HAKI ZA NAFSI


image


Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)


Haki za Nafsi.

Haki za nafsi imekokotezwa kuanzia binafsi, familia, wazazi, n.k kama ifuatavyo;

Mtu Binafsi.

Haki za msingi ni chakula, makazi, malezi, elimu, mavazi, matibabu na kufanyia kazi vipaji na neema alizonazo inavyostahiki ikiwemo;

Haki ya Macho.

Ni kutazama yaliyoamrishwa na kuyaepusha na yaliyoharamishwa.

 Rejea Quran (17:36), (41:20), (24:30-31) na (20:131).

 

Haki ya Masikio.

Ni kusikiliza yaliyoamrishwa na kutosikiliza yaliyoharamishwa pia.

Rejea Quran (8:22) na (6:25).

 

Haki ya Midomo na Ulimi.

Ni kula, kunywa na kuzungumza yaliyohalalishwa na sio yaliyoharamu.

Rejea Quran (16:114), (17:26-29), (17:53), (41:33) na (31:6).

 

Haki ya Mikono na Miguu.

Ni kushika na kuendea vyote vilivyoamrishwa na kuacha vilivyokatazwa.

Rejea Quran (25:72) na (31:18).

 

                     (b)  Haki za Familia.

Ni kusimamia malezi, elimu, uadilifu na wajibu wa kila mmoja katika familia    kwa muongozo wa Quran na Sunnah ili kuleta kufikia lengo la kuumbwa.

Rejea Quran (52:21).

 

                    (c)  Haki za Watoto.

Watoto wana haki ya kupata malezi na makuzi bora kulingana na mahitaji yao kwa mujibu wa mafundisho ya Quran na Sunnah katika sehemu zifuatazo;

 

Haki ya Uhai.

Uhai wa mtoto ni haki itokayo kwa Mwenyezi Mungu (s.w) kupitia malezi na makuzi ya wazazi. 

 

Haki ya Nasaba.

Mtoto kupata nasaba ni haki kisheria ili kuwa mwanafamilia halali.

Rejea Quran (33:4).

 

Haki ya Makuzi na Malezi bora.

Makuzi na malezi bora ya mtoto ni kupata haki zake za msingi na elimu inayomuwezesha kumuabudu Mwenyezi Mungu (s.w) ipasavyo.

Rejea Quran (66:6).

 

                    (d)  Haki za Wazazi.

Ni kuwahurumia, kuwaheshimu, kuwafanyia wema, kuwahudumia na      kuwalea ipasavyo.

Rejea Quran (31:14), (17:23-24), (4:36), (6:151), (19:14) na (19:32).

 

                    (e)  Haki za Jamaa na Majirani.

Ni kutunza uhusiano na kusaidiana pale inapohitajika kwa kuzingatia mipaka.

Rejea Quran (2:215).

 

                     (f)  Haki za Mayatima, Wajane na Masikini.

Ni kuwahifadhi na kuwasaidia wanapokuwa na shida na mahitaji ya kimaisha.

Rejea Quran (2:220), (4:2), (4:10), (2:262) na (2:267).

                    (g)  Haki za Udugu wa Kiimani na za Watu wengine.

Udugu wa kiimani ni haki na bora zaidi kuliko udugu wa damu au nasaba.

Rejea Quran (49:10), (49:13), (7:172-173), (4:7) na (5:8). 



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    2 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    3 Jifunze fiqh       ðŸ‘‰    4 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    5 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    6 Magonjwa na afya    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Mafunzo yatokanayo na maandalizi haya ya ki ilhamu
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Maswali juu ya Nguzo za uislamu
Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Maswali juu ya mtazamo wa uislamu kuhusu dini
Mtazamo wa uislamu kuhusu dini (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Mambo anayofanyiwa maiti baada ya kufa
Dhana ya faradh kwa muislamu (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Sababu za kutokubalika kwa vitabu vilivyotumwa kuwa muongozo sahihi wa maisha ya mwanadamu zama hizi
Soma Zaidi...

image Wanaowajibika kuhijji
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Mambo yanayodhaniwa kuwa yanaharibu funga lakini hayaharibu
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Mtazamo wa uislamh juu ya ibada
Katika kipengele hich tutajifunza dhana ya ibada katika uislamu,maana ua ibada Soma Zaidi...

image Sanda ya mwanaume na namna ya kumkafini
Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Nafasi ya Elimu katika uislamu
Je ni ipi nafasi ya Elimukatika dini ya uislamu? Soma Zaidi...