Habari za leo ndugu zangu mimi Ni dalili zipi hasa za awali zinazoashiria umeambukizwa ukimwi

Anataka kujuwa dalili za awali za kujuwa kuwa umeathirika na UKIMWI

Habari za leo ndugu zangu mimi ni (Jina limehifadhiwa)  ninataka kujua ni dalili zipi hasa za awali zinazoashiria umeambukizwa ukimwi. 

 

Jibu

Ni vizuri kwanza upate vipimo,  ama uonane na mhudumu wa afya upate kujifunza kuhusu afya yako.

 

Dalili za awali za kuambukizwa virusi vya ukimwi zinafanana na dalili ya maradhi mengineyo hivyo unawwza kuona dalili hizi kumbe ni maradhi mengine tu. 

 

Dalili za awali ni kama: 

1. Maumivu ya kichwa

2. Kuvimba kwa tezi za kwapa, mtoki na shingoni

3. Mafua na homa

4. Kupatwa na vipele

5. Uchovu wa mwili

 

Dalili hizi hutokea wiki ya pili hadi ya sita toka kuambukizwa na hazitarudi tena baada ya hapo. Kama utakuwa umeambukizwa virusi vitaendeleabkuathiri kinga ya mwili kimya kimya bila ya kuonyesha dalili yeyote kwa muda wa miaka kadhaa. Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/12/22/Thursday - 10:29:41 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 633


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-