Haki ya kumiliki mali na mipaka yake katika uislamu

Je unaijuwa mipaka yako katika kumiliki mali. Ama unajuwa haki zako katika mali inayomiliki. Endelea na somo

Haki ya kumiliki mali

 


Kumiliki mali ni suala la kimaumbile na limeshikamana na silka ya kujihami (self presevation).Katika historia ya binaadamu suala la kumiliki mali limekuwa likiandamana na itikadi au falsafa inayotawala mahali.

 

Kwa mfano katika baadhi ya jamii za kitwaghuti umilikaji wa mali uko chini ya familia au huwa chini ya “watu wote” (mali ya umma) au huwa chini ya mtu au watu binafsi. Katika Uislamu kila kitu kipo chini ya miliki ya Mwenyezi Mungu:

 

“Sema Ee Mola uliyemiliki Ufalme wote! Humpa ufalme umtakaye na humuondolea ufalme umtakaye na humtukuza umtakaye na humdhalilisha umtakaye, kheri imo mikononi mwako. Bila shaka wewe ni Mwenye Uwezo juu ya kila kitu ”. (3:26).

 


Hivyo ni dhahiri kuwa Mwenyezi Mungu ndiye mmilikaji wa hakika wa vitu vyote. Binaadamu anamiliki mali kwa dhamana tu siyo kwa hakika na kwa sababu hiyo ataulizwa jinsi alivyotumia. Katika Qur-an Allah (s.w) ameruhusu watu binafsi au kwa vikundi kumiliki mali pale aliposema:

 

“Chukua sadaka katika mali zao, uwasafishe kwa ajili ya hizo (sadaka zao) na kuwataja kwa vizuri (mbele yangu) na uwaom bee dua. Hakika kuwaombea kwako kutawapa utulivu (watengenekewe); na Mwenyezi Mungu ndiye asikiaye na ajuaye.” (9:103)

 

Hivyo Uislamu unakubali na kuheshimu haki ya mtu au watu binafsi kumiliki mali.

 


Mipaka ya Umilikaji mali
(i)Mali hiyo iwe imechumwa kwa njia ya halali. Uislamu unaitambua haki ya kumiliki mali na haki ya kuilinda mali hiyo, lakini mali yenyewe iwe ya halali.

 


(ii)Mtu anaweza kuiuza au kuitumia mali yake apendavyo maadamu ana akili timamu. Iwapo hana akili timamu, itabidi apatikane mdhamini wa kuingalia mali hiyo kwa niaba na manufaa yake na manufaa ya jamii.

 


(iii)Maadamu mtu anayo mali basi anao pia wajibu wa kutekeleza majukumu yanayohusiana na mali aliyo nayo.

 


(iv)Uislamu unakataza ubakhili na israfu (ubadhirifu) katika matumizi. Mwenyezi Mungu anasema:

 

Wala usifanye mkono wako (kama) uliofungwa shingoni mwako, wala usikunjue ovyo ovyo, utakuwa ni mwenye kulaumiwa na kufilisika. (17:29).

 

Enyi wanaadamu! Chukueni mapambo yenu wakati wa kila sala; na kuleni (vizuri) na kunyw eni (vizuri). Lakini msipite kiasi tu. Hakika Yeye hawapendi wapitao kiasi. (7:3 1).

 

Ubadhilifu ni kufanya mojawapo ya mambo matatu
Kwanza,
 kununua kitu usichokihitaji. Au kununua kitu unachokihitaji lakini kwa kiasi kingi kuliko unavyoweza kutumia. Kwa mfano kutengeneza chapati tano ilihali uwezo wako ni wa kula chapati mbili tu, halafu zile tatu ukazitupa jalalani.

 

Pili ni ubadhilifu kununua kitu chochote kile cha haramu, hata ikiwa kwa thamani ndogo namna gani. Kwa mfano hata kama masanduku laki moja ya bia yanauzwa kwa shilingi hamsini ukiitoa shilingi hamsini hiyo kununua pombe hiyo unaandikiwa madhambi ya ubadhilifu.

 

Tatu kutoa sadaka kwa ajili ya kujionesha kwa watu, badala ya kuandikiwa thawabu unaandikiwa madhambi ya israfu.

 


(v) Uislamu unakataza rasilimali zilizo katika jamii kuachwa bila kutumiwa Mtume (s.a.w) amesema mtu akiendeleza ardhi ana haki ya kuimiliki. Lakini akiiwacha kwa miaka mitatu bila kuitumia mtu mwingine ana haki ya kuiendeleza na kuimiliki.

 Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/08/26/Friday - 08:25:04 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 866


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Madhara ya riba kwenye jamii
Haya ni madhara ya riba katika jamii. Ni kwa namna gani jamii inadhurika kutokana na riba? Soma Zaidi...

Sera ya uchumi katika uislamu
Hapa utajifunza sera za kiuchumi katika uchumi wa kiislamu. Hapa utajifunza sera kuu tatu za uchumi wa kiislamu. Soma Zaidi...

Jukumu la serikali katika kuzuia dhuluma
Serikali ina nafasi kubwa katika kuzuia dhulma na kufanya uchumibuwe huru kuyokana na dhulma. Soma Zaidi...

Mifumo ya benki ya kiislamu.
Hapa utajifunza njia ambazo nenk ya kiislamu hutumia ili kujiendesha Soma Zaidi...

Njia haramu za uchumi.
Njia hizi ni haramu katika kukuza uchumi wako. Soma Zaidi...

Mgawanyiko katika kuitumia mali unayomiliki
Unajuwa namna ambavyo matumizi ya mali yako, yanavyogawanywa? Jifunze hapa mgawanyiko wa mali yako. Soma Zaidi...

Mifumo ya benki na kazi zake
Hapa utajifunza kazi za benki. Soma Zaidi...

Nafasi ya serikali katika ugawaji
Serikali ina nafasi katika kufanya mgawanyiko katika uchumi. Soma Zaidi...

Ni kwa nini riba imeharamishwa kwenye Uislamu
Hapa utajifinza uharamu wa riba na sababu za kuharamishwa kwake. Soma Zaidi...

Uislamu unavyokemea tabia ya ombaomba
Uislamu umekataza tabia ya kuombaomba kama ndio njia ya kuendesha maisha. Pia ukaweka suluhisho la kukomesha tabia hiyo Soma Zaidi...

Mambo muhimu ya kuzingatia katika kujenga uchumi wa kiislamu
Nazingatio muhimu katika uchumi unaofuata sheria za kiislamu. Soma Zaidi...

Ni nini maana ya uchumi katika uislamu
Katikabuislamu dhana ya uchumi imetofautiana na dhana ya kidunia hivi leo ambapo kamari na riba ni moja ya vitu muhimu katika uchumi. Soma Zaidi...