Navigation Menu



Hadithi ya samaki wa Rangi nne

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

HADITHI YA SAMAKI WA RANGI NNE.

Baba yangu alikuwa ni mfalme wa eneo hili kwa muda usiopungua miaka hamsini. Alifariki akiwa na umri wa miaka 66, na baada ya kufariki kwake mimi nilichukuwa madaraka hayo. Nchi hii i;likuwa nzuri sana ilozungukwa na visiwa vinne ambavyo ndio milima unayoiona. Nilikuwa na mke wangu ambaye ni binamu yangu. Nilimpenda sana mke wangu na niliamini kuwa naye ananipenda kama ninavyompenda. Tuliishi hivyo kwa muda wa miaka kadhaa bila ya kuona mabadiliko yoyote katika mapenzi yetu.

 

Ilitokea siku moja nilipokuwa nipo kati ya kulala ama kusinzia (mang’amung’amu ya usingizi), vijakazi wawili wa mkewangu wakawa wananipepea. Nikawasikia wanazungumza “namuonea huruma mfalme, anampenda sana mkewe lakini mkewe hampendi, anampenda mtumwa wake.” ni maneno ya mmoja wa wale wajakazi. Mwingine akadakia “yaani anatamani hata amuuwe, na vile anajuwa ucha wipo siku atamuuwa tu”. Wajakazi hawa wakati wanazungumza walidhani nimelala, kumbe nimeyasikia vizuri maneno yao.

 

Siku ilofuata nikaanza kufanya uchunguzi wa maneno yale. Niligunduwa kuwa ni ya ukweli kama walivyosema wale wajakazi. Hivyo nikamchukuwa yule mtumwa na kuanza kumwadhibu. Kwa bahati mbaya wakati wa kumwadhibu alipigwa vibaya na akapoteza fahamu. Yule mke wangu alikasirika sana na akamtibu lakini bia ya mafanikio. Alifanikiwa kumueka hai, yaani anafahamu lakini haweza kufanya chochote. Mwanamke yule kwa hasira alizonzo wakati ule aliondoka kwa muda na nisijuwe wapi alipokwenda.

 

Baada ya muda akarudi, na akachukuwa kifuu cha nazi na akaweka maji, kisha akazungumza naneno ya ajabu akamwaga juu. Visiwa vilivyouzunguka mji huu vikawa milima hiyo unayoiona na mji yakiwemo maduka na vinginevyo ukawa bwawa la maji hayo unayoyaona na watu wakageuzwa kuwa samaki hao wa rangi nne unaowaona yaani hizo rangi za samaki ni aina za watu walokuwepo eneo hili. Baada ya kufanya hayo na mimi akanimwagia maji nikawa kama hivi unavyoniona. Haikuishia hapo kila siku anakuja kunitandika mijeledi ya ngozi ya kifaru. Hunitandia kadri anavyotaka kisha huondoka. Hii ndiyo historia yangu na mji huu.

 

Kijana alimaliza kusimulia hadithi ya nchi yake, mfalme alipatwa na uchungu sana wakati akisikiliza maneno yale. Chozi lilikuwa likimtoka kwa huruma na majonzi. Kish akauliza mahala alipo huyo mwanamke. Kijana akamjibu kwa kumwambia kuwa yeye hajui alipo isipokuwa kila siku jioni baada ya kuniadhibu huenda upande ule (akaelekeza kwa kidole upande wa kusini). Mfalme alikwenda kule alikoelekezwa na kumkuta mtumwa ambaye ni mgonjwa. Akarudi kwa kijana na wakapanga mbinu yako, kisha wakakubaliana watekeleze kesho mpango wao.

 

Basi mambo yakawa kama walivyokubaliana, siku ilofata mfalme akachukuwa upanga wake na akaunoa safi. Akaenda kwenye lile jumba lenye yule mtumwa mgonjwa. Alipofika akamkata upanga na kummalizia uhai wake, kisha akamuingiza kwenye kisima cha maji. Baada ya hapo akajilaza pale kwenye kitanda kama vile yeye ndiye mgonjwa. Yule mwanamke kama kawaida yake alipokuja siku ile akamuadhibu yule kijana kisha akaelekea kule kwenye mgonjwa wake. Alipofika akamwuliza “u hali gani wangu? Vip tafadhali naomba zungumza nami japo neno moja tuu”. Mfalme alojilaza pale kama yeye ndo mgonjwa akamjibu “sina raha kwakweli” “mmmh utamu ulioje leo kusikia sauti yako. Hebu niambie kipi kinachokukosesharaha jama”. Ni maneno ya yule mwanamke. Mfalme alojifanya ndo mgonjwa akajibu “hiyo sauti ya mumeo inanipa taabu, hebu mrudishe katika hali yake ya kawaida na aondoke hapa”. Basi kusikia hivyo yule mwanamke akatoka na kwenda kuchukuwa maji akayasemea maneno flani kisha akamwagia yule kijana na hapohapo akarudi katika umbo lake. Kisha akamwambia uondoke na nisikuone tena eneo hili, sihivyo nitakuuwa.

 

Yule kijana alijifanya anaondoka na akajificha ili ashuhudie kinachoendelea. Basi huku yule mwanamke akaelekea kule moyo wake ulipozama, alipofika akamuliza mtumwa wake “nimesha fanya utakavyo, vipi unajisikia amani sasa ?” yule mfalme alojifanya mgonjwa akamwambia hapana, hizo sauti za watu ulowageuza samaki zinanipa shida usiku. Hebu warudishe katika hali yao ya kawaida pamoja na mali zao”. Yule mwanamke akatii an kutoka akazungumza maneno yake ya kichwawi na mji ukabadilika kama ulivyo zamani. Wale watu wa mfalme walokuja kuchunguza samaki walishangaa kujikuta wapo katikati ya mji.

 

Yule mwanamke mchawi akaenda kwa mtumwa wake. Akamuuliza haya sasa bilashaka umeridhika. Yule mfalme alojifanya mgonjwa akamwambia “sogea hapa karibu” mwanamke akasogea zaidi yule mfalme akachukua upanga na kumkata vipande viwili. Hna huo ukawa ndo mwisho wa mchawi huyu. Mfalme akatoka na kukutana na kijana. Waliflai sana na kuzungunza mengi zaidi kuhusu eneo lile lenye mali mengi na utajiri wa kutosha.

 

Yule mfalme akamwambia kijana “nimeflai sana, na kwakuwa tupo majirani zaidi tutakuwa ndugu”. Kijana alicheka sana kwa fyraha na mshangao. Kisha akamwambia yule mafalme “kutoka hapa mpaka kufika kwenye utawala wako ni mwendo wa mwaka mmoja. Uliweza kutumia masaa machache kwa sababu eneo hili lilifanyiwa uchawi kama ulivyoona. Basi kijana akamwahidi atamsindikiza wakati wa kurudi mpaka kwake. Mfalme aliflai sana na akamwahidi kumfanya mrithi wa utawala wake kwani yeye hakuwa na mtoto wa kumrithisha.

 

Basi mambo yakawa hivyo, na safari ilikuwa ni nzuri ya ya furaha zaidi. Wafalme hawa walizungumza mengi na kucheka utadhani mtu na mwanae. Walibeba zawadi nyingi na mali nyingi kutoka ufalme ule tajiri. Walipofika walizigawa mali zile kwa viongozi kulingana na vyeo vyao. Mfalme aliitisha mkutano mkubwa sana siku ilofata na akatangaza nia yake ya kutaka kumrithisha ufalme kijana yule na kumfanya kuwa ni mtoto wake. Basi mambo yakawa kama hivyo,

 

Nchi ilikuwa katika hali ya furaha sana kwa muda mrefu. mfalme alikuwa katika furaha kubwa zaidi kwa kupata mtoto na mrithi wa utawala wake. Yule mvuvi ambae ndio chanzo cha yote haya alipewa mali nyingi sana za kuweza kutumia yeye na vizazi vyake vingi vijavyo na akamfanya katika watu wake wa karibu. Kufikia hapa Dinar-zade akamaliza hadithi ya mvuvi. Hadithi hii mpaka kwisha ilichukuwa siku nyingi kwa mfale mpaka akalowea na hadithi. Dinar-zade aliponyeka kuuliwa kama hivi ikawa ikiisha hadithi analeta nyingine. Hivyo akaendelea kusimulia hadithi iliyonzuri kuliko hii ya mvuvi nayo i hii;-

Download app yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download

Download Now Bongoclass

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu image Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Aliflela1 Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Views 1499


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Simulizi za Hadithi Audio     👉5 Kitau cha Fiqh     👉6 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

HADITHI YA MVUVI NA JINI
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA MVUVI NA JINI Hapao zamani kulikuwepo na mvuvi aliyekuwa masikini wenye watoto watatu na mke mmoja. Soma Zaidi...

SAFARI YA PILI YA SINBAD
Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA PILI YA SINBAD Basi siku ile Sinbad mbeba mizigo aliwahi haraka sana na mapema zaidi, na akamkuta Sinbad wa baharini ameshakaa na watu wake wanamsubiri kuanza hadithi. Soma Zaidi...

SAFARI YA TATU YA SINBAD
Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA TATU YA SINBAD Siku ile ya pili Sinbad mbeba mizigo alivaa ngup zake safi alizonunua na kijipamba vyema na kuelekea kwenye kikao chao. Soma Zaidi...

SAMAKI WA AJABU
Download kitabu Hiki Bofya hapa SAMAKI WA AJABU Walikwenda upane wa magharibu na mji wakauacha upande wa kusini. Soma Zaidi...

HADITHI YA SAMAKI WA RANGI NNE
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA SAMAKI WA RANGI NNE. Soma Zaidi...

Kitabu Cha Hadithi ya kifo cha Damu
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

HADITHI YA MZEE WA TATU NA MBWA
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA MZEE WA TATU NA MBWA WAKE MWEKUNDU Kama nilivyotangulia kusema , huyu ni mkewangu wa ndoa tulioishi pamoja kwa muda wa miaka zaidi ya kuni na tano sasa. Soma Zaidi...

MWANZO WA USALITI
Download kitabu Hiki Bofya hapa USALITI UNANZA HAPA Baada ya kukaa pale siku moja nahodha akaamrisha chombo kiondoke pale na kurudi nyumbani. Soma Zaidi...

HADITHI YA BINTI WA KWANZA NA MBWA
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA BINTI WA KWANZA NA MBWA. Soma Zaidi...

HADITHI YA MWEN YEKUTABIRIWA MTOTO WA TAJIRI
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITI YA MWENYE KUTABIRIWA MTOTO WA TAJIRI Kwanza tambua ewe ndugu yangu kuwa mimi ni mtoto wa tajiri mkubwa sana katika nchi yetu hii. Soma Zaidi...