Taratibu za kumuona mchumba

Taratibu za kumuona mchumba

Taratibu za kumuona mchumba

Ruhusa ya Wachumba Kuonana Kabla ya Ndoa



Pamoja na sifa ya ucha-Mungu na wema, tunatakiwa tuwaoe wanawake tunaowapenda kwa sura na umbo; hivyo hivyo wanawake nao wachague wanaume wanaowapenda kwa sura na umbo ili kuzidisha mapenzi na upendo baina yao katika familia. Kwa mantiki hii Mtume (s.a.w) ameruhusu wachumba kuonana kabla ya kufunga ndoa kama tunavyojifunza katika hadithi zifuatazo:



Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa mwanamume mmoja alikuja kwa Mtume (s.a.w) akasema: "Ninakusudia kumuoa mwanamke miongoni mwa answari." Akasema Mtume


(s.a.w), 'Mwangalie kwanza kwa sababu kuna dosari katika macho ya Answari." (Muslim)



Jabir (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) amesema: "Mmoja wenu atakapochumbia, na akawa na uwezo wa kumtazama yule anayemchumbia na afanye hivyo." (Bukhari na Muslim)



Pamoja na ruhusa hii, bado waislamu wanalazimika kuendelea kuzingatia mipaka ya "Hijaab", kwamba hawaruhusiwi kukaa faragha au kutembea faragha mwanamke na mwanamume wasio maharimu.




                   


Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: General Main: Post File: Download PDF Views: 2031

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 web hosting     👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Dua za Mitume na Manabii     👉5 Simulizi za Hadithi Audio     👉6 Bongolite - Game zone - Play free game    

Post zinazofanana:

DARSA ZA TAWHID

Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala

Soma Zaidi...
Umuhimu wa ndoa na kuoa ama kuolwa katika jamii

Matamanio ya jimai ni katika maumbile na hayaepukiki.

Soma Zaidi...
fadhila za sura kwenye quran

FADHILA ZA BAADHI YA SURA Umuhimu na ubora wa baadhi ya sura na aya.

Soma Zaidi...