Posti hii inahusu zaidi njia au hatua tatu muhimu anazopitia Mgonjwa wa gauni, kuanzia kwa Maambukizi mpaka kwenye hatua ya mwisho hasa kama Ugonjwa huu haujatibiwa mapema.
1.Hatua ya kwanza ni pale kiroboto mwenye Maambukizi ambaye ameyapata kutoka kwa panya anamngata mtu na kuingiza wadudu ambao kwa kitaalamu huitwa yersinia pestis, wadudu hao hawapiti kwenye mfumo wa mzunguko wa damu bali upitia kwenye lymphatic na kushambulia limfu node za kwenye kwapa, kwenye shingo na sehemu mbalimbali ambazo zina limfu.
2.Pia hizo limfu zinakuwa na Maambukizi hali ambayo ufanya hizo limfu kubwa na ma upele na na upele hayo utoa usaha ambapo Usababisha maumivu makali kwa mgonjwa kwa hiyo Dalili hii kwa watu wengine ushindwa kutambuliwa mapema kama ni tauni au nini kwa hiyo matibabu ulenga zaidi Dalili hali ambayo Usababisha kushindwa kupona na kusababisha hatua nyingine kama tutakavyoona hapo chini.
3.Baada ya Maambukizi kuingia kwenye node uingiliana na mzunguko wa damu hii hatua ya wadudu kuingia kwenye mzunguko wa damu kwa kitaalamu huitwa septicaemia, kwa hiyo kwenye damu wadudu ushambulia mishipa ya damu na kufanya mzunguko wa damu kuwa wa shida hali ambayo Usababisha kupasuka kwa mishipa ya damu na kusababisha kuvuja damu kila mahali.
4.Ugonjwa ukifikia kwenye hali hii wengine udhani kwamba ni ebola na kuanza kuwa tenga na kuwakimbia wagonjwa kwa hiyo ni vizuri kabisa kuhakikisha kuwa dalili za Ugonjwa huu zinatambulika mapema na katika hatua hii matibabu yanaweza kufanya kazi.
5.hatua ya tatu ni pale ambapo wadudu wanasambaa kwenye mapafu ambapo kwa kitaalamu huitwa pneumonic, kwa hiyo wadudu wakizidi kwenye damu uhamia kwenye mapafu na kuweza kuyashambulia, na katika hatua hii mgonjwa anapumua vibaya vibaya na kwa hatua hii mgonjwa anaweza kuambukiza kwa hiyo ni vizuri mgonjwa akifikia hatua hii akaweza kutunzwa vizuri na sehemu yenye hewa.
6 . Kwatika hatua hii ni vigumu kwa mgonjwa kupona kwa sababu Maambukizi yanakuwa yamesambaa sehemu mbalimbali kwenye mwili, kwenye damu na mapafu pia na sehemu nyingine pia ushambulia kwa hiyo tunapaswa kujua Dalili hizi ili kuweza kupambana na ugonjwa huu.
7.pia jamii inapaswa kupewa elimu kuhusu Dalili za Ugonjwa huu na kuweza kutambua Dalili zake mapema ili kuweza kupata matibabu ipasavyo kwa sababu kuna dawa ambazo zinatumika dawa zenyewe ni kama ifuatavyo, dawa za antibiotics kama vile streptomycin, Tetracycline, doxycycline ambazo utumika na kuponyesha Ugonjwa huu.
8.Dawa hizi utumika kama ifuatavyo, kwa kuanza na streptomycin tumia milligram 30, vidonge viwili kwa siku tatu, Tetracycline tumia milligram kuanzia mia mbili hamsini mpaka mia tano mara nne kwa siku kumi, na doxycycline vinatumika kwa siku saba hizi dawa zinapaswa kutumika kwa maagizo ya wataalamu wa afya sio kutumia kiholela tu.
9.pia tunapaswa kujua kuwa ugonjwa huu upo na unatibika kwa hiyo mila na desturi zisizofaa tuziache ili kuweza kuokoa maisha ya watu
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Maumivu ya kifuwa yanaweza kutokea baada ya kubeba kitu kizito, ama kupata mashambulizi ya vijidudu vya maradhi. maumivu ya viungo na hata vidonda vya tumbo. Lakini sasa umesha wahi fikiria maumivu ya kifuwa kwa katikati?
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi ugonjwa wa kuharisha, kuharisha ni kitendo Cha kupitia kinyesi chenye maji inawezekana kina damu au kisichokuwa na damu.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi Maambukizi kwenye mifupa ambayo kwa kitaalamu huitwa Osteomyelitis, ugonjwa huu uaribu zaidi kwenye mifupa na sehemu nyingine ambazo zinakaribia kwenye mifupa
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi msaada kwa aliye na uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo, ni huduma maalumu ambayo utolewa kwa mtu ambaye ana uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo. Zifuatazo ni huduma maalumu kwa mwenye uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo.
Soma Zaidi...Post hii itakwena kukufundisha kuhusu historia fupi ya Ukimwi na matibabu yake. Ni wapi wapo hatarini kupata maambukizi na ni kitu gani wafanye?
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea kama mtu hajatibiwa ugonjwa wa kichaa cha mbwa.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za VVU/ UKIMWI
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na matatizo yanayoweza kusababisha Ugonjwa wa Saratani.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi Ugonjwa wa uti wa mgongo, ni ugonjwa unaoshambulia sehemu inayofunika ubongo na pia sehemu ya spinal cord
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi watu walio kwenye liski ya kupata magonjwa ya ngono, ni watu wanaofanya mambo yanayosababisha kupata magonjwa ya ngono.
Soma Zaidi...