Posti hii inahusu zaidi hasara za kuwa na wivu na kutokuwa wazi, sehemu hii inahusu zaidi maendeleo ya Lisa shuleni yanakuwa mabaya zaidi na lina anaendelea kumtunzia siri lengo lake lina ni kuendelea kuwa wa kwanza darasani.
1. Basi Lisa akawa jambazi kabisa na siku nyingine akawa anatoka nyumbani usiku na kwenda kwa mpenzi wake na akigunduliwa na mama yake anamdanganya kwamba kuna mtu alinipeleka usiku,kweli mama Lisa akaumia kweli na akaamua kwenda kwa mganga na waganga walivyo waongo, yule mganga akamwambia kwamba ni rafiki yako yaani mama lina ndiye anayemchezaea mtoto wako, kwa hiyo mama Lisa akakumbuka na neno alilolisema lina siku Lisa anakuja aliumia mno kwa hiyo mama Lisa akaamua kwenda kwa mama lina akiwa na hasira kubwa na kulalamika kuhusu yote anayotendewa mwanae.
2. Basi mama lina akaumia sana na akaamua kumuuliza mwanae lina kwa nini Lisa anafeli darasani na lina alikosa jibu la kumpa mamae ila mama yake alipombana zaidi ndipo akaamua kumwambia kila kitu kwamba lisa aendagi darasani na anashinda na mvulana, kwa hiyo mama lina aliumia sana akataka kumwambia mama Lisa ila alikosa jinsi na baadae aliamua kumwambia ila mama Lisa alikataa kabisa, basi hali ya Lisa ikawa mbaya zaidi, na walipofanya mtihani wa kuingia darasa la saba alikuwa mtoto wa tisini na tano kati ya mia moja ila Lina alikuwa wa kwanza, mama Lisa akaongeza chuki zaidi juu ya lina na mamaye.
3. Basi mama Lisa akaenda kwa watu mbalimbali akitangaza kuwa mama lina ni mchawi na amemfundisha mwanae lina naye ni mchawi kwa hiyo watu wakachukia wakataka kumfukuza mama lina kwenye nzengo yao ila wakampa mwaka mmoja kusudi mtoto amalize shule na akimaliza hawataki kumwona pale, kwa sababu baba yake lini alifariki lina akiwa mdogo kwa hiyo ilikuwa ni shida kubwa kwa mama lina kuhama pale kwa hiyo alitafuta sehemu kila kona na hakufanikiwa kwa sababu alikua hana kipato kikubwa cha kununua kiwanja kwa hiyo aliamua kumpigia mama wa kambo wa Lisa ili kumwambia kila kitu jinsi mke mwenza alivyofanyia .
4. Basi kwa sababu mama wa kambo wa Lisa lengo lake ni kuharibu maisha ya Lisa alipata nafasi nzuri ya kuharibu, kwa hiyo yule mama wa kambo wa Lisa alikuwa na pesa na alichokifanya ni kuhakikisha kujua ukweli kupitia kwa mama lina na kuhakikisha kwamba Lisa anaharbiwa kila kitu, kwa hiyo mama lina alipatiwa kiwanja na mama wa kambo wa Lisa na pia akamjengea nyumba nzuri na akasubiri mtoto wake amalize la saba wahamie huko, basi kwa sababu mama wa kambo wa Lisa alijua ukweli wote na tatizo la Lisa ,akaamua kumwambia mkewe kwamba wamlete tena mtoto nyumbani wamtafutie mwalimu awe anamfundishia nyumbani na baba Lisa akakubali.
5. Kwa hiyo mama wa kambo wa Lisa akamwambia nitamtafuta mwalimu na baba lisa akakubali, kwa hiyo mama wa kambo wa Lisa akamwendea mama lina wakamtafuta yule mwalimu anayempenda Lisa wakaongea naye na kuhaidi kumlipa hela kubwa na kumpatia sehemu ya kuishi, na yule mwalimu akakubali kazi ile na Ela ilikuwa kubwa na kufika kuanza kazi akakuta mwanafunzi ni Lisa akafurahi sana kwa sababu alikuwa anatafuta alipo hakufanikiwa kumpata kwa sababu Lisa hakuwa na simu, basi yule mama wa kambo akamwambia baba Lisa kwamba Lisa anapaswa kuwa na chumba chake karibu na mwalimu ili akipata shida kimasomo mwalimu anafundisha, na baba Lisa akakubali lile ombi.
6. Basi maisha ya kusoma yakaanza siku zote Lisa alikuwa analala kwa yule mwalimu wake yaani walikuwa kama mke na mme na yule mama wa kambo wa Lisa alifahamu hilo akafurahi sana akatamani yule Lisa ababeshwe mimba na kuharibikiwa maisha ila kaka alikuwa makini, sasa ikafika siku ya kufanya mtihani wa robo muhula, kwa sababu yule kaka alikuwa anafundisha pale akaiba mitihani akasolve yote na Lisa na Lisa alipokuja kufanya mtihani akawa mtu wa tano ila lina alikuwa wa kwanza,baba yake akafurahi sana akampa yule kijana zawadi ila mama wa kambo wa Lisa hakufurahi kwa hiyo akaanza kumfanyia yule mwalimu visa na kuamua kumfukuza yule mwalimu na kumtafuta mwalimu mwingine kijana ambaye atamfundisha Lisa, ila Lisa kwa sababu alikuwa ni binti wa kuvutia alipendwa na yule kijana ila Lisa alikataa kwa sababu hisia zake zote zilikuwa kwa mwalimu wake.
7. Basi kwa sababu ya hisia za Lisa kwa mwalimu wake akamwambia yule mwalimu kijana kama utanisumbua nitamwambia baba, basi yule kijana akaanza kumfundisha kwa kumtugia mitihani migumu na Lisa anafeli na baba yake anamtukana kwamba hana akili ila yale maswali magumu yalimsaidia kuona maswali ya shule ni marahisi sana,kwa kipindi hicho maisha ya Lisa yakabadilika na akaanza kusoma na yule mama baada ya kuona juhudi za Lisa akaamua kumnunulia simu nzuri sana na kumwekea Salio la kutosha, hapo Lisa akafurahi sana na akaanza kuchati na yule mwalimu na akili zikaanza kupotea tena ila yule kijana siku moja akagundua hilo akapaswa kumsema kwa baba yake na baba alipoona hayo akagundua kwamba tatizo la mwanae ni lipi na akaamua kuonge na mama mzazi wa Lisa kuhusu tabia yake na ndipo mama Lisa aliona aibu na kujifanya kwamba hajui lolote.
8. Kwa sababu baba Lisa alimpenda sana binti yake aliamua kumwamisha bila kumwambia mama wa kambo wa Lisa na akampeleka shule za private akamrudisha darasa la tano, kwa sababu Lisa hakuwa na kitu kinachomsumbua akasoma kwa bidii kubwa na akafahamu kingereza na baada ya mwezi mmoja walimpeleka darasa la sita na akasoma vizuri bila shida na akawa anawazidi wanafunzi wengine na kufanya vizuri sana, kwa hiyo mama wake wa kambo hakujua mtoto yuko wapi na mama Lisa hakujua kwa sababu baba Lisa aliona wote hawana uwezo wa kumwambia mtoto wake ukweli ila watampoteza, ila kwa sababu yule binti alivutia yule kijana aliyemfundisha mara ya pili akawa anamfatilia kwa mbali na ndiye aliyemwambia baba yake ampeleke mbali na akina mama hao wawili.
9. Basi ikafika siku ya likizo yule kijana akamwambia baba Lisa kwamba yeye ana sehemu nzuri na akampeleka Lisa akawa anaishi naye akamshauri vizuri kuhusu kusoma na kutimiza ndoto na yule Lisa akamwelewa kabisa akawa anasoma na yule kijana alikuwa mkali sana kwa Lisa ila lengo lake ni kwamba baada ya Lisa kukaa vizuri na kumaliza aje awe mke wake, kwa hiyo Lisa alikaa huko na kusoma ila mama yake na mama wa kambo hawakujua Lisa yuko wapi,ila baba yake alisema mtoto yuko kwenye mikono salama,
10. Basi Lisa akafanya mtihani wa darasa la saba akafaulu vizuri na baba akampatia yule mwalimu zawadi nzuri kwa sababu ya kumtunza binti yake, sasa swali linabaki kichwani mwa baba je huyu binti pamoja na uzuri wake na akili yake ataenda kusoma wapi?.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Jamvini Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 848
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio
👉2 Kitau cha Fiqh
👉3 Madrasa kiganjani
👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉5 Kitabu cha Afya
👉6 kitabu cha Simulizi
Mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili
Posti hii inahusu zaidi hadithi ya vijana wawili ambapo mtihani unafika ila Jackie hakujiandaa alishutuliwa na marafiki zake baada ya kuona mwenendo wake haueleweki. Soma Zaidi...
WAKATI WA KUFUMBUKA
Post hii ni mwendelezo wa hadithi inayohusu Kufumbuka ambapo , John anaonekana kama sio mtoto wa Mzee maganga kwa sababu na miungu imekili kwa sababu chakula chote kimeliwa na kuisha. Soma Zaidi...
NIMLAUM NANI? (Sehemu ya pili)
Post hii ni mwendelezo wa hadithi iliyopita ambapo Frank aliwakuta Amina ambaye ni mpenzi wake ameumbatiana na James ambaye ni rafiki yake ,kwa hiyo tuendelee kusikia yaliyotokea baada ya Amina na James kukutwa na Franki. Soma Zaidi...
NIMLAUMU NANI part 1
Post hii inahusu hadithi Moja ya kijana maaalufu aliyeitwa Frank, ni kijana aliyekuwa mwaminifu ila amekumbana na wasichana wengi wanamasaliti ukizingatia Frank alikuwa kijana mstaalabu na mwaminifu sana ila anafikia kufanya maamuzi magumu kufuatana na ku Soma Zaidi...
Mtoto wa tajiri na mtoto wa maskini ( sehemu ya tatu)
Post hii inahusu zaidi mtoto wa tajiri na mtoto wa maskini wakipanda gari kuelekea shule kuanza maisha mapya. Soma Zaidi...
Chemsha bongo na bongoclass
Jipime uwezo wako wa kufikiri pamoja nasi. Soma Zaidi...
Mtoto wa tajiri na mtoto wa maskini ( sehemu ya nne)
Post hii inahusu zaidi watoto Hawa wawili wakiwa kwenye kituo cha mapumziko ambapo mtoto wa tajiri anabugia soda aliyopewa na yule mwalimu pia tumbo linaanza tena na anaanza kuendesha Soma Zaidi...
WAKATI WA KUFUMBUKA SEHEMU YA 1
Post hii inahusu zaidi hadithi mpya na nzuri inayoitwa wakati wa Kufumbuka, ni hadithi inayohusu maisha ya kawaida ambapo watu ushindwa kudhamini watu wa karibu nao na kuona watu wa mbali ndio wenye maana ila shida zikifika ndipo wanaona umuhimu wao. Soma Zaidi...
Mtoto wa Tajiri na maskini ( sehemu ya kwanza)
Post hii inahusu hadithi fupi tu kuhusu mtoto wa tajiri na maskini, palikuwepo na watoto wawili mmoja akiwa mtoto wa tajiri na mwingine wa maskini. Soma Zaidi...
Mwendelezo wa hadithi ya mahusiano ya vijana wawili
Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya mahusiano ya vijana wawili baada ya kuhamia shule mpya. Soma Zaidi...
Mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya sita
Post hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya sehemu ya sita.sehemu hii inaonyesha jinsi bibi alivyo ndumila kuwili na hapendi kuonekana mbaya. Soma Zaidi...
SAFARI YA MUUJIZA
Post hii inahusu hadithi moja iliyotokea Kwa mama mmoja mwenye familia ya watoto watano.ambapo mama aliolewa na mwanaume mwenye maambukizi ya virus vya ukimwi na kupata watoto bila maambukizi kusambaa kutoka Kwa baba kwenda Kwa mama. Soma Zaidi...