fangasi wa kwenye Mdomo na koo
fangasi wa kwenye Mdomo na koo
- Fangasi hawa wa kwenye mdomo watambulikao kama thrush ama oropharyngeal candidiasis wanaweza kuishi kwenye koo na tundu zima la koo kuelekea kwenye tumbo na hawa wanajulikana kama esophageal candidiasis ama candida esophagitis. Fangasi hawa ni maarufu sana kwa watu wanaoishi na HIV ana UKIMWI.
Dalili za fangasi hawa
- Kuwa na madoa meupe kwenye sehemu ya ndani ya shavu, ulimi, sehemu ya juu ya mdomo, na koo.
- Unahisi kama kuna pambai kwenye mdomo
- Kupetea kwa ladha ya unachokila
- Maumivu wakati wa kula ama kumeza
- Kupasuka na kuwa wekundu kwenye kona za mdomo
Walio hatarini kupata fangasi hawa:
Fangasi hawa si kawaida sana kuwapata watu wenye afya madhubuti. Ijapokuwa wapo watu ambao wapo hatarini sana kupata fangasi hawa kama watoto chini ya umri wa mwaka mmoja, na watu wenye matatizo ya kiafya kam wenye:-
- Watu wanaotumia meno bandia
- Watu wenye kisukari
- Watu wenye saratani
- Watu wenye HIV ama UKIMWI
- Watu wanaotumia dawa amazo zinakausha mdomo
- Watu wanaovuta sigara.
- Watu wanaotumia dawa za kupulizia za pumu
Njia ya kupambana na fangasi hawa:
Wengi wanaopata fangasi hawa ni wale ambao mfumo wao wa kinga umeathirika hivyo miili yao haiwezi kupambana vyema na mashambulizi. Hivyo kupambana na fangasi hawa hakikisha unaweka mwili wako katika hali njema ya kiafya. Muone daktari akuelekeze namna ya kuboresha afya yako. Pia piga mswaki kila unapotumia dawa ya kupulizia ya pumu. Wacha kuvuta sigara.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 web hosting 👉2 Dua za Mitume na Manabii 👉3 Bongolite - Game zone - Play free game 👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉6 kitabu cha Simulizi
Post zinazofanana:
Namna ya kuepuka Ugonjwa wa ngiri.
Posti hii inahusu zaidi namna au njia za kuepuka na Ugonjwa huu wa ngiri ambao uleta madhara kwa watoto, vijana na watu wazima, kwa hiyo ili tuweze janga hili ni lazima tufanye yafuatayo.
Soma Zaidi...Maziwa ya mama: Faida zake kwa afya ya mtoto.
Maziwa ya mama, yanayojulikana kitaalamu kama "dhahabu nyeupe," ni chakula kamili na cha kipekee chenye virutubisho vyote vinavyohitajika na mtoto katika miezi sita ya kwanza ya maisha yake. Yanatengenezwa na mwili wa mama kulingana na mahitaji halisi ya mtoto, yakibeba kingamwili, vitamini, na madini muhimu. Makala hii inaangazia faida za kipekee za kunyonyesha kwa afya ya muda mfupi na mrefu ya mtoto.
Soma Zaidi...Dalili za saratani ya kibofu Cha nyongo
Saratani ya kibofu cha nyongo ni Saratani inayoanzia kwenye kibofu cha nyongo. Nyongo yako ni kiungo kidogo, chenye umbo la peari upande wa kulia wa tumbo lako, chini ya ini lako. Kibofu cha nyongo huhifadhi nyongo, Kioevu cha usaga
Soma Zaidi...Homa za mara kwa mara: Chanzo chake na nini cha kufanya.
Homa sio ugonjwa; ni silaha ya mwili wako. Inapopanda, inamaanisha mfumo wako wa kinga unawaka moto kupambana na adui aliyepo ndani. Lakini, je, inakuwaje unapopata homa hizo mara kwa mara? Homa za mara kwa mara ni kengele ya onyo kwamba kuna kitu hakiko sawa ambacho hakijatibiwa kikamilifu. Makala haya yanakusaidia kutambua nini cha kufanya ili kuondokana na mzunguko huu wa maumivu
Soma Zaidi...​Dalili za Upungufu wa Damu kwa Watoto
​Upungufu wa damu ni hali inayotokea pale mwili unapokosa chembechembe nyekundu za damu za kutosha. Post hii inatoa mwongozo kwa wazazi kutambua viashiria muhimu ili kuwasaidia watoto
Soma Zaidi...Dalili za Mimba Kabla ya Kipimo:
​Kipindi cha kusubiri ili kufanya kipimo cha mimba kinaweza kuwa na msisimko na wakati mwingine wasiwasi. Makala hii inakupatia mwongozo wa ishara za awali ambazo mwili wako unaweza kuzionyesha kabla hata ya kupata majibu ya vipimo vya maabara au vya nyumbani.
Soma Zaidi...