Hatari ya kutokwa na damu wakati wa ujauzito
Posti hii inahusu zaidi hatari za kutokwa na damu wakati wa ujauzito, hali hii utokea wakati wa ujauzito ambapo Kuna baadhi ya wajawazito utokwa na damu jambo ambalo hatupaswi kutarajia kwa sababu tunafahamu kabisa mama akishapata ujauzito na damu zinakom
Hatari ya kupata ya kutokwa na damu wakati wa ujauzito.
1. Ikitokea mtu akapata damu kwenye kipindi cha ujauzito Kuna hatari ya mimba kuharibika na kutojifungua mtoto.kwa hiyo kama Mama ana mimba na akaona damu inatoka kawaida kama yupo kwenye siku za mwezi nai vizuri kabisa kuwahi hospital Ili kuangalia zaidi kwa sababu uenda kukatokea hatari ya mimba kuharibika kwa sababu dalili hii sio nzuri kwa mama Mjamzito.
2. Pia Kuna hatari ya kujifungua mtoto kabla ya wakati wake.
Na tatizo hili la kutokwa na damu wakati wa ujauzito Kuna hatari ya kujifungua mtoto kabla ya wakati wake, kwa sababu mimba ikishatungwa hakuna mfumo wowote wa urutubishaji unaotoka na mtu akatokwa na damu kama vile Hana mimba kwa hiyo kama ikitokea Mama akatokwa na damu labda inawezekana Kuna maambukizi zaidi ambayo usababisha damu kutoka na hali hiyo usababisha mtoto kuzaliwa kabla ya wakati.
3. Vile vile kutokwa na damu wakati wa ujauzito usababisha kuzaliwa kwa mtoto mwenye uziti wa chini.
Kwa kawaida uzito wa mtoto ni kuanzia kilo mbili na nusu mpaka kilo tatu na nusu, uzito wa mtoto ukianzia kilo tatu na nukta sita na kuendelea hii nayo ni shida na ikitokea mtoto akazaliwa chini ya uzito wa kilo mbili na point nne ni uzito mdogo kwa hiyo Kuna sababu mbalimbali ambazo usababisha mtoto kuzaliwa akiwa na uzito mdogo ni kwa sababu ya kuwepo kwa kitendo cha kutokwa na damu wakati wa ujauzito, kwa hiyo ni vizuri kabisa kuwahi hospitals endapo tatizo hili likijitokeza Ili kuepukana na changamoto hii.
4. Tatizo lingine ambalo linaweza kutokea ni kupungukiwa na damu wakati wa kujifungua.
Kwa kawaida Mama akikaribia kujifungua ni vizuri kabisa kuwa na damu ya kutosha kwenye mwili Ili kuweza kujifungua salama kwa sababu wakati wa kujifungua utokea matatizo mbalimbali kama vile kumwaga damu au pengine mtoto anaweza kuwa amekaa vibaya na wakaamua kufanya upasuaji na damu umwagika kwa hiyo ni vizuri kabisa kuwepo kwa damu ya kutosha ila kwa sababu ya kuwepo kwa tatizo la kutokwa na damu wakati wa ujauzito usababisha damu kupungua mwilini.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Simulizi za Hadithi Audio 👉2 Kitau cha Fiqh 👉3 kitabu cha Simulizi 👉4 Dua za Mitume na Manabii 👉5 Kitabu cha Afya 👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina
Post zinazofanana:
Njia za uzazi wa mpango kwa watu wenye Ukimwi
Posti hii inahusu zaidi njia za uzazi wa mpango kwa watu waliopata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.
Soma Zaidi...Fahamu dalili za hatari kwa wajawazito.
Posti hii inahusu zaidi dalili za hatari kwa mama mjamzito, kwa sababu kuna baadhi ya Dalili zikitokea kwa mama mjamzito ni vizuri kabisa kuwahi hospitali mara moja.
Soma Zaidi...Uchungu usio wa kawaida kwa akina Mama.
Posti hii inahusu zaidi uchungu usio wa kawaida kwa akina Mama, kwa kawaida uchungu unapaswa kuwa ndani ya masaa Kumi na mawili ila Kuna wakati mwingine uchungu unaweza kuwa zaidi ya masaa Kumi na mawili na kusababisha madhara yasiyo ya kawaida kwa Mama n
Soma Zaidi...Mabaka yanayowasha chini ya matiti.
Posti hii inahusu zaidi mabaka yanayowasha chini ya matiti, ni ugonjwa ambao uwapata wanawake walio wengi na wengine hawajapata jibu Sababu zake ni zipi na pengine uchukua hatua za kutumia miti shamba wakidai juwa hospitalini nugonjwa huu hautibiwa, ila n
Soma Zaidi...Sababu za Kukoma hedhi (perimenopause)
Kukoma hedhi hufafanuliwa kuwa hutokea miezi 12 baada ya kipindi chako cha mwisho cha hedhi na huashiria mwisho wa mizunguko ya hedhi. Kukoma hedhi kunaweza kutokea katika miaka ya 40 au 50. Kukoma hedhi ni mchakato wa asili wa kibaolojia. Ingawa pia in
Soma Zaidi...Sababu za Mayai kushindwa kuzalishwa kwa mwanamke
Posti hii inahusu zaidi sababu za kushindwa kuzalishwa mayai kwa mwanamke, ni tatizo ambalo utokea kwa mwanamke ambapo mwanamke anashindwa kuzalisha mayai.
Soma Zaidi...