image

Hili ndio lengo la kufunga.

Ni kwa nini Allah ametutaka tugunge. Je kuna lengo gani hasa katika kufunga.

Lengo la Funga

Lengo la funga limebainishwa katika Qur-an pale ilipotolewa amri ya kufunga:

 

“Enyi mlioamini! Mmeamrishwa kufunga kama walivyoamrishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu ”. (2:183)

 

Hapa tunabainishwiwa kuwa lengo la kufunga ni kuwafanya Waumini kuwa wacha-Mungu. Neno “Taqwa ” ambalo linatafsiriwa kuwa ni “Uchamungu” lina maana pana zaidi. “Taqwa” ni hali ya kuhofu ghadhabu za Mwenyezi Mungu (s.w) ambayo humfanya mja ajiepushe mbali na yale yote yanayomghadhibisha Mwenyezi Mungu (s.w) na ayaendee mbio kwa unyenyekevu na kwa jitihada kubwa yale yote aliyoamrisha Mwenyezi Mungu (s.w) na yale yote anayoyaridhia. Maana ya ‘Taqwa’ inabainishwa vyema na Hadith ifuatayo:

 


Siku moja Umar (r.a) alimuuliza Ubbay bin Ka ’b (r.a) amueleweshe maana hasa ya Taqwa. Ubbay (r.a) alijibu: “Amir Muuminin, umewahi kupita njia ya kichaka chenye miba?” Umar (r.a) akajibu: “Naam, nimepita mara nyingi” Kisha Ubbay (r.a) akamuuliza ni hadhari gani uliyoichukua wakati ukipita huko? “Nilishikilia na kukusanya pamoja nguo zangu na kutembea kwa uangalifu katika kupita njia hiyo”, alisema Umar (r.a) ili sehemu yoyote ya nguo zangu isije shikwa na miba hiyo”. Kutokana na jibu hili, Ubbay (r.a) alisema: “Hii hasa ndio maana ya “Taqwa”.

 


Kutokana na mfano huu mtu mwenye “Taqwa” au Muttaq ni yule mwenye shauku na jitihada kubwa kuepukana na kila aina ya mwiba (uovu) katika kila hatua na kila kipengele cha maisha yake yote na wakati huo huo huwa na shauku na jitihada kubwa ya kuyakimbilia mema katika kila hatua ya maisha yake ili kupata radhi za Mwenyezi Mungu (s.w). Muttaq ni mtu mwenye cheo na hadhi kubwa sana mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w) kama tunavyofahamishwa katika Qur-an:

 

“... Hakika aheshimiwaye sana miongoni mwenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule aliye Muttaq (am chaye Mw enyezi Mungu zaidi) katika nyinyi. Kw a yakini Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mw enye khabari ya mambo yote. (49:13).

 


Hiki ni cheo kikubwa sana ambacho hakina mfano wake katika vyeo vya hapa ulimwenguni. Cheo hiki hakipatikani kwa kuomba kura au kwa hongo, bali kinapatikana kwa kujizatiti kujiepusha na makatazo yote ya Mwenyezi Mungu (s.w) na kujitahidi kutenda mema na kutekeleza maamrisho yote ya Mwenyezi Mungu (s.w) kwa matarajio ya kupata Radhi ya Mwenyezi Mungu (s.w).

 





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 756


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Aina za talaka, sharti zake na taratibu za kutaliki katika uislamu
Maana: ni utaratibu wa kuvunja mkataba wa ndoa baina ya mume na mke mbele ya mashahidi wawili kwa kuzingatia sheria ya Kiislamu. Soma Zaidi...

Hukumu ya Mtu asiyefunga kwa makusudi mwezi wa ramadhani
Soma Zaidi...

Umuhimu na nafasi za hijjah katika uislamu
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

sadaka
Soma Zaidi...

Mafunzo ya swala
Jifunze namna ya kuswali, zijuwe aina za swala na ujifunze masharti ya swala, kwa nini swala hazijibiwi? nini kifanyike? Soma Zaidi...

Namna ya kulipa swaumu ya ramadhani na ni nani anatakiwa alipe
Soma Zaidi...

Jinsi ya kuswali swala vitani
Post hii itakufundisha taratibu zinazofanyika ilibkuswalibukiwa vitani. Soma Zaidi...

JIFUNZE FIQH
Fahamu darsa mbalimbali za fiqh kama swala, twahara, zaka pamoja na funga. Zijuwe sharti za swala, funga na zaka. Soma Zaidi...

kanunu na sheria za biashara katika islamu
Soma Zaidi...

Dhana ya kumiliki raslimali katika uislamu
Ni ipi raslimali ya halali kuimiliki katika uislamu. Soma Zaidi...

Jinsi ya kuzika maiti wa kiislamu hatuwa kwa hatuwa
Post hii itakufundisha taratibu za kuzika maiti wa kiislamu hatuwa kwa hatuwa. Soma Zaidi...

Jinsi ya kushona sanda ya maiti na kumvisha yaani kumkafini
Hapa utajifunza taratibu za kumkafini maiti wa kiislamu. Yaani kushona sanda yake na kumvisha. Soma Zaidi...