Hadithi ya Kaka wa sita wa kinyozi

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani

HADITHI YA KAKA WA SITA WA KINYOZI

Kaka yangu wa sita amekatwa mdomo wa chini. Nitakusimulia kisa hiki kwa ufasaha na kwa ufupi. Habari ni kuwa kaka yangu wa sita hakuwa ni mtafutaji sana wa mali ila alikuwa ni mcheshi na mpenda utani sana. Alikuwa na hali ya kipato cha chini na ilitokeaga siku nyingine anakosa hata cha kukila. Kaka yangu wa sita naye ni kama wenzie hakuwa na mke wala mtoto na hakupatapo kuoa. Hakuwa na makazi ya kudumu kwamuda mrefu hivyo alizoea sana kutanga tanga. Jambo ambalo lilikuwa linampatia sifa kaka yangu huyu ni kuwa alikuwa ni kijana mwenye sura nzuri. Alikuwa akipendwa sana na wabinti na hata wake za watu. Nadhani hali hii ndiyo iliyomfanya asiwe na makazi maalumu ili kuepuka mitihani na wake za watu na watoto za watu.

 

Ilitokea siku moja kaka hakupata kula toka asubuhi mpaka mwishoni mwa mchana. Katika hali hiyo hakupatapo kutia kitu mdomoni iwe kinywaji ama chakula. Katika hali kama hiyo kaka alidhoofu sana kwa ghafla ndani ya siku moja tu. Katika kutembea kaka akafika kwenye nyumba moja pembeni kidogo na mji. Kaka alikwenda kuomba walau apate hata tunda moja la kufunguwa kinywa chake. Alikuatana na mlinzi wa geti. Kaka akaeleza shida yake kwa mlinzo aliyeonekana mwenye busara sana na mwenye huruma. Mlinzi alimueleza kuwa aingie ndani na atakutana na mwenye nyumba.

 

Kaka akaingia ndani, huko akakutana na bostani kubwa na la kifahari. Matunda yaliyowiva yalikuwa yakining’inia kama taa za fanusi zilizotengenezwa Misri. Maembe machungwa na midizi iliyopangiliwa kwa mistari kwa pamoja ilipendeza vyema. Kaka njaa ndio ilizidi baada ya kuona minanasi iliyokatika sura njema. Kaka hakujuwa ni wapi atamuona mwenye nyumba. Aliendelea mbele huku akiona vitu vizuri na vya kupendeza. Hatimaye alianza kuona kiti kizuri chenye miguu ya kumeremeta. Mzee wa makamo alikuwa akisoma kitabu kikubwa sana. “Asalaamu Alykum” “waalykumsalaam habari yako kijana” “Nzuri tuu” yalikuwa ni salamu kati ya kaka na mzee wa makamo.

 

Baada ya salamu kaka akaeleza shida yake. Mzee alionekana kufurahi sana na alionyesha tabasamu la udadisi. Mzee akamchukuwa kaka hadi kwenye baraza ya nyumba na kukete wakiwa wanaangaliana. Mzee naye akasema kuwa hata yeye ana njaa sana. Alikuwa akisubiri mtu wa kukaa na kula naye, kwani yeye hakuzoea kula akiwa pekeyake hata siku moja. Kaka alifurahi na kuona kuwa nitakula na mwenye nyumba kubwa na ya kifahari. Bila shaka aliamini kuwa leo atakula vitu vya utamu sana.

 

Mzee akaagiza vijana wake walete viliwa. Mmoja akaleta birika la kunawia maji. Cha kushangaza birika lilikuwa tupu, na katika hali hiyo akafanya kama anamnawisha mzee na mzee akafanya kama ndio ananawa. Alipomaliza kunawa alifanya kama anakung’uta mikono. Ukweli ni kuwa hakuna alichonawa ila ilikuwa tu ni utani. Mzee huyu alizijuwa vyema sifa za kaka kuwa anapenda utani. Lakini leo kaka mpenda utani ana njaa sana. Na anafanyiwa utani kwenye chakula. Leo uvumilivu wa kaka unakwenda kupimwa. Baada ya kijakazi kumnawisha mzee alienda kwa kaka naye akafanya vile vile kama anamtirizia maji. Kaka naye akafanya kama mzee vile ananawa kisha akakung’uta mikono yake. Kijakazi akaondoka.

 

Kijakazi mwingine akaja, mzee akamwambia tuwekee nyama ya kuoka na mikate pamoja na mchuzi wa kuchovyea. Kijakazi akafanya kama anatenga. Alipomaliza akaondoka. Ukweli ni kuwa alitenga hewa tu. Mzee akamwambia kaka waanze kula. Mzee akajifanya kama anakata kipande cha nyama huku anaminyana kwa taabu. Akamwambia kaka akamate kipande kile wavutiane. Kaka akafanya kama anakamata kipande kisha kikakatika na wakaendelea kula. Hapa walikuwa hawalikiuhalisia ila kila kitu kilikuwa ni hisia tu. Kaka akagunduwa kuwa stiki za kuchokole meno hazipo. Hapo akajifanya kana kwamba nyama imemkwama kwenye meno yake.

 

Mzee akamuita kijakazi alete stiki, punde ikaletwa na kaka akaanza kuchokowa meno. Kisha akaendele akula kawaida. Nmzee alikuwa akionyesha tabasamu la udadisi muda wote. Kaka akajifanya anakula kwa pupa maana ana njaa sana. Haukupita muda kaka ndipo akapaliwa na kipande cha mkate. Mzee kwa shauku akamkamata kaka na kuktia ngumi mgongoni, ngumu iliyoingia vyema mgomgoni mwa kaka aliyekuwa ana njaa kali sana. Kaka alikasirika sana na alitamani amrudishie ila alivumilia. Kaka akasema kimoyoni huyu mzee nitamlipa masikhara yake leoleo hii na atajuta kufanya utani na mimi.

 

Mzee akajifanya ameshiba hivyo akaagiza vinywaji viletwe. Kaka alitaka aletewe mvinyo uliotemgenezwa kutoka nchi ya uhabeshi. Mzee akaagiza mvinjo wa tende na zabibu. Wote kwa pamoja waliagiza kwa sauti. Punde kijakazi akafanya kama anatenge bilauri na birika mbili akaweka mbele yao ili waweze kujitilia wenyewe. Ukweli ni kuwa kaka alikuwa na njaa sana lakini alijitahidi kuvumulia yote haya huku akitafuta nafasi ya kulipa huu utani. Nafasi aliyoitafuta kaka sasa ndipo imepatikana maana sasa ameanza kujifanya amelewa.

 

Katika hali kama hiyo mvinyo wa kihabeshi ulionekana mkali sana. Sasa kaka amelewa na ameanza kutapika. Akajifanya amemtapikia mzee. Na mzee akajifanya kama anafuta matapishi kwenye kanzu yake. Haukupita muda kaka akamtandika kofi kubwa mzee kwenye shingo. Akamuongeza tena kwenye uso, hadi mzee akaona nyotanyota. Mzee tabasamu likaondoka na akahamaki na kuuliza mbna unaniadhibu? Kaka alifurahi baada ya kuvunja utani wa mzee. Kaka ndipo akajifanya anaongea kwa kulewa, na kumwambia mzee “unataka lingine, wanasema kofi na mlevi zito, na kulewa huku niliko nako nataka nikuongeze lingine”. hapo mzee akacheka sana na kutamka “umeshinda kijana”.

 

Kumbe muda wote mzee alikuwa anamjaribu kaka na sasa kaka ameshinda majaribu. Mzee akajitambulisha vyema kwa kaka, na kaka akjitambulisha. Japo mzee alikuw akimfahamu kaka, maana mzee alikuwa ni rafiki na baba. Baada ya hapo mzee akaagiza chakula cha ukweli kiletwe, na hapo ilikuwa ni kula na kunywa kiukweli. Baada ya hapo mzee alimtaka kaka waishi pale kwa pamoja. Waliishi pamoja kwa muda wa miaka 20, kisha mzee akafariki. Ndugu za mzee wakazichukuwa mali zote na kaka wakamuhisabu kuwa ni mtumwa wa mzee na wakamuuza kwenye biashara za utumwa.

 

Kaka alinunuliwa na mzee mmoja hivi. Kwa kuwa kaka alikuwa na sura nzuri, mke wa mzee alikuwa akimtamani kaka. Siku moja walikutwa wakiwa wamekee kwa pamoja kwa ukaribu sana. Mzee alikasirika na kumkata kaka mdomo, akamtandika na kwenda kumtupa mbali maeneo ya milimani. Wapitanjia walimuokota kaka na kumtibu kumpatia mavazi na chakula. Nilipozipata habari hizi nilikwenda kumtafuta kaka na kumchukuwa.

 

Baada ya kumaliza masimulizi haya haya ya kaka sita pamoja na yeye mwenyewe mkinyozi akamueleza kadhi je umeamini kuwa mimi si mtu wa maneno mengi, bali nazungumza ukweli?. kadhi alifurahi sana na kuniruhusu niondoke pale. Kisha kinyozi akaendelea kusema kuwa katika pirika pirika ndipo nikakutana na baba wa huyu kijana wakati huo kijana huyu akiwa ni mdogo. Niliweza kuishi na baba wa huyu kijana kwa muda mrefu, na kabla ya kufariki alinitaka niendelee kumlinda kijana wake. Niliendelea kufanya hivi kwa siri kwa muda mrefu. Hivyo sikuwa nikimtakia maomvu huyu kijana kama yeye alivyofikiria.

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021-11-08     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1045

Post zifazofanana:-

Madhara ya maumivu kwenye nyonga na kiuno.
Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea ikiwa matibabu kwenye nyonga na kiuno hayatafanyika. Soma Zaidi...

Maambukizi katika mfumo wa Uzazi wa mwanamke
Maambukizi kwenye Njia ya Uzazi kwa kifupi hujulikana Kama PID.ni Maambukizi ya mfumo wa Uzazi yanayoathiri wanawake, Maambukizi haya kwa Kawaida huhusisha sehemu Kama shingo ya uzazi,nyuma ya mfuko wa Uzazi na mirija ya uzazi. Soma Zaidi...

Aina za fangasi
Somo hili linakwenda kukuletea baadhi ya aina za fangasi Soma Zaidi...

Sababu za kushuka surat al-Fiyl
Al fiyl ni neno la Kiarabu lenye maana ya tembo. Sura hii inazungumziakisa cha jeshi lenye tembo. Jeshi hili lilikuwa na nia ya kuvunja al qaaba Soma Zaidi...

Mafunzo ya DATABASE - MySQL database somo la 5
Huu ni muendelezo wa mafunzo ya DATABASE kwa kutumia software ya MySQL na hili ni somo la tano. katika somo hili utajifunza type of data yaani aina ya taarifa ambazo unaweza kuzihifadhi kwenye database yako. Soma Zaidi...

Fahamu matatizo ya ini kuwa na kovu
kovu (Fibrosis) ya ini inayosababishwa na aina nyingi za magonjwa na hali ya ini, kama vile Homa ya Ini na unywaji pombe kupita kiasi. Ini hufanya kazi kadhaa muhimu, ikiwa ni pamoja na kuondoa vitu vyenye madhara katika mwili wako, kusafisha damu yako Soma Zaidi...

Dalili za maambukizi ya sikio kwa watoto
Posti hii inazungumzia kuhusiana na dalili za maambukizi ya sikio kwa watoto. Soma Zaidi...

Samaki aina ya salmon
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sifa za samaki aina ya salmon Soma Zaidi...

Papai lililo iva ni salama kwa mama mjamzito au halifai
Papai ni moja kati ya matunda yenye vitamini C na virutubisho vinginevyo. Lakini papai pia ni moja kati ya vyakula ambavyo mjamzito anatakiwa awe makini navyo. Soma Zaidi...

Kulelewa kwa Mtume, maisha yake ya Utotoni na kunyonya kwake.
Historia na sura ya Mtume Muhammad S.A.W sehemu ya 06. Hapa utajifunza kuhusu historia ya Mtume akiwa mtoto. Soma Zaidi...

Hadithi ya binti wa kwanza na mbwa
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Dalili ya pressure ya kupanda
Post ya leo inaenda kufundisha dalili na hatari za presha ya kupanda. Presha ni ugonjwa unaosababishwa na baadhi ya vitu mbalimbali.pressure hujulikana kwa jina lingine ambolo ni hypertension (pressure ya kupanda). presha hugundulika pale ambapo presha ya Soma Zaidi...