Haki za muislamu kwa muislamu mwenziwe

Haki za muislamu kwa muislamu mwenziwe

Hizi ndio haki kuu tano unazopasa kumpatia Muislamu mwenzio.

HAKI 5 ZA MUISLAMU ANAZOPASA KUPEWA: 

 
وعن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال‏:‏ ‏"‏حق المسلم علي المسلم خمس‏:‏ رد السلام، وعيادة المريض، واتباع الجنائز، وإجابة الدعوة، وتشميت العاطس” ‏(‏‏(‏متفق عليه‏)‏‏)
 
 
 
Imesimuliwa kutoka kwa Abu Hurairah kuwa Mtume s.a.w amesema : "Haki za muislamu kwa muislamu mwenziwe ni tano: kurudisha salamu, kumuangalia anapoumwa, kuifuata jeneza lake, kuitikia wito anapokuita, na kumuombea dua anapopiga chafya". 
 
 
Maelezo
Kwa mujibu wa hadithi haki hizo ni; -
1. Kujibu salamu ya Muislamu anapokusalimia. Hii inamaana kujibu salamu ni jambo la lazima. Endapo hutajibu salamu baada ya kusalimiana utakuwa umevunja haki hivyo utaingia kwenye makosa. 
 
 
2. Kwenda kumangalia anapoumwa. Nibsunnah kumuombea dua mgonjwa. Unapomuangalia mgonjwa unafaidika wewe na yeye kiroho na kiafya pia. 
 
 
3. Endapo atafariki ni haki yake kumsindikiza kwa kilifuata jeneza lake hadi kwenda kumzika. Hii inaambatana na kumswalia. Hata hivyo sio lazima kwako endapo wapo walioshiriki kumswalia. Hata hivyo kama huna uhuru ni haki yake umshindikize mpaka atakapozikwa. 
 
4. Endapo muislamu mwenzio atakuita ni haki yake kuitikie wito huo. Nenda kwanza kasikilize anakuitia nini,  kisha kukubali na kukataa hupatikana baada ya kujuwa wito ulikuwa na sababu gani. 
 
Hata hivyo haki hii inatakiwa ifanyike kwenye misingi ya sheria. Sio sawa kumuita mwanamke katika mazingiravtatnishi.  Ama hata mwanaume kumuita mwanaume kwenye mazingira hatari. Hivyo kwa kuangalia usalama wako pia haki hii inapaswa kutekelezwa katika misingi salama. 
 
 
5. Kumuombea dua anapopiga chafya. Endapo atapiga chafya na akasema alhamdu lillah wewe unatakiwa umwambie yarhamuka llahu. Kisha yeye anatakiwa ajibu yahdikumullahu wayuswlih baalakum. 
 

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Views: 2163

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 web hosting     👉4 Simulizi za Hadithi Audio     👉5 Dua za Mitume na Manabii     👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    

Post zinazofanana:

Mifumo ya benki ya kiislamu.

Hapa utajifunza njia ambazo nenk ya kiislamu hutumia ili kujiendesha

Soma Zaidi...
Mifumo ya benki na kazi zake

Hapa utajifunza kazi za benki.

Soma Zaidi...
Aina za Najisi na twahara katika uislamu

Post hii inakwenda kukufundisha aina za najis. Pia utajifunza aina za twahara katika uislamu

Soma Zaidi...