image

Hatua za kupambana na ugonjwa wa UTI

Posti hii inahusu zaidi hatua au mbinu za kupambana na ugonjwa wa UTI kwa sababu ugonjwa huu umekuwa tishio kubwa kwa sasa kwa hiyo tunapaswa kutumia njia mbalimbali ili kuweza kupambana na Ugonjwa huu.

Hatua za kupambana na ugonjwa huu wa UTI.

1. Hatua ya kwanza ni matumizi ya maji ya kunywa na baada ya kunywa maji nenda haja kubwa mara kwa mara ili kuweza kupunguza uchafu mwilini.

 

 

 

2. Katika matumizi ya vinywaji epuka sana vinywaji ambavyo vinaweza kuhatarisha kibofu cha mkojo kwa sababu kama kuna maambukizo kwenye kibofu cha mkojo kupona ugonjwa wa UTI ni ndoto vinywaji vyenyewe ni kama vile kahawa na matumizi mengi ya vinywaji vyenye wingi wa caffeine.

 

 

 

 

 

3. Nenda haja ndogo baada ya kufanya ngono zembe.

Kwa hiyo baada ya kufanya tendo la ndoa nenda haja ndogo ili kama kuna maambukizi yoyote ya ugonjwa wa UTI uweza kuondoka.

 

 

 

 

4. Kawaida jipanguse kutoka mbele kwenda nyuma.

Kwa sababu kujipangusa kutoka nyuma kwenda mbele unasababisha bakteria walio kwenye kinyesi kuja mpaka kwenye kibofu cha mkojo na kusababisha Maambukizi kwa hiyo siku zote wafundishe watoto kujisafisha kutoka mbele kwenda nyuma sio nyuma kwenda mbele.

 

 

 

5. Hakikisha kila siku sehemu za siri ni safi mda wote ili pia kupunguza Maambukizi unapaswa kuosha sehemu za siri bila kutumia sabuni za manukato tumia sabuni ya kawaida ya kipande.

 

 

 

6. Kila mara jaribu kuoga maji masafi na yanayotiririka kwa sababu maji masafi yanasababisha kuwepo kwa hali ya usafi na kuzuia kuwepo kwa Maambukizi kwenye via vya uzazi.

 

 

 

 

7. Kwa kawaida ugonjwa huu mwanzoni ilionekana ni ugonjwa unaowapata sana akina dada au wanawake kwa ujumla ila kwa sasa ugonjwa huu uwapata wote yaani wanawake na wanaume kwa hiyo wote tuna haki ya kupigana na ugonjwa huu ili tuweze kuondokana nao na inawezekana.

 

 

 

 

 

8. Kwa hiyo usipotibu ugonjwa huu unaweza kupata madhara mengi pamoja na ugumba kwa wanawake, kupata kansa ya kibofu kwa mwanaume na madhara mengine mengi.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 963


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Presha ya kushuka/hypotension
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu presha ya kushuka/ hypotension Soma Zaidi...

Aina za minyoo
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu baadhi ya aina za minyoo Soma Zaidi...

Undetectable viral load ni nini?
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maana ya undetectable viral load Soma Zaidi...

Matibabu ya fangasi
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu matibabu ya fangasi Soma Zaidi...

Ugonjwa wa Malengelenge sehemu za siri
Malengelenge sehemu za siri ni maambukizi ya kawaida ya zinaa ambayo huathiri wanaume na wanawake. Makala ya malengelenge sehemu za siri ni pamoja na maumivu, kuwasha na vidonda katika sehemu yako ya uzazi. Lakini huenda usiwe na dalili au ishara za mal Soma Zaidi...

Vyakula hatari kwa mwenye vidonda vya tumbo
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula hatari kwa mwenye vidonda vya tumbo Soma Zaidi...

Dalili za saratani ya tishu (leukemia)
Posti hii inazungumzia kuhusiana na saratani za tishu ambazo kitaalamu hujulikana Kama Leukemia kawaida huhusisha seli nyeupe za damu. Seli zako nyeupe za damu ni wapiganaji hodari wa maambukizo - kwa kawaida hukua na kugawanyika kwa utaratibu, kadri mwi Soma Zaidi...

Dalilili za kukosa oksijeni
Posti hii inazungumzia kuhusiana na dalilili za kukosa oksijeni ambalo kitaalamu hujulikana Kama apnea.kukosa oksijeni ni tatizo ambapo kupumua kwako hukoma na kuanza unapolala. Soma Zaidi...

Tatizo la tezi koo
Posti hii inahusu zaidi tatizo la tezi koo, ni tatizo ambalo uwapata watu mbalimbali ambapo Usababisha koo kuvimba na mgonjwa huwa na maumivu mbalimbali na pengine mgonjwa upata kikohozi kwa sababu ya kuwepo kwa Maambukizi kwenye koo. Soma Zaidi...

Magonjwa ya moyo
Posti hii inahusu zaidi magonjwa ya moyo, kwa kawaida watu wakisikia habari za magonjwa ya moyo huwa hawaelewi yanakuwaje kuwaje, Leo nataka niwafahamishe kuhusu magonjwa ya moyo na sehemu mbalimbali zinazoathirika. Soma Zaidi...

Madhara ya kutotibu ngiri.
Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea pale ambapo Ugonjwa wa ngiri unaposhindwa kutibiwa mapema. Soma Zaidi...

vidonda vya tumbo, dalili zake, chanzo chake na tiba yake
Makala hii itakwenda kukupa elimu juu ya vidonda vya tumbo, nini hasa chanzo chake, vipi vinatokea ni zipi dalili zake, ni zipi njia za kujilinda dhidi ya vidonda vya tumbo. Pia tutaangalia matibabu ya kutibi vidonda vya tumbo. Soma Zaidi...