Hii ndio hutuba ya ndoa ya kiislamu
Hapa utajifunza utaratibu wa hutuba ya ndoa ya kiislamu. Sharti za jutuba ya ndoa na jinsibya kuozesha
Khutuba ya Ndoa
Kabla ya kuozesha (kufungisha ndoa), ni Sunnah kwanza kuleta khutuba ya ndoa (mawaidha ya ndoa) kwa ufupi iii kuwakumbusha wanaooana na Waislamu wengine wachunge ahadi waliyoichukua mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w) kuwa watakaa kwa wema katika maisha ya ndoa na ikibidi kuachana, wataachana kwa wema vile vile.
Ni vyema katika mawaidha haya kuwafahamisha hawa wenye kuoana na kuwakumbusha Waislamu wote waliohudhuria kuwa maisha ya ndoa yatakuwa ya furaha na upendo endapo kila mmoja, mume na mke, atajua wajibu wake kwa mwenziwe na akawajibika kwake ipasavyo. Ndoa iliyofanikishwa kulingana na ahadi ya ndoa ni msingi wa furaha, ushirikiano, utulivu na amani katika familia na jamii kwa ujumla. Ndoa pia imekusudiwa iwaokoe wenye kuoana na adui Shetani na iwasalimishe kwa Mwenyezi Mungu (s.w). Kwa ujumla, katika khutuba hii, ni vyema umuhimu wa ndoa uelezwe kwa muhtasari.
Msisitizo wa Khutuba unaonekana katika hadithi zifuatazo:
Abu Hurairah ameeleza kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema; Ndoa yoyote ambayo ndani yake hamna Tashahhud (Maamkizi ya Mwenyezi Mungu (s.w) ni kama kata isiyo na mkono. (Tirmidh).
Abu Hurairah ameeleza kuwa Mtume (s.a.w) amesema: Jambo lolote muhimu lililofanyika bila ya kumtukuza (Kumhimidi) Mwenyezi Mungu (s.w) kwa utukufu wake, limekosa baraka. (Ibn Majah).
Kutckana na hadithi ilisimuliwa naAbdullah bin Mas'ud (r.a), Mtume (s.a.w) amelündisha tashahud mbili, ya kwanza ni ile ya swala (Tahiyyatu) na ya li ni ile inayopalikana katika khutuba ya kukidhiwa haja, kama vile khutuba ya ndoa, ambayo inaanza na kuendelea kama iluatavyo:
Sfa zote anastahiki Mwenyezi Mungu (s.w). tunamtukuza kwa Utukufu wake, Tunataka msaada wake, na msamaha Wake, na tunajikinga kwake na shari ya nafsi zenu na shari ya vitendo vyetu viovu. Ambaye Mwenyezi Mungu amemuongoa, hakuna awezaye kumpoteza, na ambaye amempoteza hatakuwa na wa kumwongoa. Na ninashuhudia kuwa hapana mola ila Mwenyezi Mungu (s.w), na ninashuhudia kuwa Muhammad ni Mtumwa wake na Mjumbe Wake.
Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu kama ipasavyo kumcha wala msfe ispokuwa mmekwisha kuwa Waislamu kamili. (3:102).
Enyi Watu! Mcheni Mola wenu ambaye amekuumbeni katika nafsi (asili) moja. Na akamuumba mkewe katika nafsi ile ile. Na akaeneza wanaume wengi na wanawake kutoka wawili hao. Na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye kwaye mnaombana.Na (muwatazame) jamaa. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mlinzi juu yenu. (4:1).
Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu na semeni maneno ya Haki Atakutengenezeeni vizuri vitendo vyenu na Atakusameheni madhambi yenu; Na anayemtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake bila shaka amefuzu kufuzu kukubwa. (33:70-71).
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game 👉2 ai web app 👉3 Dua za Mitume na Manabii 👉4 Kitau cha Fiqh 👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉6 Simulizi za Hadithi Audio
Post zinazofanana:
Mwenendo wa mwenye kunuia hijjah na umrah
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Jinsi Uislamu Ulivyokomesha Biashara ya Utumwa wakati na baada ya Mtume Muhammad (s.a.w)
- Uislamu ulieneza nadharia kuwa wanaadamu wote ni sawa na wote ni watumwa mbele ya Mwenyezi Mungu (s.
Soma Zaidi...Maneno mazuri mbele ya mwenyezi Mungu
kuna adhkari nyingi sana ambazo Mtume wa Allah ametutaka tuwe tunadumu nazo. lajkini kuna adhkari ambayo imekusanya maneno matukufu na yanayopendwa sana na Allah.
Soma Zaidi...Aina mbili za talaka zisizo na rejea katika uislamu
Huwezi kuruhusiwa kumrejea mke endapo utamuacha kwa talaka hizi mbili.
Soma Zaidi...