image

Hadithi ya waziri aliyeadhibiwa

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

HADITHI YA WAZIRI ALIYEADHIBIWA.

Kulikuwa na mfalme aliyekuwa na mtoto wake mmoja wa kiume. Alimpenda sana mtoto huyu, huenda ni kwa sababu alikuwa ni mmoja na ni wakipekee. Mtoto huyu alipenda sana kuwinda na alikuwa ni hodari wa kupanda farasi, hasa alikuwa na uwezo wa kumdandia farasi kwa haraka sana. Zaidi haayo aliweza kuelewa lugha nyingi. Alikuwa anapokwenda kuwinda akienda na waziri ambaye alipewa kazi ya kumlinda mtoto huyu.

 

Walitoka sikumoja kwenda kuwinda, waliwinda kwa muda mrefu bila ya kupata kitu. Mtoto huyu akaona kibendera kimenyanyuliwa (isharaya kuonekana kiwindwa) alijuwa kuwa aliyonyanyuwa ni waziri. Basi akakifata kibendera na akakutana na swala mzuri mwenye afya. Alimfata na swala akikimbia, alichukuwa muda mwingi na hatimaye akaamuwa kurudi. Kwa bahati mabya alipotea nyia na asijuwe pa kurudia. Hakujuwa waziri yupo wapi, hivyo akazidi kutokomea mwituni.

 

Ilipofika karibia na jioni alikutana na bint mmoja msituni, akamkaribia na kumsalimia. “unafanya nini hapa na na ninnani wewe?” ni maswali aliyomuuliza binti yule. “mimi ni mtoto wa mfalme wa hindi na hapa nimepote” yalikuwa majibu ya bint. Basi akamchukuwa kwenye farasi wake na wakawa wanatafuta njia. Wakapita sehemu kuna jumba lililohamwa siku nyingi. Yule bint akashuka na kijana akashuka pia. Bint akawa anaelekea mule ndani. Alipoingia ndani yule kijana akiwa nje akasikia sauti ya yule bint ndani kwa lugha ya kihindi (yule binti alidhani yule kijana hatelewa lugha ile) “wanangu nimekuleteeni nyama kubwa yenye afya leo” akasikia sauti nyingine zikijibu “iko wapi mama tuile tuna njaa sana mama”. Kijana akagunduwa yule bint si mtu wa kawid,

 

Yule kijana kusikia vile kwa uhodari alio nao akaruka kweye farasi haraka na kuondoka. Baada ya mwendo wa dakika kadhaa akakutana na njia ya kuelekea kwao. Alipofika akamweleza baba yake kuhusu kilicho tokea. Mfalme alikasirika na akamwadhibu waziri kwa kutokuwa makini na kusababisha ajali kwa mwanae.

 

Baada ya kusimulia hadithi hii waziri akamwambia mfalme “angalia sana mfalme, unaonekana umemwamini sana tabibu, lakini usijejuta kwa kumuamini kwako kama alivyojuta huyu mfalme aliyemwadhibu waziri wake baada ya kumwamini”. Maneno haya yalimpenye sana mfalme, hivyo akaamuwa kumuamini waziri wake. Hivyo akaamuwa kumuuwa yule tabibu wake.

 

Siku iliyofuata akaamrisha askari wakamkamate tabibu na kumleta mbele yake. Tabibu akiwa hajui kinachoendelea, anashangaa kuambiwa amekamatwa kwa kosa la kupanga njama za kumuua mfalme. Tabibu akawa anajitetea “sasa kama ningetaka kumuuwa mfalme ina maana gani nikamponya?”. Ijapokuwa alizidi kujitetea lakini mfalme alishaamuwa ubaya hivyo hakusikiliza maelezo yake.

 

Katika hali ngumu kama hii, yule tabibu akataka apewe ruhusa ya mwisho kuzungumza. “zungumza bila shaka, hata uzungumze vip leo utauliwa tu rafiki yangu tabibu.”. Ni maneno yaliyojaa kejeli kutoka kwa mfalme. Tabibu akazungumza “mimi sina kosa mfalme, ninaapa kwa jina la Allah, mimi sina kosa kabisa, lakini kama haina budi mimi kuuliwa, kuna kitabu changu kipo nyumbani, kitazungumza ukweli wote, juu yangu mimi. Kitabu hiki kitazungumza pindi utakapo niua”.

 

Baada ya mazungumzo haya mfalme akapatwa na mshangao na kuzungumza kimoyomoyo “yaani ili hicho kitabu kizungumze ukweli wa mambo mpaka wewe nikuuwe ndo kizungumze? Hii kweli ni khabarikubwa. Basi sina budu kukuuwa ili nione maajabu ya kitabu kinachozungumza”. Mfalme akamuuliza tabibu tukupe muda gani ukakilete hicho kitabu? “miachieni leo ili niweze kukiandaa kisha kesho nitakuja nacho hapa, na hukumu yangu itatekelezwa.” ni maneno ya tabibu kumwambia mfalme.

 

Basi mfalme akaamrisha askari wake wamlinde tabibu. Tabubu alipotoka pale akaenda nyumbani kwake na kuiaga familia yeke kwa uchungu na machozi ya hali ya juu. Baada ya pale akachukuwa hicho kitabu akakipaka dawa iliyo na rangi ya kijibu. Dawa hii ipo kama ungaunga, na haina harufu kali. Akakipaka kitabu kurasa zote. Ilipofika asubuhi akachukuwa beseni la maji lakini halikuwa na kitu ndani na akatoka kwake akiongozwa na askari wa mfalme. Alipofika sehemu ya hukumu akaanza kutoa maelekezo yake.

 

“nitakapokuwa nimeuliwa chukueni kichwa changu kisha kiwekeni juu ya kitabu kilichopo kwenye beseni hili. Pindi damu itakapoanza kutotesha gamba la nje la kitabu hiki mfalme atakichukuwa na kufungua mpaka ukurasa wa 6 wa kitabu hiki.” haya yalikuwa ni maelekezo ya tabibu kwa mfalme kuonesha maandalizi ya kitabu kitakachozubgumza. Basi haukupita muda dabibu akauawa kwa upanga.

 

Kwa shauku mfalme akafuata maelekezo kama alivyoambiwa. Damu ilipoanza kutotesha kitabu akakichukuwa kwa shauku kubwa. Akawa analamba kidole chake kutia mate ili afunguwe kurasa kwa urahisi, kichwa kikasema “funguwa mpaka ukurasa wa sita”. Akaanza kufunguwa huku anatia mate kidole na kisha nafungua, alifanya hivi mpaka akafika kurasa wa sita na hakukuta maandishi yoyote. Kichwa kikasema “fungua mpaka mwisho” akaendelea kufungua huku analamba kidole kutia mate, mpaka akafika mwisho na asione chochote.

 

Ghafla macho yake yakaanza kulegea na mwili ukaanza kupoteza nguvu, damu zikaanza kutoka puani, kisha kichwa kikaseme “na ukatili wako, haukujuwa kama ulikuwa ukilamba sumu iliyopo kwenye kurasa. Umebakiwa na muda mchache kufa. Hivi ndivyo watu waovu wanavyolipwa uovu.” baada ya maneno haya kichwa kikapoteza maisha na haukuchukuwa muda mfalme akafa huku anajuta kwa kumuua tabibu na kuamini maneno ya waziri wake.

 

Baada ya kumaliza kusimulia hadithi hii mvuvi akamwambia jini “kama mfalme angemwamini tabibu na kupotezea maneno ya waziri wake, haya yole yasingetokea. Hivi pia ndivyo itakavyokuwa kati ya mimi na wewe, nikikuamini nitajuta. Hivyo mimi nakutupa baharini sasa hivi na nitaweka alama na tangazo hapa ili kula mvuvi ajuwe kilichopo hapa nin nini. Na nitajenga na nyumba pia nitakaa hapa kuwaonya wavuvi.

 

Jini kusikia maneno haya akamwambia usinifanyie kama imma alivyomfanyia ateka. Mvuvi kwa shauku akauliza “kwani imma alinfanyia nini ateka?”. Jini likamjibu “unadhani nitakwambia wakati umenifungia humu?, nifungulie na nakuahidi nitakufanya tajiri maisha yako yote, nakuahidi”. Mvuvi kwa kupenda mali akakubali ahadi ya jini na akamfungulia, jini lilipotoka likapiga teke chupa ile na likacheka kwa sauti ya juu. Hali hii ilimuogopesha sana mvuvi. “usiogope rafiki yangu, nimefanya hivi kukutisha tuu, mimi naamini sana ahadi”. Ni maneno ya jini kumwambia mvuvi. Kisha akamwambia amfate na achuuwe na nyavu zake.

 

Walikwenda upane wa magharibu na mji wakauacha upande wa kusini. Walikwnda kwa muda usiopunguwa masaa saba. Kisha wakakutana na milima minne. Wakaipanda milima ile juu ya milima wakakuta kuna kijibwawa cha maji yaliyo meupe sana. Kisha jini akamwambia mvuvi atupe nyavu yake. Alipotupa akavuwa samaki wanne wa rangi tofauti. Mvuvi alishangaa hajawahi ona samaki wenye umbo na rangi kama hizi maishani kwakwe. Kisha jini likamwambia “chukuwa samaki hawa na ukawauze kwa mfalme, utapata utajiri bila shaka. Ila kumbuka utavua hapa kwa siku mara moja tu?” kisha jini likapiga miguu yake chini na kupotea.

 

Mvuvi akatoka na samaki wake wale na akakutana na mpishi wa mfalme, mpishi akawachukuwa samaki wale mpka kwa mfalme. Mfalme alishangaa uzuri ulioje wa samaki wale. Akawanunua kwa pesa nyingi sana iliyomfanya mvuvi asahau maisha ya kimasiki jitena. Mpishi akatoka kwendapika samaki wale. Akaanza kuwakaanga , pindi walipoanza kuiva, upande mmoja akawageuza ghafla akashangaa ukuta wa jiko umepasuka na kukatokea mwanamke mzuuri. Mwanamke yule akaaambia samaki “je mnafanye kazi niliyo watuma?” samaki wakamjibu “ndio tunafanya kaz” kisha mwanamke yule akapiga teke karai lile na samaki wakaanguka na kugeuka mkaa. Baada ya hapo akapoka na ukuta ukarudi ukawa kama vile ulivyokuwa.

 

Matukio yote haya yakifanyika mpishi aliyaona, na alikuwa akishangaa. Zaidi ni pale alipoona samaki wa mfalme wamegeuka mkaa, aliogopa sana na akatoka kumtafuta mvuvi ili amwambie amletee wengine. Kwa kuwa mvuvi aliwauza wawili akampatia wale wawili walobakia kwa pesa nyingi sana. Kisha mpishi akaenda jikoni. Tukio lielile likatokea tena na samaki wakageuka mkaa. Mara hii aliamua kumweleza mfalme mfalme alishangaa sana na kaamrisha aletwe mvuvi. Mvuvi alipofika akampewa amri ya kuleta samaki kama wale siku itakayofata.

 

Mambo yakawa kama hivi siku ilofata mvuvi akawaleta samaki wale na akapewa pesa kama ile ya jana mara mbili yake maana amempa wote wanne. Mfalme akaingia jikoni mwenyewe na akaanza kuwakaanga. Tukio kama la jana likatokea tena na samaki wakageuka mkaa. Sasa mfalme akaona hawa sio samaki wa kawaida. Akaagiza mvuvi aletwe. Alipokuja mvuvi akamweleza nataka unipeleke nikapaone hapo unapovua samaki hawa. Mvuvu akawaeleza ni bali lamda kwa kesho. Mvuvi alijitetea hivi akiogopa ahadi aliyoekeana na jini

 

Basi siku iliyofata mfalme akatoka na msafara wake kuelekea kule kwenye bwawa. Wakafika mida ya mchana, kwenye bwawa lililozungukwa na milima minne. Watu wote walistaajabu kuona bwawa likiwa milimani na lina maji masafi sana kiasi kile. Kila mmoja alitamani luyaonja maji yale. Ilipofika jioni mfalme akamwagiza mlinda mlango kuwa anatoka lakini asimwambie mtu yeyote. Na atakaemuuliza mwambie amesema hataki kusumbuliwa. Basi mambo yakawa kama hivi.

 

Usiku ule mfalme alitoka na upanga wake akiwa anazunguruka katika eneo lile, alikuwa akisaidiwa na mwanga wa mwezi ulioonekana unawaka sana. Katika kuzunguruka akaona kinjia kidogo kinaelekea upande wa ashariki kutokea kwenye ziwa. Akafata njia ile akakutana na bostani nzuri, yenye maua na matuta mazuri sana. Alistaajabishwa na bostani ile yenye vitu vizuri ambavyo kwenye ufalme wake havipo. Kwa sahuku aliendelea kuchunguza ndani mule kuona maajabu zaidi.

 

Kwa muda mrefu katika kuzunguka kwake alikutana na geti kubwa la rangi ya dhahabu, akaingia kupitia geti hili. Akakutana na njia iliyowekwa taizi za almasi. Alishangazwa na ururi ulioje wa njia hiyo. Mbele yake akakutana na kitu kizuri, kiti hiki kimenakshiwa dhahabu na fedha. Kuangalia vizuri akaona kwenye kiti kiel kuna mtu amekaa. Mtu huyu ni wa ajabu sana, alikuwa ni jiwe kwa chini mapaka kiunono. Kuanzia kiunini mpaka juu ni mtu aliye sawa.

 

Kwa shauku mfalme akataka kujuwa nini kunaendelea eneo lile. Akawa anamuuliza kuhusu yeye ni nani na anafanya nini pale. Na ni kipi kimetokea eneo lile. Maswali yote aliuliza bila ya kujibiwa. Kijana yule alikuwa anatokwa na machozi muda wote ule. Kisha kijana akaanza kuzungumza “hayo maji unayoyaona sio maji, na hao samaki unaowaona ni watu. Hiyo milima ni visiwa na mimi ndiye mfalme wa eneo hili” ni maneno ya kijana aliye jiwe nusu. Mfalme akauliza nini kilitokea sasa. Kijana akaanza kusimulia hadithi ya eneo hili kama ifuatavyo;-           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021-11-08     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1007


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Safari ya tatu ya Sinbad
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

Kitabu Cha hadithi ya Chongo
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

Safari ya nne ya Sinbad
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

Kisa Cha mfugaji na mkewe
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Safari ya majibu juu ya maswali mawili
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

HADITHI ZA ALIF LELA U LELA: HADITHI YA WANAWAKE WATATU NA CHONGO WATATU
Soma Zaidi...

ALIF LELA U LELA: UTANGULIZI
ALIF LELA U LELA. Soma Zaidi...

Kitabu Cha Hadithi ya kifo cha Damu
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

Usaliti unaanza hapa
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

HADITHI ZA SINBAD
Soma Zaidi...

Hadithi za Sinbad
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

HADITHI YA BINTI MWENYE KUFICHWA MTOTO WA MFALME
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA BINTI MWENYEKUFICHWA, MTOTO WA MFALME. Soma Zaidi...