Hadithi ya binti mwenye kufichwa mtoto wa mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela
HADITHI YA BINTI MWENYEKUFICHWA, MTOTO WA MFALME.
Juwa ewe mwenye kuja kwa jina la Habili kwa cheo cha mchanja kuni kuwa mimi ni mtoto wa mfalme niliyetambulika kwa uzuri na hta mawaziri na watoto wa wafalme wakawa wanagombana kwa kutaka kunipata kuwa mke wao. Ugovi huu ulikuwa mkali hata ukaingiliwa na viumbe visivyo onekana navyo vikataka kunioa nao ni maini waliombali na rehema za Mwenyezi mungu.
Nyumbani kwetu kulikuwana kisima kilichoaminika kuwa ni cha muda mrefu kisichopungua umri wa miaka 150. katika kisima hiki kijana wa kijini alichikuwa madaraka ya kutawala majini waliopo kwenye kisima kile. Siku ile nilikwenda kuchota maji kisimani pale nikiwa kichwa changu kipo wazi kinyume na maamrisho ya dini yetu. Bila ya kutambua unywele wangu mmoja uliangukia kwenyekisima kile na kumganda kiongozi mpya a majini alipokuwa akipewa majukumu.
Nilirudi nikiwa na mabadiliko katika kichwa changu hata ndoo ya maji niliiona n nzito sana kuibeba hivyo nikatumia mikono yangu kubeba maji yale. Siku ile sikupata usingizi kwa maumivu ya kichwa na nilipopata usingizi nilshituka kwa ndoto za kutisha nilizokuwa ninazipata. Sikujuwa chanzo cha matatizo haya yote. Ilipofika asubuhi nilimueleza baba yangu ju ya maumivu ya kichwa changu. Baba alimwita daktari wetu na kuanza kunitibia. Kwa muda wa siku 5 sikupata nafuu zaidi ya maradhi yaliyokuwa yakinizidia.
Kwa muda wa miezi waganga na madaktari wote walishindwa kutibu ugonjwa wangu. Ilifikia hali kuwa mbaya hata nikawa sinafahamu juu ya niayofanya, unaweza kusema nilikuwa mkichaa ambaye akili zinaingia na kutoka. Hali hii ilimpa baba yangu wakati mgumu hata akafikiri ni maradhi yaliyosababishwa na wale wachumba wliokuwa wakinigombania. Habari za ugonjwa wangu zilienea nchi nzima na kila mtaalamu wa tiba alikuja kujaribu bahati yake kwani donge nono liliahidiwa kwa atakayenitibu.
Miezi sita ilifika na habari za ugonjwa wangu zikaenea nchi za majirani. Baba alifikia hatua akatangaza kwa yeyote aatakayenitibu ataniozesha nae. Jambo hili lilisababisha hata wataalamu wa ta kutoka nchi za jirani wa lengo la kunioa pindi wakifanikiwa kunitibu. Bila ya mafanikio yeyote juu ya ugonjwa wangu ijapokuwa wapo walofaniukiwa kunipa nafuu lakini haichukui muda kabla ya ugonjwa kunizidia.
Siku niliota ndoto ya kushangaza. Ndoto hii nilipomwambia baba alijaribu kuwauliza wataalamu wenye kujuwa tafsiri za ndoto. Basi akaja mtaalamu na akaniambia nimueleze ndoto ile bila hata ya kuacha hata sehemu ndogo. Basi nilikaa kimya kwa muda kisha nikakusanya mawazo yangu na kuanza kumuelezea ndoto yangu kama ifuatavyo;-
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉2 Kitau cha Fiqh 👉3 Kitabu cha Afya 👉4 Simulizi za Hadithi Audio 👉5 Madrasa kiganjani 👉6 web hosting
Post zinazofanana:
HADITHI YA KISIWA CHA MAWE YANAYOLIA
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YAKISIWA CHA MAWE YANAYOLIA.
Soma Zaidi...HADITHI YA CHONGO WATATU NA WANAWAKE WA BAGHADAD
Download kitabu Hiki Bofya hapa HATITHI YA CHONGO WATATU WATOTO WA WAFALME NA WANAWAKE WA BAGHDAD Hapo zamani katika nchi ya Baghdad kulikuwepo na mbeba mizigo maarufu sana.
Soma Zaidi...Kuelekea bonde la uokozi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad
Soma Zaidi...MALIPO YA WEMA NI WEMA
Download kitabu Hiki Bofya hapa MALIPO YA WEMA NI WEMA Basi baada ya kupita kwa muda Zubeidaha akapewa chai na chakula safi na akawekwa kwenye kiti kilicho kizuri na akaambiwa msubiri atakuja sasa hivi.
Soma Zaidi...Hadithi ya chongo watatu wa mfalme na wanawake wa Baghdad
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela
Soma Zaidi...