HADITHI YA TABIBU WA MFALME


image


Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela


HADITHI YA TABIBU WA MFALME

Katika nchi ya Zouman iliyopo maeneo ya uajemi alikuwepo mfalme mkubwa sana. Mfalme huya alipenda kusoma na kucheza mpira wa farasi, alimwamini sana waziri wake. Mfalme huyu alikuwa na ugonjwa ambao matatibu wengi walijitahidi lakini walishindwa. Kila tabibu mzuri katika nchi yake alijaribu bila ya mafanikio. Mfalme alikata tamaa ya kupon augonjwa wake.

 

Ilitokea katika nchi ile kuna tabibu ambaye ni mjuzi sana lakini hakutambuwa kama mfalme ana tatizo hilo. Tabibu huyu aliitwa Douban. Alipo[ata taarifa za ugnjwa wa mfalme alikusanya mavitabu yote na utabibu na kuanza kustadili kuhusu ugonjwa wa mfalme wake. Na hatimaye akafanikiwa kugunduwa dawa itakayomtibu mafalme. Dawa ambayo ingemtibu mfalme hata bila ya kumgusa.

Siku ilofata alivaa nguo zake safi za kitabibu na akaenda ikulu kuomba kumuona mfalme. Kwa kuwa alijitambulisha kama tabibuilikuwa ni rahisi kwake kumuona mfalme. Alipiga magoti na kumueleza mfalme kilicho mleta. “nina dawa ya kutibu maradhi yako hata bila ya kukugusa kwa uwezo wa Allah” ni tabibu akimwambia mfalme. “ukitibu maradhi nilonayo nitakufanya tajiri na utakuwa ni katika watu wangu wa karibu” kwa furaha mfalme akimwambia tabibu Douban. “Ndio mkuu tutaanza tiba yetu kesho IN shaa Allah” ni maneno aliyoyasema tabibu.

 

Siku hiyo tabibu alivaa safi mavari yake na kuiweka dawa yake tayari kwa ajili ya kumtibu mfalme. Aliiweka dawa yake kwenye fimbo ya kuchezea mpira wa farasi. Kisha akamwambia mfalme atumie fimbo ile kuchezea mpira wa farasi na apige kwa nguvu mpaka jasho limtoke. Mambo yaka wa kama hivyo na mechi ikaanza. Mfalme alicheza kwa uwezo wake wote na akawa anapiga mpira kwa fimbo yenyedawa. Kila anapopiga ndio dawa inavyiongia kutoka kwenye fimbo kuingia mwilini mwake. Mechi ilipoisha akamwambia mfalme akifika nyumbani kwake aoge kisha alale. Mfalme alifanya vivyohivyo na alipoamka ailikuwa ni asubuhi. Alistaajabu kuona ampona kabisa maradhi yake.

 

Aliagiza tabibu Douban aletwe mbele yake ili amlippe alichomwahidi. Mambo yakawa vivyo hivyo aliletwa tabibu na kutoa heshima kwa mfalme. Mfalme alifurahi na kumpa utajiri yeye na familia yake. Tabibu Douban akawa ni katika watu wa karibu na mfalme. Baadhi ya viongozi wa nchi walimonelea wivi tabibu. Waziri mkuu alikuwa ni muhanga wa jambo hili. Alikuwa akikasirika sana kumuona tabibu na mfalme. Hakupenda ukaribu wao na alitafura mbinu na njama mbalimbali kuweza kuwatenganisha.

 

Sikumoja kaamuwa kutekeleza mpango wake, alimfata mfalme na akamweleza kuwa amegunduwa kuwa huyu tabibu anataka kukuuwa. “kama angetaka kuniuwa kwa nini amenitibu” ni swali la mfalme kwa waziri. “huenda ange kuuwa muda ule angejulikana, lakin sasa umemwamini muda si mrefu atatekeleza madhambi yake” waziri akimjibu mfalme. Mabishano haya yalichukuwa muda mfalme akimtetea tabibu na waziri akimkandamiza tabibu. Mwisho mfalme akamwambia tabibu “nakumbuka vizuri maneno ya waziri mfani alipomwambia mfalme Sinbad alipotaka kumkinga mwanae asiuliwe” . “ni maneno ganihayo ewe mfalme wangu” waziri akimuuliza mfalme kwa shauku. Mfalme akamjibu “alimwambia usiamini maneno ya mtu yeyote hata akiwa mkweo kisha akamsimulia hadithi hii”;



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Jifunze fiqh       ðŸ‘‰    2 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    3 Hadiythi za alif lela u lela       ðŸ‘‰    4 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    5 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    6 Mafunzo ya php    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Hadithi hii inahusu hasara za wivu na kutokuwa wazi
Posti hii inahusu zaidi hasara za wivu, kwa sababu ya kuwepo kwa marafiki wasio waaminifu wanasababisha kuharibiana maisha bila kujua kwa sababu ya kuonekana wivu na kutokuwa wazi. Soma Zaidi...

image Hadithi ya chongo wa pili mtoto wa mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Hadithi ya mvuvi na jini
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili
Post hii inahusu zaidi hadithi ya vijana wawili ambapo mitihani inaisha na wanaanza kuhukumiwa mmoja baada ya mwingine. Soma Zaidi...

image Ndoto ya mgonjwa, binti mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Hadithi ya chongo wa kwanza mtoto wa mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme
Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme, tunajua kuwa mama yake na binti alimtorisha yule binti mbali kabisa ila kijana naye aliamua kutoroka na kumfuata binti mfalme na hatimaye akampata alipo. Soma Zaidi...

image Kuelekea bonde la uokozi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

image Usuluhishaji wa walio dhurumiwa
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Ugeni wa dhati
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...