Hadithi hii inahusu hasara za wivu na kutokuwa wazi

Posti hii inahusu zaidi hasara za wivu, kwa sababu ya kuwepo kwa marafiki wasio waaminifu wanasababisha kuharibiana maisha bila kujua kwa sababu ya kuonekana wivu na kutokuwa wazi.

Hasara za wivu na kutokuwa wazi.

1. Palikuwepo na wasichana wawili marafiki sana na waliofahamika pia kwa wazazi wao kuwa ni marafiki majina ya wasichana hao ni lisa na Lina ,urafiki wao ulitokana na wazazi wao waliishi sehemu moja na watoto hao walikua wanapendana kwa sababu ya wazazi wao pia walikuwa marafiki.

 

 

 

2.Watoto lina na Lisa wakiwa na miaka mitano walipelekwa kuanza chekechea walipelekwa na mama Lisa kuandikishwa kwa sababu ya kuzoeaana lina hakuona shida kwamba amepelekwa na mama Lisa shule kwa sababu alimwona kama mama yake pia, kwa hiyo mama Lisa aliwaandikisha na akawaacha pale shule na wakati wa kuondoka waliweza kurudi nyumbani kwa sababu hapakuwa mbali.

 

 

 

 

3. Siku zilienda na watoto hao wakawa wanasoma shule na matokeo yao yalikuwa mazuri mno na walikuwa hawaachani kila sehemu ukimwona lina kuna Lisa,na waalimu waliwapenda sana kwa sababu ya urafiki wao, nidhamu na pia ufaulu wao na kwa sababu walikuwa wadogo hawakuona shida kuishi na kupendana na kusaidiana katika kila kitu hasa kusoma pamoja na kucheza pamoja.

 

 

 

 

 

4. Basi watoto hao walipofika darasa la sita wakaanza kukua kimwili na kuanza kuwa na hisia hali ambayo iliwafanya kuwa tofauti kidogo kwa sababu palikuwepo na wanachuo wa mazoezi yaani kwa kitaalamu huitwa wanachuo wa field, yaani wale waliokuja kufanya mazoezi shuleni, mmoja kati yao akaanza mahusiano na Lisa ila Lisa hakumwambia lina na lina aliona kila kitu kinachoendelea kwa hiyo Lisa akapunguza kutembea na lina kwa sababu akihofu anaweza kumwambia mama yake.

 

 

 

 

5. Siku zikaendelea na Lisa akafanya mtihani akawa mtoto wa thelathini kati ya mia moja na siku zote alikuwa mtoto wa kwanza au wa pili walikuwa wanapisha na lina ,ila lina siku hiyo akawa wa kwanza mama Lisa akashangaa sana na alikuwa ameshashutuka kwa sababu Lisa alikuwa hana mahusiano mazuri na lina na siku hizo walikuwa hawasomi wala kucheza wote kama mwanzo, basi mama Lisa akaamua kwenda shule kwa waalimu kuuliza waalimu wakamwambia aende kwa lina atapata jibu kamili na waalimu walijua kila kitu ndipo mama Lisa akaenda kwa mama lina kupata jibu kamili.Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/08/23/Tuesday - 07:58:29 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 624


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Hadithi ya chongo wa tatu mtoto wa mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Hatima ya kijana mchonganishi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Hadithi iliyosimuliwa na mshona nguo
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

USALITI (sehemu ya kwanza)
Post hii inahusu zaidi vijana wawili ambao ni msichana na mvulana walioingia kwenye mahusiano wakiwa sekondari na wakahaidiana kuoana ila kwa sababu mbalimbali walizokutana nazo kwenye safari yao ya mahusiano mmoja akamsaliti mwingine na kusababisha kupo Soma Zaidi...

Muendelezo wa hadithi ya mshona nguo
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Utajiri wa baba na kifo chake
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

NIMLAUMU NANI part 1
Post hii inahusu hadithi Moja ya kijana maaalufu aliyeitwa Frank, ni kijana aliyekuwa mwaminifu ila amekumbana na wasichana wengi wanamasaliti ukizingatia Frank alikuwa kijana mstaalabu na mwaminifu sana ila anafikia kufanya maamuzi magumu kufuatana na ku Soma Zaidi...

Matibabu ya vidonda sugu
Some Hili linakwenda kukueleza kuhusu matibabu ya vidonda vya tumbo sugu Soma Zaidi...

Ndani ya pango la makaburi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

Kwanini vidole gumba vilikatwa
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa y Soma Zaidi...

Ndoto ya mgonjwa, binti mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Kutokana kwenye kisima mpaka kuwa mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...