Historia ya bi Khadija na familia yake na chanzo cha utajiri wake.

Sira na historia ya Mtume Muhammad s.a.w, sehemu ya 17. Historia ya Bi Khadija na familia yake.

HISTORIA YA BI KHADIJA
Bi Khadija jinalake halisi ni Khadija bint Khuwald bin Asab baba yake alikuwa ni mfanya biashara. Baadhi ya historia zinataja kuwa alifariki wakati wa vita vya Alfijar mwaka 585 BK, tumetaja muhusu vita hivi kurasa za hapo juu. Nasaba yake pia inakutana na nasaba ya Mtume Muhammad kwa upande wa bab yake na baba yake. Mama yake aliitwa Fatima Bint Za’idah na alikuwa katika kabila la maqurayshi, kabila la Mtume Muhammad (s.a.w). mama yake Khadija alifariki mwaka 575 KK. Khadija aliolewa na Muhammad mwaka 595.



Bi Khadija alishapata kuolewa na wanaume wawili kabla hata ya kuolewa na Muhammad na lishazaa watoto. Khadija alikuwa na katika wafanyabiashara wa Makkah wakubwa sana wakati huo. Historia inaonesha kuwa wakati waarabu wa kikurayshi walipokuwa wakikusanya bishaa zao ili kwenda kuziuza maeneo ya Syria na Yemen, msafara wa Khadija ulikuwa ni sawa misafara ya maquraysh wote ikusanywe pamoja. Hii inaonesha alikuwa ni tajiri zaidi wakati huo.



Tofauti na biashara Hadija alifahamika kuwa ni katika wanawake wazuri na wenye akili zaidi kuliko wanawake wote wa Makkah wakati huo. Watu wenye vyeo vyao na utajiri walikuwa wakienda kutoa posa lakini walikuwa wakirudi patupu. Hadija alikuwa ni katika wanawake waliokuwa wakiheshimika sana. Alikuwa ni mkarimu na mwenye kusaidia sana masikini na wasio na kitu. Na aliendeleza tabia hii hata baada ya kuolewa na Muhammad.



Hadija alipewa majina mbalimbali kutokana na cheo chake mbele za watu wa Makkah. Waarabu walimuita Ameerat-Quraysh (princess of quraysh) pia walimuita Khadija al-Kubra (Khadija the great). ijapokuwa Makkah wakati huo watu walikuwa wakiabudu masanamu lakini Khadija katu hajapatapo kusujudia masanamu.



Ijapokuwa Khadija alikuwa ni mfanyabiashara mkubwa lakini hajapatapo kusafiri na biashara zake ili kwenda kuuza. Alikuwa akiajiri wanaume waendde kumfanyia biashara na anawalipa kwa makubaliano maalumu. Mwaka 595 Khadija alihitaji mtu wa kwenda kumfanyia biashara zake maeneo ya Syria. Kwa kuwa alipatapo kusikia sifa za Muhammad kuwa ni Mwaminifu na ni mkweli hivyo akamtafuta na wakakubaliana kuwa atamlipa zaidi kuliko ambavyo anawalipa watu wengine.



Nafisa alikuwa ni rafiki wa karibu sana wa Khadija, hata wakati Khadija alipotaka kuolewa na Muhammad alimtumia nafisa ili aende kuzungumzana Muhammad kuhusu jambo hili. Tumeshazungumza khabari hii hapo kurasa za nyuma. Mjomba wake Khadija alifahamika kwa jina la Waraqa bin Nawfal. Huyu alikuwa ni mkristo na ni mchamungu na alitambua vyema ujio wa Mtume wa Mwisho. Hata wakati watu wote wa Makkah hawakujuwa kuwa Muhammad atakujakuwa Mtume Waraqa alishatambua jambo hili. Waraqa ndiye aliyesimamia ndoa ya Khadija na Muhammad. Dada yake alifahamika kwa jina la Hala bint Khuwayld.



Bi Khadija anajulikana kwa kuwa ndiye Mtu wa kwanza kutamka shahada ya kuamini utume wa Mtume Muhammad s.a.w. Khadija alitumia mali zake katika kuendeleza harakati za dini mpaka alipofariki mwaka wa 10 baada ya utume (yaani Miladiya) ni sawa na 620 katika mji wa Makkah. Khadija alifariki akiwa na umri wa miaka 65. na alizikwa sehemu iitwayo jannat al-Mu’allah mjini Makkah. Bi kahdija alishapataga kuolewa na ‘Atiq bin ‘Aidh Al-Makhzum na Abu Hala Malak ibn Nabash. Na alizaaa pamoja na waume wote hao watoto. Alizaa na Mtume Muhammad (s.a.w) watoto sita.

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021/11/30/Tuesday - 08:46:06 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 4255

Post zifazofanana:-

Sababu za kumsafisha mgonjwa kinywa
Posti hii inahusu zaidi sababu za kumsafisha mgonjwa kinywa, Mgonjwa akiwa anaumwa na pia anakula chakula ni lazima asafishwe kinywa Ili kuweza kuepuka madhara mengine yanayoweza kujitokeza kwa sababu ya kuwepo kwa uchafu kinywani. Soma Zaidi...

Faida za kula magimbi (taro roots)
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula magimbi Soma Zaidi...

Dalili za ukimwi, unavyoenezwa na njia za kujikinga
Ukimwi ni upungufu wa kinga mwilini.unasababishwa na virusi ambavyo hutokea kwa mtu mwingine kwa njia mbalimbali Soma Zaidi...

Yafahamu magonjwa ya kurithi na dalili zake pia na jinsi ya kujikinga nayo
Posti hii inahusu zaidi magonjwa ya kurithi ambayo hubebwa na vinasaba vya urithi kutoka kizazi kimoja kwenda kingine.magonjwa haya hata hivyo ,si kila kasoro huwa ni ugonjwa kwa mtu mfano ,ualbino na kitoweza kutofautisha rangi kama vile nyekundu na kija Soma Zaidi...

Dalili za Utasa wa wanaume
Posti hii inazungumzia kuhusiana na Utasa wa Mwanaume hutokana na uzalishaji mdogo wa mbegu za kiume, utendakazi usio wa kawaida wa manii au kuziba kwa manii ambayo huzuia utoaji wa mbegu za kiume. Magonjwa, majeraha, matatizo ya kiafya sugu, u Soma Zaidi...

Upungufu wa vyakula vya madini
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu madhara ya upungufu wa vyakula vya madini Soma Zaidi...

Mfumo wa ulinzi na usalama katika fola ya uislamu madinah
Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Nguzo za kufunga ramadhani
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Ugonjwa wa Saratani ya ini.
Saratani ya ini'ni'Saratani'inayoanzia kwenye seli za ini lako. Soma Zaidi...

Madhara ya mafuta mengi mwilimi
Post hii itakufundisha madhara ya kuwa na mafuta mengi mwilimi Soma Zaidi...

Faida za kunywa maziwa
Somo hili linakwenda kukuletea faida za kunywa maziwa kiafya Soma Zaidi...

Huduma ya Kwanza kwa aliyeungua
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa aliyeungua Soma Zaidi...