HADITHI ILIYOSIMULIWA NA KIJAKAZI WA SULTANI


image


Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani


HADITHI ILIYOSIMULIWA NA MJAKAZI WA SULTANI

Mtukufu sultani, nakwenda kukusimulia tukio lililotokea leo hii wakati tulipokuwa tunaburudika. Tulikuwa tupo kwenye tafrija moja hivi jana wakati wa jioni kabla ya juwa kuzama. Katik tafrija hiyo tulipata kusikiliza usomaji wa quran kwa sauti nzuri sana hata machozi yakatutoka. Baada ya hapo tukabahatika kusikiliza mashiri. Mshairi maarufu kutokea India alikuwepo, na alighani kwa sauti njema sana.

 

Baada ya burudani kuisha ndipo tukaletewa chakula kizuri sana. Vyakula vya kuoka, na nyama iliyo kaushwa vizuri ililetwa bele ya hadhara. Vinywaji vilivyo vizuri vikahudhurishwa mbele yetu. Basi tulikaa vikundi vikundi kuzunguruka sahani za vyakula. Katika kundi nililokaa nilikuwa na aliyekuwa na shughuli yake siku ile. Na hapa kitu cha kushangaza ndipo kikatokea.

 

Katika vyakula vilivyoletwa kulikuwepo na zerbajeh. Hiki ni chakula zilichotengenezwa kwa mchanganyiko wa vyakula kadhaa na matunda. Chakula hiki unapokila harufu yake inaweza kukaa kwa muda wa siku nzima kwenye mikono. Ni chakula kitamu na kipendwacho na watu wa Baghadad. Basi ghafla mwenzetu mmoja alipoona chakula kile akaanza kutetemeka na kutokwa na majasho kana kwamba ameona kitu cha kutisha sana.

 

Yule bwana hakutaka hata kula chakula kile. Sikuwa na wasiwasi sana nikajuwa lamda hali chakula kile, ama lamda kuna mtu anamdai ndio maana akapata woga. Wakati tunakula nikamuona yule bwana kidolechake gumba kimekatwa. Alipokuwa nakata nyama, nikagundua vidole vyake gumba vya mikono vyote vimekatwa. Hapo nilishindwa kujizuia kuwa na shauku, nikataka kumuuliza kulikoni. Lakini ikabidi nimsubiri amalize kula.

 

Kumbe wakati ule hata yule mwenye shughuli yake alikuwa anashuhudia yanayotokea. Alikuwa akinisubiri nianza kuuliza. Kwa kuwa yeye ndiye mwenye shughuli isingekuwa vyeka kumkera mgebi wake. Ndipo naye akasubiri amalize kula ili amuulize. Yule bwana alipomaliza kula nikamuuliza “ndugu yangu nimeona hata huugusa chakula hiki “zerbajeh” ama hukupendi” naye akajibu “ninakipenda ila baada ya kula ni lazima nioshe mikono yangu mara 40 kwa maji, mara 40 kwa alita na mara 40 kwa sabuni. Sasa vitu hivi hapa havipo na si vyema kusumbuwa watu kwenye shughuli hii”

 

Kwa shauku zaidi nikamuuliza ana nini hasa. Ndipo akanieeza kuwa chakula hiki ndio sababu ya yeye kukatwa vidole gumba vya mkono wake. Kisha akatuonyesha na vidole kumba vya miguu yake, pia vimekatwa. Hapo nikapata shauku zaidi kujuwa hasa kwa nini amekatwa vidole gumba vyake vyote vinne kwa sababu ya chakula tu.

 

Wakati mazungumzo yetu haya yanaendelea yule bwana Mansur mwenye shughuli yake alikuwa anasikiliza. Basi akaagizwa kuletwe ndoo mbili za maji, sabuni na alita. Hapo kopo la kunawia na alita zikaandaliwa kwa ajili ya kutoa povu vyema. Kisha ikaletwa tena sahani yenye zerbajeh. Akaambiwa ale kisha atanawa kama anavyotaka. Basi akala vyema akanywa maji na kumshukuru Mungu. Kisha akaanza kunawa na alita mara 40 kisha sabuni mara 40 kisha maji mara 40. alipomaliza tukamtaka atusimulie hadithi yake ndipo akasimulia hadithi ifuatayo:-



Sponsored Posts


  πŸ‘‰    1 Magonjwa na afya       πŸ‘‰    2 Madrasa kiganjani       πŸ‘‰    3 Hadiythi za alif lela u lela       πŸ‘‰    4 Maktaba ya vitabu       πŸ‘‰    5 Mafunzo ya html kwa kiswahili       πŸ‘‰    6 Mafunzo ya php    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Hadithi ya aliyekatwa vidole gumba
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

image Safari ya saba ya Sinbad
Posti hii inakwenda kukuletea muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

image Hadithi katika kijiji cha burugo
Β Posti hii inahusu zaidi jinsi ya watu walivyoishi katika kijiji cha burugo .tunajuwa hadithi ni sehemu mojawapo ya kubirudisha na kujifunza kitu flani kutoka kwenye jamii . Soma Zaidi...

image Hadithi ya mzee wa kwanza na mbuzi wake
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Kisa Cha mfugaji na mkewe
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Hadithi ya Binti mfalme
Posti hii inahusu zaidi hadithi ya Binti mfalme ni hadithi ya kusisimua, kuhusu hadithi hii ni kwamba mfalme alihitaji mtoto wa kiume ila wanawake wote hawakumpata ila alitokea mke mdogo mmoja wa mfalme akajifungua watoto wawili mapacha mmoja wa kiume na mwingine wa kike ila wa kike alifichwa akaletwa wa kiume na WA kiume alipofikia wakati wa kuoa alimpenda sana yule pacha wake bila kujua kwamba alikuwa ndugu yake. Soma Zaidi...

image Hadithi ya binti mwenye kufichwa mtoto wa mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Hadithi ya kinyozi msiri wa mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Kwanini dirisha moja?
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

image Hadithi ya mji uliogeuzwa mawe
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...