Hadithi ya kisiwa cha mawe yanayolia

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad

HADITHI YAKISIWA CHA MAWE YANAYOLIA.

Nimesimuliwa na manahodha wenzangu ambao walipata habari za kisiwa hiki kupitia mababu wa manahodha wenzao ambao walipata habari hizi kutoka kwa mababu wa zamani. Habari za kisiwa hiki ni kuwa, alikuwepo kwenye kisiwa hiki mfalme aliyekuwa anapendwa sana na watu wake. Alikuwa anaushawishi sana na ni mpenzi wa watu. Mfalme na watu wake walikuwa wakiabudia masanamu na kuyafanya ndio miungu yao mikuu. Bila ya kufahamu kama kuna Mungu muumba ambaye anatambulika kwa majina mengi kama Allah kwa waislamu lakini mfalme huyu aliamini kuwa masanamu yao ndio miungu mikubwa.

 

Hali hii ilikuwa ni kawaida kwa mji huu na wananchi wake. Na Mwenyezi mungu aliwapa kila kitu wanachoihitaji. Ilitokea siku moja akaja mtu mkubwa sana akawa anazungumza habari juu ya Mungu Mmoja aliyeumba kila kitu. Habari hiki ziliwashituwa watu wa mji ule kwa tabia yao ya kuabudia masananmu. Mtu yyle alikaa nchini pale kwa muda wa mwaka mmoja akiwa anatoa habari zile na watu wasi mwamini. Mfalme wa nchi ile alikuwa akikasirishwa sana na uwepo wa mtu yule eneo lile.

 

Baada ya mwaka kuisha watu kadhaa walianza kuelewa kuwa masananmu si miungu kwani yametengenezwa na mawe tu na ni kazi ya wafinyanzi. Fikra hizi zilipoanza kuelezwa na wananchi mfalme aliamrisha watu wote wanaomuamini mtu yule wakamatwe. Na mambo yakawa hivyo na walikamatwa watu wote waliomuamini maneno yake mtu yule. Walianza kuadhibiwa na kuuliwa ila yule aliyekubali kuabudu masanamu yao alikuwa akiachiwa. Basi waliuliwa wote hata yule mtu akauliwa pia.

 

Baada ya kufanyika yalofanyika kwa muda wa siku tatu nchi ile ilikuwa na amani. Kuanzia siku ya nne amani ilitoweka kwani moshi mkali sana ulikuja na ukaanza kukausha watu wote na kugeuka mawe. Mashi ule ukauazunguka mawe yale, na kwa kuwa mawe yale ni watu wakawa wanalia kwa moshi ule na kuomba msamaha kwa Allah. Machozi yao ndo yanaendelea hadi leo kama mnavyoona mawe haya yanavyolia. Basi hii ndio hadithi ya mawe haya.

 

 

Safari yetu iliendelea tukafanya biashara maeneo kadhaa. Tukiwa njiani maji yalituishia hivyo tukamwambia nahodha atupeleke kwenye kisiwa chochote jirani na tulipo ilo tulapate maji ya kunywa. Nahodha alifanya hivyo na akatupekeka kwenye kisiwa flani ambacho hakikuwa kikishi watu ala alitutahadharisha kuwa eneo lile linaishi wanyama wakari hivyo tufanye tufanyayo na tuwahi kutoka. Basi tukaanza kuchota maji na tulipomaliza wenzangu wakaanza kuzunguka kwenye kisiwa kile waone kama kuna chochote wanaweza kukichukiwa wakauze mbele ya safari.

 

Walizunguka na baada ya muda wakaona kuna kitu kama jiwe kubwa sana jeupe. Wakalisogelea wakidhani inaweza kuwa madini. Walipofika karibu niligunduwa kuwa lile ni yai la ndege mkubwa sana anayeitwa rock. Kwani nilishakumbana na hali kama hii huko nyuma. Basi nikawaambia wenzangu yai hili ni la rock hivyo tuondokeni kwa haraka hapa akitukuta tutauliwa wote. Wenzangu walinibishia na wakalipasua, na kulikaanga wakaanza kulila hata kulibakisha kidogo. Mara tukaona kufuli kikubwa kinakuja nahodha akatuambia tuwahi kuondoka.

 

Kwa umahiri alio nao nahodha aliweza kuweka jahazi sawa na kuanza kuondoka wale ndege walikuwa ni wawili na walipogunduwa kuwa yai lao limeliwa walipiga kelele sana na wakaondoka. Kwa muda hatukuweza kuwaona kabisa tukadhani kuwa tuposalama. Baada ya muda kidogo tukaona kundi kubwa la ndege aina ile linakuja na kila mmoja akiwa amebeba jiwe tayari kutupiga. Na mawe walobeba yalikuwa ni makubwa sana kiasi kwamba kama wawili yanapiga jahazi hakuna atakayepona.

 

Basi ndege wale wakaanza kutupa mawe yale na kwa bahati mbaya jiwe moa likapiga jahazi letu kwa mbele. Kwa umadhubuti wa jahazi lile liliweza kupasuka na kufanya maji yaingie. Jahazi likaanza kuenda hovyo na kukagonga mwamba na kupasuka kabisa. Mimi niliponea kupata ubao nikaukamata kikwelikweli na nikaenda nao hadi ufukweni. Niifika eneo lenye ufukwe mzuri uliopandwa bostani nzuri na ya kivutia. Bila ya kujali ni ya nani nilianza kula matundwa kwa njaa nilonayo. Niliposhiba nikaingia ndani ya bostani ili niweze kuomba msamaha kwa madunda nilokula.

 

Niulimkuta mwenyewe na akaniambai ili anisamehe ni lazima nifanye kazi ya kumuuzia matinda yake sokono kwa muda wa mwezi mzima. Kwa kuwa mimmi ni mfanya biashara sikuona jambo lile ni adhabu. Nilimuuzia matunda yake na alishangaa kuona kuwa kila siku faida ilikuwa ikiongezeka maradufu. Alinipenda sana mzee yule na akaniamini zaidi. Alinifanya kama mtoto wake. Kwa biashara ile na mimi nilipata mtaji na kuanza bishara ndogo ndogo na hatimaye nikapata mtaji wa kuweza kuanza biasha ra za kusafiri. Lengo langulilikuwa ni kurudi kwetu Baghadad.

 

Ilitokea sikumoja nikapata habari kuwa kuna jahazi la wafanyabiashara kutoka Baghadad limekuja na linatarajia kurudi baghadad baada ya wiki moja. Nilimuomba ruhusa yule mzee nieze kurudi nyumbani na alikubali kwa unyongesana. Siku moja akaniita usiku na kuniambia kuwa alinithamini kama mtoto wake na kwa kuwa yeye hana mtoto hata mmoja alitowa hazina ya mali zake ikiwemo madini ya dhahabu, almasi na thamaqni nyinginezo na pesa nyingi sana. Akanikabidhi na aliniambia kuwa anatarajia kuuza shamba lake lile ali arudi nami Baghadadi nilimkubalia na alifanya hivyo.

 

Baada ya maandaizi yalipokamilika tulianza safari ya kurudi na tulifika Baghadadi kwa salama na amani. na hii ndio stori yangu ya safari yangu ya nne. Baada ya kuzungumza haya Sinbad akampatia Sibdad wa nzhikavu pesa kadhaa kwa ajili ya kufidia muda wake wa kukaa naye. Pa akamwahidi kesho aje tena kusikiliza yalomkuta kwenye safari yake ya sita.Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021-11-08     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1167


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Hadithi hii inahusu hasara za wivu na kutokuwa wazi
Posti hii inahusu zaidi hasara za wivu, kwa sababu ya kuwepo kwa marafiki wasio waaminifu wanasababisha kuharibiana maisha bila kujua kwa sababu ya kuonekana wivu na kutokuwa wazi. Soma Zaidi...

Utajiri wa baba na kifo chake
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Muendelezo wa hadithi ya mshona nguo
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Mtoto wa Tajiri na maskini ( sehemu ya kwanza)
Post hii inahusu hadithi fupi tu kuhusu mtoto wa tajiri na maskini, palikuwepo na watoto wawili mmoja akiwa mtoto wa tajiri na mwingine wa maskini. Soma Zaidi...

Safari saba za sinbad
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

Dalili ya mimba ya wiki moja(1)
Mwanaume na mwanamke wanapo kutana na kujamiina kama mwanamke yupo kwenye ferlile process ni rahisi kupata mbimba. Sparm Zaid ya million moja huingia kwenye mfuko wa lakin sparm moja ndio huweza kuingia kwenye ovum(yai)lakin nyingine hubaki kwenye follopi Soma Zaidi...

Hadithi ya Kaka wa kwanza wa kinyozi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Kiapo cha sultani
Posti hii inakwenda kukusimulia hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Hadithi ya Kaka wa sita wa kinyozi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili
Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili,ambapo Mama yake na Jackie pamoja na jack wakiwa hospital na jack anaendelea kumwita Julius kila mara. Soma Zaidi...

Madhara ya fangasi ukeni
Maambukizi ya fangasi katika sehemu za Siri za mwanamke husababishwa na fangasi wanaoitwa CANDIDA ALBICANS pia maambukizi haya hujulikana kama YEAST INFECTION. Pia hupatikana katika midomo, mpira wa kupitisha chakula,kibofu Cha mkojo ,uume na uke. Soma Zaidi...

Hadithi ya tabibu wa mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...