HADITHI YA KAKA WA PILI WA KINYOZI


image


Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani


HADITHI YA KAKA WA PILI WA KINYOZI

Kaka yangu wa pili alikuwa ni mtu wa maneno mengi sana. Alikuwa ni masikini lakini ni mcheshi sana. Watu wengi walimpenda wazee na watoto, vijana na mabinti. Kaka alikuwa ni maarufu sana kwenye kitongoji alichokuwa akiishi. Kulikuwa na shutuma kuwa kaka anatoka na wake wa wenzie. Ijapokuwa shutuma hizi hazikuwa ni za kweli lakini zilikuwa ni hatari. Na hii ni kutokana na maneno mengi ya kaka na ucheshi wake. Pia kaka hakuwa mtu mwenye tabia njema kama mimi na hakuwa ni mwenye kufanya ibada kama mimi.

 

Siku moja alikutana na bibi mmoja akamtaka wazungumze kidogo. Huyu ni bibi ambaye alikuwa ni mtu wa mtaani. Hakuwa akionekana sana wakati wa mchana. Hakuwa akijulikana sana na watu, na hakuwa akijulikana kazi yake wa la anapoishi. Ila kaka alikuwa akifahamiana na huyu bibi kwa kuwa walikuwa wakikutana mara kadhaa. Kwa kuwa kaka yangu alikuwa ni mtu wa maneno mengi aliweza kufahamiana na watu wengi. Basi katika mazungumzo bibi alimwambia kaka kuwa kuna itajiri atampatia maana amemuona ni mtu mcheshi na watu.

 

Bibi aliongeza kuwa amemchaguwa kaka kwa kuwa anaamini atakapokuwa tajiri ataweza kunufaisha watu wengi. Kaka alikubali mazungumzo ya bibi yule. Bibi akaongeza kumwambia kaka kuwa kunaq sharti moja tua nalo ni kufanya kila nitakacho kuambia mimi tu na usiniulize swali lolote. Kwa kuwa kaka alipenda utajiri na alitaka kuwa tajiri alikubali sharti hili bua hata ya kuuliza maana yake. Baada ya mazungumzo ya bibi na kaka waliondoka kwa pamoja na kuelekea kwenye kutafuta utajiri.

 

Wakaenda mpaka katikati ya mji wakaingia kwenye jumba mija kubwa sana. Ijapokuwa kaka alikuwa ni mwenyeji wa mji lakini hakupatapo kulifahamu jumba hili kama lipo hapa. Hakupata hata kuliona siku moja. Akamfuata bibi yule nyuma hata wakaingia ndani. Wakakaribishwa na manukato mazuri sana, harufu ilioje ya manukato hayo. Kaka alianza kujihisi yupo dunia ya maajabu. Alikaribishwa na wabinti wa mirika, uzuri ulioje wa wabinti hao. Ukumbi ulikuwa na mapambo ya dhahabu na mazuri mazri. Kwenye mkeka mkubwa ilio na mapambio mazuri alikaa mwanamke mmoja mzuri sana.

 

Wale wabinti watatu waliokuja kumpokea yule bibi pamoja na kaka walikaa pamoja nao. Wabinti walikaa mbele ya dada mkubwa. Yule mwanamke mkubwa na mrembo kuliko wote alinyanyuka na kumpiga kofi kubwa sana mgongoni. Kaka alikaribia kukasirika na kutoa maneno ya ukali, yule bibi akamtuliza kaka na kumwambia usisubutu kufanya chochote hata niwambie. Na hii ni ndogo yapo mengine mengi. Baada ya kuangaliana kwa muda kidogo yule mwanamke akaagiza aletewe mvinyo wa zabibu.

 

Alikunywa kwa muda kisha akawapa pamoja na wale wabinti wanywe. Baada ya kuanza kulewa wakaanza kumpiga mabao kaka pamoja na kumrusha rusha pale ndani kwenye makochi na masofa. Kaka alikaribia kukasirika na kurusha makonde, ila kwa bahati nzuri wakatulia. Kisha yule bibi akamfata kaka na kumwambia kuwa huyu mwanamke amekupenda, na yupo tayari kukupa utajiri wake wote. Ila kuna mambo mawili yamebaki, ila tambua hutapigwa tena. Jambo la kwanza unatakiwa unyolewe ndevuzako. Kaka alikataa lakini kwa kufikiria utajiri aliamua kuachana na ndevu ili apate utajiri.

 

Wakaja wabinti wawili na kuanza kumnyoa ndevu zake zote hata akawa kama mtoto asiye na hata maoteo ya ndevu. Walipomaliza kumnyoa wakampata mafuta mazuri na kumpulizia manukato. Kaka alikuwa ananukia sana. Kisha akapelekwa mbele ya yule mdada mkubwa. Yule dada alifurahi sana na akanyanyuka akaanza kushika kichwa za kaka. Kaka alijisikia raha sana, kisha yule mwanamke akachukuwa mvinyo na kuendelea kunywa. Yule bibi akamwambia kaka kuwa muda si mrefu huyu mwanamke ataanza kulewa, hivyo akinyanyua umfatilie nyma, akikimbia mkimbize mpaka atakkapoingia kwenye chumba akilala, utajiri wako utaanzia hapo. Ila hakikisha humkimbizi mpaka umkamate. Unatakiwa umfatilie nyuma nyuma, na usiwe naye karibu.

 

Basi kama alivyo sema yule bibi, haukupita muda yule dada akaanza kulewa na wale wabinti wawili wote wakaondoka. Kisha yule mwanamke akanyanyuka ghafla na anza kukimbia. Yule bibi akamkumbusha kaka kwa kumwambia usithubutu kumkamata, na kaa naye mbali ila usimpoteze. Kaka akaanza kumfatilia, mara aingie chumba hiki mara kile mara uani mara atoe maneno yasiyo eleweka, ilimradi karaha. Kaka akiwa ana kfatilia, ilifika wakati akaanza kukimbia kwa kasi na kaka akawa anamkimbia, akasahau kuwa ameambia wake naye mbali, kaka alimkimbiza hata akakaribia kumkamata, vile ataka kumkamata tu akaingia mlango wa uwani. Kaka alipoingia naye mlago wa uwani akajikuta yupo katikati ya mji na watu wengi wana mwangalia.

 

Kaka alikuwa maenyolewa ndevu, amepakwa rangi kichwani na amenyolewa nyusi. Nguo alizovaa zilikuwa kama za kituko vile. Watu walianza kumshangaa kaka na wengine kumtupia mawe. Nyumbaaliyotoea ilikuwa ni ya kiongozi wa serikali. Basi kaka akakamatwa na kupelekwa kwa kadhi. Hukumu ikatoka kaka apigwe fimbo nyingi na ahamishwe mji. Basi baada ya viboko vikali kaka akatiwa kwenye gari la punda na kuenda kutupwa mbali na mji. Nilifatilia na kumchukuwa kaka yangu. Haya yote yalimpata kutokana na maneno yake mengi na kuwa msahaulifu wa sheria. Sasa ninakwenda kukusimulia kilichomkuta kaka yangu wa tatau.



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    2 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    3 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    4 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    5 Jifunze fiqh       ðŸ‘‰    6 Maktaba ya vitabu    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image UFUPISHO WA ALIFU LELA ULELA KITABU CHA KWANZA
Posti hii inakwenda kukisimulia kuhusu hadithi za alifu lela ulela KITABU CHA KWANZA Soma Zaidi...

image Deni la mapenzi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

image Alif lela ulela
Posti hii inakwenda kukusimulia hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili
Posti hii inahusu zaidi hadithi ya vijana wawili ambapo mtihani unafika ila Jackie hakujiandaa alishutuliwa na marafiki zake baada ya kuona mwenendo wake haueleweki. Soma Zaidi...

image Safari ya nne ya Sinbad
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

image Hadithi ya binti wa kwanza na mbwa
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Safari ya saba ya Sinbad
Posti hii inakwenda kukuletea muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

image NIMLAUM NANI? (Sehemu ya pili)
Post hii ni mwendelezo wa hadithi iliyopita ambapo Frank aliwakuta Amina ambaye ni mpenzi wake ameumbatiana na James ambaye ni rafiki yake ,kwa hiyo tuendelee kusikia yaliyotokea baada ya Amina na James kukutwa na Franki. Soma Zaidi...

image Mahusiano ya vijana wawili
Posti hii inahusu zaidi mahusiano yaliyotokea kati ya vijana wawili ila yanafika baadae mmoja akamsaliti mwenzake. Soma Zaidi...

image Safari ya majibu juu ya maswali mawili
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...