HATMA YA KINYOZI MAISHANI MWANGU


image


Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani


HATIMA YA KINYOZI MAISHANI MWANGU

Baada ya muda kusubiri ndipo akaletwa kinyozi. Kinyozi alikuwa na upara, na ndevu ndefu zilizokuwa nyeusi sana na zenye afya. Nilipomwangalia vyema niligundua kuwa hakuwa ni mzee. Ijapokuwa sura yake haikuwa ni ngeni sana, lakini sikujuwa hata kidogo niliipata wapi. Sikutaka kujuwa mengi sana, nikamueleza kuwa aninyoe mnyoo wa kawaida sana, na nywele ziwe fupi. Kinyozi naye hakutaka kuchelewa akatoa vifaa vyake na kuanza kunoa kisu, ama kinyoleo chake.

 

Kinyozi alinoa kwa haraka hata nikadhani anaweza kumaliza kichwa changu ndani ya muda mchache sana. Allipomaliza kunoa akakiendea kichwa changu na kuanza kukiangalia vyema. Ghafla akaondoka na kuelekea kwenye vifaa vyake. Kisha akatoa kitu kama yai kisha akaeekeza kwenye jua kwa muda kidogo. Kisha aakaza kunieleza kuwa “siku ya leo ni mbaya sana kwako, unatakiwa unieleze unakotaka kuelekea ili nikusaidie” sikuelewa anazungumzia utumbo gani, nikamwambia aninyoe haraka.

 

Alichokifanya ni akachukuwa kisu na kuninyoa kidogo kisha akaanza tena kunieleza utumbo wake. “baba yako namfahamu sana na alikuwa hafanyikitu bila ya kunishauri, pia nakumbuka nilikuwa nikikubeba sana ulipokuwa ukimsumbua baba yako kwa kutaka safari zisizo kuhusu”. napo nikaanza kukumbuka kuwa kumbe ndio maana ninaifahamu sura yake. Lakini sikuweza kuvumilia utumbo wake aliousema maana muda unazidi kusogea halafu ameninyoa kidogo anaendelea kubwabwaja. Nilimchukia hata nikamueleza kuwa ondoka na nitaita kinyozi mwingine. Aliposikia maneno yakke basi kwa haraka akaendelea kuninyoa tena kidogo kisha akaanza kubwabwaja.

 

Nilijaribu kumdanganya kuwa nina haraka kuna mwaliko nimepewa na rafiki zangu. Nilijuta kuyasema maneno haya maana ndipo akataka tuende sote. Alining’ang’ania sana kuenda, nikamueleza afanye haraka kuninyoa nitamchukuwa. Hapo ndipo akaninyoa kwa haraka, kisha akalinganisha vyema kichwa changu. Alipomaliza nikamuelekeza sehemu aende atanikuta. Alikataa, kabisa kwa madai kuwa anataka tuende wote vinginevyo hataenda.

 

Nilichofanya nikampatia vyakula na vinywaji kisha nikamueleza atangulie huku na mimi nakwenda kutafuta matunda mazuri. Nilichokifanya nikamuelekea aende dukani kwangu, maana kuna kijiwe pale nje, hivyo lazima atawakuta watu. Yote haya nilikuwa nayafanya ili niweze kumtoroka niende kwa mwanamke yule. Nilipanga tukikubaliana nipose kabisa. Kumbe wakati ninawaza haya yeye alitambua fika kuwa yote ninamdanganya tu.

 

Alichokifanya alichukuwa vitu na kuelekea nilipomuelekeza. Na mimi kwa haraka nikatoka na kupotelea mtaani. Nilikwenda mpaka kwenye lile jumba la mzee tajiri, nilipomuona yule binti bila ya kutambuwa kumbe kinyozi alikuwa ananifatilia kwa mbali. Nikaingia ndani, sasa wakati naingia kumbe yule mwenyewe alikuwa bado yupo ikabidi nijifiche mule ndani. Ghafla nikasikia makelele. Mzee tajiri alikuwa akimpiga mtumwa wake kwa makosa aliyoyafanya. Alimpiga na kwa bahati mbaya alifariki dunia.

 

Kinyozi alikuwa akifatilia mambo yote haya kwa ukaribu japo alikuwa kwa mbali. Alitambua kuwa aliyekuwa akipigwa ni mimi, hivyo akajuwa kuwa nitakuwa nimekufa tayari. Alichokifanya alikimbia kwa haraka mpaka dukani kwangu na kuchukuwa vijana kwa wazee wote waliokuwepo pale. Wakaja kwenye jumba la tajiri na kuanza kumzogoma tajiri kwa kosa la kumuuwa mtoto wao. Yaani waliamini mimi mtoto wao nimeuliwa na tajiri.

 

Tajiri hakuwa mwenye kuyaelewa maneno yako vyema ndipo akamuomba mmoja wao aeleze kwa ufasaha hasa nini kimetokea. Ndipo kinyozi akatoka na kusema “Binti yako na mtoto wetu wanapendana, na wewe umemkamata kijana wetu leo ukampiga na kumuuwa hivyo lazma ulipe”. tajiri akawaeleza kuwa mimi hayo mambo siyajuwi na ndio kwanza hivi nina yasikia, na kama huamni ingia ndani ukamtafute kijana wako, kama ukimkuta amekufa nitalipa chochote mkitakacho na hata shingo yangu nitakupatieni”.

 

Kinyozi akatoka na kuingia ndani, akafika kwenye ukumbi ambao nipo. Nilipomuona nikaingia kwenye sanduku kubwa na kujificha. Alipoona hakuweza kuniona aliliburuta sanduku na kutokanalo nje. Nikakurupuka kwenyesanduku lile na kutaka kukimbia. Nilishangaa sana kuona nje kunakundi kubwa la watu. Nikatoa vipande vya dhahabu nilivyo navyo nilivyopanga kumpatia yule binti. Nilivirusha vipande vile vya dhahabu kwenye kundi la watu. Lengo watakapoanza kugombe dhahabu nitatoka mbio.

 

Basi mambo yakawa kama hivyo, watu wakaanza kugombe dhahabu ndipo nikatoka na kukimbia ili nisikamatwe. Ukweli ni kuwa ningekamatwa na yule mzee tajiri bila shaka angeniuwa. Nilipokuwa nakimbia nilishangaa kumuona kinyozi yupo nyuma yangu. Nilikasirika sana, lakini sikuwa na jinsi. Nilikimbia mpaka mbali sana nikakaa kupumzisha nafsi yangu. Kabla sijasimama nikajikwa kwenye jiwe na kuanguka chini Loo!loo nikavunja mguu wangu. Nilipatwa na maumivu makali sana. Nikakaa chini pembeni kidogo baada ya kujiburuza. Na kinyoz akakaa pembeni yangu. “angalia sasa kwa ujinga ulioufanya, nimekosa kukutana na mwanamke wa maisha yangu na nimevunja mguu wangu” ni maneno niliyomwambia kinyizi.

 

“hivi huini kuwa nimekuokoa kutokana na kuuliwa na tajiri” huu ndio upuuzi aliyo nijibu eti ameniokoa. Kisha akaanza kunipa huduma ya kwanza kwenye mguu wangu. Nilikaa kwake kwa muda wa siku tatu, na hata sikutaka kurudi nyumbani kwa kuhofia usalama wa familia yangu. Siku ya nne nikaandika barua ya kumtaarifu yule binti kuwa ninasafiri ila nitarudi kwa ajili yake. Kama bado atanisubiri haitachukuwa muda mrefu. Kisha nikaipiliza barua hii kwa bibi ipeleke.

 

Sikutaka tena kumuona kinyozi wala kuishi naye mji mmoja. Niliandika barua kuipatia familia yangu na kuwaeleza kuwa ninasafiri kidogo. Lengo ni kuwa mbali na kinyozi ili kutuliza nafsi yangu. Nilibeba hakiba yangu na kuja hapa baghadad, ni miezi mingi yamepita, sasa nilishangaa tena leo kumuona hapa. Moyo wangu uliumia sana nilipomuona leo. Na hii ndiyo hadithi yangu mimi na huyu kinyozi.

 

Basi muandaaji wa sherehe akamuuliza kinyozi je anayoyasema ni ya Ukweli. Kinyozi akazungumza kuwa ni kweli kabisa na asingelikuwa yeye kijana angeuliwa kabisa.kisha kinyozi akaendelea kusema “mimi si mtu wa maneno mengi kama walivyo kaka zangu, na nimeokoa maisha ya huyu kijana lakini yeye ananidharau na kuniona kuwa ni mtu muongo na mwenye maneno mengi. Mimi kaka zangi wengine ni vipofu, viziwi, wasio na mikono , na mabubu. Yote haya wameyapata kwa sababu ya midomo yao na maneno yao mengi, ngoja niwasimulie yaliyowapata kaka sangu saba, kisha ndio mtajuwa kuwa mimi si mtu wa maneno mengi, na isingelikuwa ni mimi kijana angekufa”

 

Alipomaliza kusema maneno haya akaanza kuhadithia yaliyowakuta kaka zake sita hata wakapata ulemavu kwenye viungo vyao.



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    2 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    3 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    4 Jifunze fiqh       ðŸ‘‰    5 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    6 Mafunzo ya html kwa kiswahili    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image SAFARI YA MUUJIZA
Post hii inahusu hadithi moja iliyotokea Kwa mama mmoja mwenye familia ya watoto watano.ambapo mama aliolewa na mwanaume mwenye maambukizi ya virus vya ukimwi na kupata watoto bila maambukizi kusambaa kutoka Kwa baba kwenda Kwa mama. Soma Zaidi...

image WAKATI WA KUFUMBUKA SEHEMU YA 2
Post hii ni mwendelezo wa hadithi ambayo Kwa jina inaitwa wakati wa Kufumbuka, ni mwendelezo wa pale maria anawekwa mbele ya wazee Ili akili kwamba John sio mtoto wa Mzee maganga ila maria akikumbuka wazi kwamba John ni mtoto wa Mzee maganga anakataa kukiri na anaangua kilio na watoto pia wanaangua kilio na pia wanaamua kumpeleka Mari kwenye mizimu Ili iweze kuamua. Soma Zaidi...

image USALITI (sehemu ya tatu)
Post hii ni mwendelzo wa hadithi ya ukweli ambayo imetokea siku sio nyingi jinsi Moses alipoacha kumwoa Rhoda naye akachanganyikiwa takribani miaka kama mitano hivi. Soma Zaidi...

image USALITI (sehemu ya kwanza)
Post hii inahusu zaidi vijana wawili ambao ni msichana na mvulana walioingia kwenye mahusiano wakiwa sekondari na wakahaidiana kuoana ila kwa sababu mbalimbali walizokutana nazo kwenye safari yao ya mahusiano mmoja akamsaliti mwingine na kusababisha kupoteza mwelekeo wa maisha ya msaliti wa. Soma Zaidi...

image Hadithi ya waziri aliyeadhibiwa
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Hadithi iliyosimuliwa na mshona nguo
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

image The fastest (anakwenda mbio zaidi)
Posti hii inakwenda kukuletea sifa za mnyama anayekwenda mbio zaidi Soma Zaidi...

image Hadithi ya Khalid mwenye kuneemeshwa na Jalid
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Mshenga wa aladini mbele ya mfalme
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

image Hadithi ya samaki wa Rangi nne
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...