image

Hadithi ya mji uliogeuzwa mawe

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

HDITHI YA MJI ULOGEUZWA MAWE.

Mimi ni mtoto wa mfalme wa nchi hii ambayo umemuona amegeuzwa jiwe kama watu wengine. Nilipokuwa mdogo nilikuwa nikilelewa na bibi mmoja laiyekuwa ni muiislamu. Watu wa mji huu walikuwa wanaabudu masanamu hivyo bib i yule alifanya siri imani yake. Na kwa usiri huo akanifundisha imani ya uislamu juu ya mungu mmoja na akanifundisha kusoma Qurani. Katika muda wote niloishi nae yapata miaka 10 alikuwa akinisisitiza kufanya siri imani ile na mambo yakawa hivyo mpaka bibi yule alipofariki.

 

Mwaka juzi alikuja mtu mmoja hapa nchini kwetu, mtu huyu ulikuwa ikilingania watu kuhusu kumuabudu mola mmoja tofauti na watu walivyozoea. Mfalme aliongea maneno ya ajabu na ya kipuuzi kuhusu sauti ile. Mtu yule aliondoka na akarudi tena mwaka jana na maneno yalikuwa ni yalelyale. Na mfalme yaani baba yangu alirudia maneno yaleyale. Na mara ya tatu mwaka huu alirudi tena Mtu yule na mambo yakawa vile vile.

 

Wiki mbili baada ya kuondoka kwa Mtu yule ikatokea sauti ikionya na kulingania juu ya imani ya munngu mmoja. Hali ikawa kama mwanzo Mfalme wetu akatoa kejeli na maneno machafu sana. Kwa hakika niliumia na nikataka kwenda kumtia adabu baba yangu mwenyewe lakini nilishindwa kufanya hivyo. Machozi yalinitoka na nisijuwe jambo la kufanya na hakina wa kunishauri. Basi haikupita muda mrefu ile sauti ikatoweka na hapo anga ikafunga kuwa nyeusi kutokana na wingu lisilojuliukana kama la mvua au upepo mkali.

 

Wingu lile liliendelea kusogea chini hata likakaribia kufunika nyumba. Ulikuwa ni wakati wa muda wa swala ya adhuhuri na watu wamechanganyika katika utaftaji. Wengine wapo masokoni na wengine mashambani na hali kadhalika. Wingu lile likaambatana na upepo mlaini ambao haukuweza kuharibu hata kipande cha nguo kilichokuwa kinaning’inia. Upepo ule uliingia masikion, puani na kila sehemu yenye tundu na kutokea upande mwingine.

 

Haukupita muda wat wote wakawa katika hali uloiona kuwa mawe. Na kia mtu vile alivyo ndivyo alivyobaki. Hata walokuwa wamelalaq wamebakia mawe kwenye vitanda. Nilitoka kuchunguza zaidi sikuona hata mnyama ambaye aligeuzwa jiwe. Kwa hakika msiba huu uliwapata wanadamu tuu. Basi nikawa sina pa kwenda hiyo nikabakia kisiwani hapa peke yangu kama unavyonioa. Na hii ndiyo historia ya kisiwa hiki kilichogeuzwa mawe.

 

Wakati kijana anamaliza kusimulia hadithi ile Zubeida akawa analia na machozi yanamtiririka kama chemchem iliyoanzia mlimani. Basi kijana kwa huruma akawa anamfuta machozzi Zubeida. Baada ya muda Zubeida akauliza “sasa wanyama walikwenda wapi?” kijana akamjibu baada ya kutokea yaliyokwisha tokea ilikuja tena ile sauti na kuniambia kuhusu hatima ya wanyama. “ama kuhusu wanyama amri yao ipo kwako, eidha utawatumia kama chakula chako mpaka Allah atakapoleta nusra , ama awahamishe awapeleke anakotaka ama wageuzwe kuwa vitu vya thamani na iwe kama zawadi ya Zubeida mwenye kupotea njia mwana wa tairi na msalitiwa na ndugu zake.

 

Basi nikachaguwa jambo la tatu, na pindi ulivyokuja nilifahamu hakika ni wewe Zubeidah. Zubeida akamuuliza “ni kitu gani kilichokufahamisha” akaendelea ile sauti niliiulisa sasa ni kwa namna gani nitamfahamu Zubeidah ikajibu siku moja kabla ya kuja kwa Zubeiday bahari itakuwa chafu sana na upepo maini utaingia kisiwani hapa na kusafisha nyia ya Zubeida mwana wa tajiri, msalitiwa. Hivyo Zubeida atakuwa hana jinsi ila atakufikia tu popote utakapokuwepo muda huo. Basi nilipoziona ishara hizo nilifahamu ujio wako hivyo ili kukurahisishia kunipata nikawa nasoma Qurani kwa sauti ya juu ndivyo ukanisikia.

 

Ama kuhusu kusalitiwa kwa Zubeida na ndugu zake nilishindwa kujuwa mengi zaidi maana sauti ile ikanambia hainipasi kujuwa siri za mambo yajayo. Halikadhalika ninachofahamu zaidi kuhusu huo usaliti ni kuwa maisha yangu ama yako yatakuwa hatarini. Basi Zubeida na yule kijana wakatoka pale na Zubeidah akashauri waoane na wakakubaliana kufunga ndoa punde watakapofika nyumbani.

 

Basi kijana akampeleka Zubeidah kwenye zawadi yake na akakuta mali nyingi sana na tayari imeshafungwa vizuri kwenye mkokoteni. Basi wakaburuza mkokoteni wao mpaka kwenye chombo chao na kuuingiza ndani. Wakawa wanapunga upepo ufukweni na kubadilishana mawazo na kuchat. Wakiwa katika hali hiyo ghafla akatokea nge anakimbizwa na kunguru Zubeidah akachukuwa kijiwe na kumpiga kunguru na ukawa ndio mwisho wa maisha ya kunguru yule na nge akatokomea kwenye mawe. Na wawili hawa wakaendelea kuzungumza. Wakati yote haya yanafanyika dada zake na Zubeidah walikuwa wakiona wivu na kijicho kwa mafanikio ya ndugu yao.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1195


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

HADITHI ZA ALIF LELA U LELA (sehemu ya kwanza): KIAPO CHA SULTAN
Soma Zaidi...

Hadithi ya chongo wa pili mtoto wa mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Hadithi za Sinbad
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

Hadithi ya mzee wa pili na mbwa wawili weusi
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

HADITHI ZA SINBAD
Soma Zaidi...

Kitabu Cha hadithi ya wanawake watatu
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

Kwisha kwa chakula
Posti hii inakwenda kukuletea muendelezo wa safari za Sinbad Soma Zaidi...

HADITHI ILIYOSIMULIWA NA MLEVI MBELE YA SULTANI
Soma Zaidi...

MWANZO WA USALITI
Download kitabu Hiki Bofya hapa USALITI UNANZA HAPA Baada ya kukaa pale siku moja nahodha akaamrisha chombo kiondoke pale na kurudi nyumbani. Soma Zaidi...

HADITHI YA SAMAKI WA RANGI NNE
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA SAMAKI WA RANGI NNE. Soma Zaidi...

HADITHI YA CHONGO WA TATU MTOTO WA MFALME
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA CHONGO WA TATU MTOTO WA MFALME Mimi ni mtoto wa mfalme kama nilivyotangulia kusema na ni mtoto wa kipekee kwa baba na mama. Soma Zaidi...

BINTI WA NDOTONI
Download kitabu Hiki Bofya hapa BINTI WA NDOTONI. Soma Zaidi...