Mtume Yusufu(a.
Mtume Yusufu(a.s) alikuwa mtoto wa Mtume Ya’aquub bin Is- haq bin Ibrahiim. Kwa hiyo Yusufu(a.s) ni kijukuu cha (mjukuu wa mtoto wa) Mtume Ibrahiim(a.s) na mjukuu wa Mtume Is-haqa(a.s.).
Mtume Ya’aquub(a.s) alikuwa na watoto 12. Nabii Yusufu(a.s) alichangia mama na mmoja wa hao. Wengine 10 walikuwa na mama zao.
Ndoto ya Nabii Yusufu(a.s) Maisha ya Nabii Yusufu(a.s) yanaanza kusimuliwa ndani ya Qur’an pale alipomwambia babake kuwa:
Yusufu alipomwambia baba yake “Ewe babaangu! hakika nimeona katika ndoto nyota kumi na moja na jua na mwezi. Nimeviona hivi vikinisujudia(12:4)
Mtume Ya‘aquub, kwa ilimu aliyopewa na Mola wake alifahamu tafsiri ya ndoto ile kwamba inabashiri kuwa Yusufu atakuja kuwa mtu mwenye hadhi kubwa na Mtume. Akamtahadharisha kuwa:
Akasema (baba yake): “Ewe mwanangu! Usiwasimulie ndoto yako (hii) nduguzo wasije wakakufanyia vitimbi (kwa ajili ya husuda). Hakika Shetani kwa mwanadamu ni adui aliye dhahiri.(12:5)
Namna hivi Mola wako atakuchagua na kukufundisha hakika ya mambo. Na atatimiza neema zake juu yako na juu ya kizazi cha Ya‘aquub, kama alivyoitimiza zamani juu ya baba zako Ibrahim na Is-haqa. Bila shaka Mola wako ni Mjuzi na Mwenye hikima: (12:6).
Umeionaje Makala hii.. ?
Sira na historia ya Mtume Muhammad s.a.w, sehemu ya 17. Historia ya Bi Khadija na familia yake.
Soma Zaidi...Luqman ni katika watu wema kabisa waliopita zama za nyuma.
Soma Zaidi...(i) Suratul- ‘Alaq (96:1-5)“Soma kwa jina la Mola wako aliyeumba Aliyemuumba mwanaadamu kwa ‘alaq.
Soma Zaidi...Sahaba wa kwanz akufariki akiwa shahidi, alifariki kwa sababu ya mateso aliyoyapata kutoka kwa Makafiri wa ki Quraysh
Soma Zaidi...Mtume aliyemfuatia Nabii Idrisa(a.
Soma Zaidi...Kutokana na Historia ya Nabii Musa na Harun(a.
Soma Zaidi...