image

Hizi ndio nyakati za swala tano na jinsi ya kuchunga nyakati za swala.

Posti hii inakwenda kukufundisha kuhusu jinsi yavkuchunga nyakatibza swala tano.

3. Kuchunga wakati

“... Kwa hakika swala kwa waumini ni faradhi iliyowekewa nyakati makhususi” (4:103).
Swala tano zilizofaradhishwa kwa Umma huu wa Mtume Muhammad (s.a.w) ni:- Adhuhuri, Alasiri. Magharibi, Ishai na Alfajiri. Wakati wa kuswali kila swala unabainishwa katika hadith ifuatayo:

 


“Abdullah Ibn ‘Amir amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema, Wakati w a sw ala ya adhuhuri ni kuanzia jua linapopinduka hadi kivuli cha mtu kin apokuwa sawa na kimo (urefu) chake. Na unamalizika kwa kuingia

 

Alasiri. Na muda wa swala ya Alasiri (ni kuanzia inapomalizika Adhuhuri) hadi jua linapopiga umanjano. Muda wa swala Magharibi (ni mara baada ya kuzama jua na) utabakia mpaka wingu jekundu litow eke. Muda wa swala ya Isha (ni baada ya kutoka Mgharibi) na kubakia hadi katikati ya usiku. Na wakati wa swala ya Alfajiri unaanza kwa kudhihirika kwa ukanda mweupe mpaka kabla ya kuchomoza jua. Jua linapochomoza jizuilie kusw ali kw ani huchomoza kati ya pembe za shetani. (Muslim)
Kutokana na hadithi hii, nyakati za swala tano ni:

 


Adhuhuri: Inayopasa kuswaliwa mara tu jua linapogeuka kuelekea Magharibi mpaka kuingia swala ya al’asiri.

 


Al’asiri: Huanza pale urefu wa kivuli unapokuwa sawa na kitu chenyewe mpaka kivuli kinapokuwa mara dufu ya urefu wa kitu ch en yewe.

 


Magharibi: Huanza mara tu jua linapozama na kuingia pale mawingu mekundu yanapobadilika kuwa ya kimanjano wakati inapoingia swala ya Isha.

 


Isha: Kuanzia mara tu yanapobadilika mawingu kuwa ya kimanjano mpaka usiku wa manane.

 


Alfajir: Huingia kwa kutokea alama ya mstari mweupe unaotokea Mashariki ambao ni alama ya kwisha kwa usiku na kuanza kwa mchana. Kuingia kwa Alfajiri kwa alama hii ya uzi mweupe ndio mwisho wa kula daku kwa mwenye kufunga kama isemavyo Qur-an:

 

“... Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa Alfajiri katika weusi wa usiku ...” (2:187)
Hizi ndizo swala tano na nyakati zake kama alivyotufundisha Mtume (s.a.w) ambazo hutegemea uchunguzi wa mwendo wa jua katika saa ishirini na nne za siku.

 

Utaalamu wa karne hii umerahisisha kuzijua nyakati za mwanzo na mwisho wa kila, swala kwa kutengeneza ratiba ya nyakati za swala kwa kutumia takwimu za mwendo wa jua katika nyakati zilizonukuliwa kwa muda mrefu na wachunguzi wa hali ya hewa.


Kuswali swala katika wakati wa mwanzo ni bora zaidi kama tunavyojifunza katika hadith ifuatayo:-
“Ummi Farawata(r.a) amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) aliulizwa, ni kitendo gani kilicho bora kuliko vyote? Akajibu: “Swala wakati wake wa mwanzo”.(Ahmad, tirm idh, Abu Daud).

 


Swala hukubaliwa kwa Kuwahi rakaa moja ndani ya wakati

 


Iwapo Muislamu kwa dharura atachelewa kuiswali swala ya faradh kiasi cha kupata rakaa moja tu ndani ya wakati,swala yake itakubaliwa kwa mujibu wa Hadith ifuatayo:


Abu Hurairah(r.a) ameeleza kuwa Mtume (s.a.w) amesema: “Mwenye kupata rakaa moja ya swala ameipata swala ”.(Maimamu sahihi sita tu).
Si vizuri kabisa kwa Muislamu, kwa makusudi kuchelewesha swala kiasi hicho.

 


Nyakati zilizoharamishwa kuswali

Kwa mujibu wa Hadith mbali mbali kuna nyakati tano zilizoharamishwa kuswali na Mtume (s.a.w):-
1. Kuswali sunnah baada ya swala ya Alfajiri mpaka jua litakapochom oza.


2. Wakati wa kuchomoza jua mpaka litakapopanda juu kabisa kiasi cha urefu wa mkuki.


3. Jua linapokuwa katikati wakati wa mchana mpaka litakaposogea kidogo upande wa Magharibi.


4. Kuswali sunnah baada ya swala ya alasiri mpaka jua litakapozama kabisa.
5. Wakati wa kuzama jua.

 





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2306


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Mazao ambayo inapasa kutolewa zaka
Soma Zaidi...

Namna ya kumvalisha sanda maiti, na kushona sanda ya maiti
Soma Zaidi...

Ni mali ipi inatakiwa kutolewa zaka?
Soma Zaidi...

HUKUMU YA KUUWA MTU (KUMWAGA DAMU) KWENYE UISLAMU
عَنْ ابْنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه و سلم "لَا يَحِلُّ دَمُ امْرِئٍ مُسْلِمٍ [ يشهد أن ل?... Soma Zaidi...

Jinsi ya kuswali swala ya kuoatwa kwa juwa ama swala ya kuoatwa kwa mwezi.
Post hii itakufundisha kuhusu swala ya kupatwa yaani kupatwa kwa juwa na kupatwa kwa mwezi swalat kusuf na swalat khusuf Soma Zaidi...

Jinsi uislamu ulivyokomesha biashara ya utumwa wakati na baada ya mtume Muhammad (s.a.w)
Soma Zaidi...

Kusimamisha swala za Sunnah
Nguzo za uislamu, kusimamisha swala za Sunnah (EDK form 2: Dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Maana ya Swaumu na Lengo la kufunga
Soma Zaidi...

Haki na Wajibu wa mume kwa mkewe na familia
Soma Zaidi...

Msisitizo juu ya kutoa zaka na sadaka
Soma Zaidi...

Kufunga Mwezi wa ramadhani kisheria
Soma Zaidi...

Jinsi ya kushona sanda ya maiti na kumvisha yaani kumkafini
Hapa utajifunza taratibu za kumkafini maiti wa kiislamu. Yaani kushona sanda yake na kumvisha. Soma Zaidi...