Historia ya adhana na Iqama na jinsi ya kuadhini.

Hadithi hii inakwenda kukufundisha historia fupi ya adhana pia utakwenda kujifunza jinsi ya kuadhini na kuqimu.

Adhana na iqama

Katika kutekeleza amali ya kusimamisha swala kwa nyakati zake na hasa za mwanzo, kumewekwa mwito maalum wa kuwakumbusha na kuwafahamisha waumini kuingia kwa kila swala. Mwito huu ni Adhana. Adhana ni miongoni mwa sunnah kubwa kabla ya swala.

 

Historia ya Adhana

 


Waislamu walipohamia Madinah walipata hali ya utulivu na amani pamoja na uhuru kamili wa kuabudu. Walipata fursa ya kukutana pamoja kwa swala za jamaa na mashauri mengine yaliyohitajia mkusanyiko wa Waislamu. Hivyo katika hali hii tatizo lililowakabili kwa siku za mwanzo za maisha ya Madinah ni namna ya kuitana kwa mkusanyiko wa swala na mikusanyiko mbali mbali ya Kiislamu. Waliwakuta Mayahudi wakiitana kwa mikusanyiko yao kwa tarumbeta (sauti ya upembe) na Wakristo wakiitana kwa kengele. Namna zote hizi mbili hazikumpendeza Mtume (s.a.w) na Waislamu kwa ujumla. Mtume (s.a.w) aliona kuwa si vyema kuitana kwa mikusanyiko mitakatifu kwa njia hizo za kitwaghuti, bali alipendelea kuwa sauti ya binaadamu ingelitumiwa kufanya kazi hiyo ambayo itaamsha hamasa za waumini na kuleta mwamko mpya wa imani zao na matendo yao. Hali ya mahangaiko ya kutafuta namna ya kuitana inaelezwa vyema katika Hadithi ifuatayo:

 


Ibn Umar amesimulia kuwa: “Waislamu walipokuja Madina, walikusanyika pamoja kwa swala, na walipendelea kufanya hivyo kwa wakati mmoja, lakini hapakuwa na yeyote wa kuwaita. Siku moja ilibidi w ajadili jam bo hili na baadhi yao w akasem a: “Tutum ie kitu kam a kengele wanayotumia Wakristo na wengine wakasema: Tutumie tarumbeta kama mayahudi. Umar akasema: Kwa nini asichaguliwe mtu akawa anawaita watu kwa ajili ya swala? Mtume (s.a.w) akasema: Oh! Bilali, nenda ukawaite watu kwa Swala”. (Muslim)

 


Hadithi hii pamoja na maelezo juu ya historia ya Adhana kwa ujumla hufafanuliwa na hadithi nyingi. Katika Hadithi nyingine tunafahamishwa kuwa maoni waliyoyatoa maswahaba kwenye mkutano wao yalifikishwa kwa Mtume (s.a.w) lakini hayakumvutia. Aliona kwamba si sahihi kutumia njia ya kitwaghuti katika miito mitakatifu, bali alikubaliana na Umar (r.a) kuwa sauti ya binaadamu katika wito huu ni bora kuliko chochote kingine. Pia imesimuliwa katika hadithi iliyopokelewa na Imamu Abu Daud kuwa wakati tatizo hili lilipokuwa bado halijapatiwa ufumbuzi, siku moja, swahaba mmoja, Abdullah bin Zayd alikuja kwa Mtume (s.a.w) na kumsimulia:

 


“Usiku uliopita am enijia ndotoni m tu akishikilia mkononi m wake ken gele na nikamuomba aniuzie; Aliponiuliza, kuwa nataka kufanyia nini chombo kile, nilijibu kuwa, ni cha kuwaitia watu kwenye swala, baada ya kumjibu hivyo alisema: “Siwezi kukufahamisha njia iliyo bora kuliko hiyo? Nilijibu kuwa nilikuwa tayari kumsikiliza aniambie. Hivyo alinifahamishamane

 

Allaahu Akbaru x 2, Allahu Akbar x 2, Ashhadu anllailaha illallah x2, Ashhadu anllailaha illallah x2, Ashahadu annna Muhammadar-Rasuullullaah x2, Ashahadu annna Muhammadar-Rasuullullaah x2, Hayya ‘alas-swalaat-Hayya ‘alasswalaat x2, Hayya ‘alas-swalaat-Hayya ‘alasswalaat x2, Hayya ‘alal-fallah. Hayya ‘alalfallah x2 Hayya ‘alal-fallah. Hayya ‘alalfallah x2, Allahu Akbaru, allaahu Akbaar, Laaillaaha illaallah.

 

NB: x2 maana yake Mara mbili

 

Wakati wa Adhana ya swala ya Asubuhi - Muadhini baada ya kusema Hayya’allal falaah aongeze: Asswalaatu khairum minan-naumi. (mara 2) “Sw ala ni bora kuliko usingizi”. Kisha aendelee Allahu Akbaru hadi mwisho.

 


Kuitikia Adhana

 


Ni sunnah kuitikia adhana kama alivyotufundisha Mtume (s.a.w) katika Hadithi ifuatayo:-
Umar (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: “Muadhini anaposema “Allaahu Akbaru x 2 ”. Mtu aitikie: Allahu Akbar x 2. Kisha anaposema: “Ashhadu anllailaha illallah ”, aitikie: “Ash-hadu anllailaha illallah ”. Kisha anaposema: “Ash-hadu anna Muhammadar-Rasuullullaah” aitikie: “Ashahadu annna Muhammadar-Rasuullullaah ” Anaposema “Hayya ‘alas-swalaat-Hayya ‘alasswalaat”, aseme: “Lahaula walaa Quwwata illa billah” (Hapana hila wala nguvu zinazomkiuka Allah). Kisha akisema: Hayya ‘alal-fallah. Hayya ‘alalfallah ” asema: “Lahaula walaa Quwwata illa billah ”. Kisha akisema: “Allahu Akbaru, allaahu Akbaar, aitikie: “Allaahu akbar Allahu Akbaar”. Kisha anaposema: “Laaillaha illaallah ”, aitikie: “Laaillaaha illaallah ”, akifanya hivyo kwa unyenyekevu na mazingatio ataingia Peponi. (Muslim).

 


Dua baada ya Adhana

 


Baada ya adhana kwisha Muislamu anatakiwa amswalie Mtume (s.a.w) kisha aombe dua. Kutokana na hadithi iliyosimuliwa na “Abdullah ibn, Umar (Mtume (s.a.w)) alisema kuwa:-

 


Ukisikia adhana rudia kama asemavyo muadhini, kisha niswalie mimi mara moja Allah humuongezea rehema (humswalia yeye) mara kumi. Kisha niom bee sehemu ya wasillah. Hii ni sehemu huko Peponi iliyohifadhiwa kwa ajili ya mmoja katika waja wa Allah: nategemea huenda nikawa mimi, na yeyote atakayeniombea Allah anipe afya hiyo ya wasilah basi uombezi wangu utaruhusiwa kwake (siku ya Kiyama). (Muslim).

 


Allaahuma rabba haadhihid-daawatit-taamma. Wasswalaatil-qaaimah. Ati Muhammadal-wasiilata walfadhiilat Wab-’ath-hu
maqaaman mahmuudanil-ladhii wa’ad-tahu.Innaka laa tukhliful miiaad.

 


Tafsiri:

 


“Ewe Allah, Mola wa mlingano huu uliokamilika na swala iliyosimama,Mpe Muhammad (s.a.w) daraja kubwa na enzi na mpe hicho cheo ulichomuahidi, Hakika yako wewe si mwenye kuvunja miadi”. (Bukh ari).

 


Ni vyema kipindi kati ya adhana na Iqama kiwe kirefu kidogo, kiasi cha kumuwezesha mtu kujitayarisha na kuwahi swala ya jamaa. Hivyo, hapana budi pawe na kipindi cha kuwangojea watu. Kipindi hiki ni kiasi cha kuswali rakaa mbili.

 


Ames imulia Abdullah bin Mughaffal al-Muzani (r.a): “Kuna swala (sunnah) kati ya Adhana mbili (adhana na iqama) na kaongeza: kwa mtu anayetaka kuswali”.
Pia katika hadithi tunafahamishwa kuwa kipindi kati ya adhana na Iqama ni wakati mzuri wakuomba dua. Anas bin Malik (r.a) amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) amesema:-
Hairudishwi (haikataliwi) dua, baina ya Adhana na Iqama. (Abu Daud, An-Nisani, tirmidh).

 


Iqama

 


Ni wito au amri yakusimama tayari kuanza swala. Utakuta maneno ya Iqamat ni yale yale ya Adhana lakini hutamkwa nusu yake tu isipokuwa neno la mwisho (Laailaaha illa-llahu) ambalo huwa hutamkwa mara moja kuongezea maneno:
Qad qaamat sw-swalat - qad-qaamat sw-swalat (Sw ala ipo tayari).

 

Haya husemwa baada ya maneno (Njooni katika kheri). Ndivyo tunavyofahamishwa katika Hadithi ifuatayo:
Ibn Umar (r.a) amesimulia kuwa palikuwa na adhana wakati wa Mtume (s.a.w) kila tamko mara mbili na Iqamat mara moja isipokuwa aliongezea kusema: Swala iko tayari. Swala iko tayari. (Abuu Daud, Nisai).
Swala ya Sunnah baada ya Iqamat

 


Ikisha kimiwa kwa ajili ya swala ya jamaa, hairuhusiwi kuendelea na swala ya sunnah kama tunavyojifunza kutokana na hadith ifuatayo:
“Abu Hurairah ameeleza kuwa Mtume (s.a.w) amesema: Swala ya faradh ikianza,hapana swala nyingine (kuswaliwa ” Na katika riwaya nyingine Mtume (s.a.w) amesema: Sw ala ni ile ambayo imetolewa Iqama ”. (Ahmad, Abu Daud, At-tirmidh, an-Nisai na Ibn Majah).Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/08/14/Sunday - 01:19:02 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1134


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Swala ya jamaa na taratibu zake
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu swala ya jamaa na taratibu zake. Soma Zaidi...

Jinsi ya kuelekea qibla katika swala.
Je unadhani ni kwa nini waislamu wanaelekea kibla, na jinsi gani utaweza kukipata kibla. Soma Zaidi...

Lengo la kusimamisha swala kwa mwanadamu
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu lengo la kusimamisha swala. Soma Zaidi...

Swala ya idil fitir na idil haji nanjinsi ya kuziswali
Hapa utajifunza jinsi ya kuswali swala ya idil haji na swala ya idil fitir Soma Zaidi...

Swala ya tarawehe jinsi ya kuiswali
Post hii itakwenda kukufundisha kuhusi swala ya tarawehe, faida zake na jinsi ya kuiswali. Soma Zaidi...

Al-Arbauwn An-Nawawiyyah hadithi ya 2: Ujio wa Jibril kwa Mtume (s.a.w)
Hii ni hadithi ya pili katika kitabu cha Arbain Nawawiy Soma Zaidi...

Zijuwe nguzo 17 za swala.
Ili swala itimie utahitajika kutimiza nguzo zake na masharti yake. Hapa utajifunza nguzo 17 za swala. Soma Zaidi...

Ni nini maana ya swala
Post hii inakwenda kukugundisha kuhusu maana halisi ya ibada ya swala. Soma Zaidi...

Swala ya kuomba mvua swalat istiqaa na jinsi ya kuiswali.
Hapa nitakujulisha kuhusu swala ya kuomba mvia, na taratibu za kuiswali. Soma Zaidi...

Namna ya kuswali hatuwa kwa hatuwq
Post hii itakufundisha jinsi ya kuswali hatuwa kwa hatuwa. Soma Zaidi...

Ijuwe swala ya Tawbah na jinsi ya kuiswali
Post hii itakufundisha kuhusu swala ya sinnah ya tawba. Soma Zaidi...

Jinsi ya kiswali swala ya haja
Post hii itakufundisha kuhusu swala ya haja na jisi ya kuiswali. Soma Zaidi...