahudi na mwanamke Muislamu. Mtu atakayemwozesha binti yake kwa Mkristo, ajue wazi kuwa ameruhusu zinaa. Vile vile kwa waislamu ni haramu kushiriki katika sherehe za ndoa za namna hiyo kama ilivyo haramu kushiriki katika sherehe zote za kidini za Makafiri, Washirikina na Ahlal-Kitaabi. Kusherehekea pamoja nao, moja kwa moja, ni kuwaunga mkono katika hayo wanayosherehekea kinyume na Mwenyezi Mungu (s.w).




                   




Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 340


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Sifa na vigezo vya dini sahihi
1. Soma Zaidi...

Mambo gani ni Haramu kwa mwenye janaba?
Hadathi ya kati na kati (Janaba). Soma Zaidi...

Sera ya uchumi katika Uislamu
4. Soma Zaidi...

KUCHIMBWA UPYA KWA KISIMA CHA ZAMZAMA NA KUNYWA MAJI YA ZAMZAMA KISIMA KILICHO BARIKIWA
KUCHIMBWA UPYA KISIMA CHA ZAMZAMKwa kifupi ni kuwa Abdul-Muttalib alipata agizo kutoka ndotoni kuwa achimbe kisima cha zamzam, na akaelekezwa sehemu ya kupachimba. Soma Zaidi...

MJADALA JUU YA NDOA YA MTUME S.A.W NA BI KHADIJA (HADIJA)
LAKINI UMRI WANGU MKUBWABaada ya kuwaza na kufikiri muda mrefu, bibi Khadija (Radhiya Llahu anha) akafikia uamuzi wa kutaka kuolewa na Muhammad (Swalla Laahu alayhi wa sallam). Soma Zaidi...

DUA 11 - 20
11. Soma Zaidi...

.Mazingatio muhimu katika uchumi wa Kiislamu
3. Soma Zaidi...

haki za mwanamke za kisiasa katika uislamu
Haki ya Kushiriki Katika Siasa. Soma Zaidi...

ukweli na sifa zake kwenye uislamu na sifa za mtu mkweli
Ukweli ni uhakika wa jambo. Soma Zaidi...

Maana ya Funga ya ramadhani kisheria na Aina za funga
Amesema mtume (s.a.w) kuwa Allah (s.w) amesema: kila amali ya mwanaadamu ni kwa ajili yake isipokuwa funga. Soma Zaidi...

kujiepusha na uongo na sifa za uongo
Uwongo ni kinyume cha ukweli. Soma Zaidi...

Quran haikuchukuliwa kutoka kwenye biblia
Soma Zaidi...