Menu



Huduma kwa mama mwenye kifafa cha mimba.

Posti hii inahusu zaidi huduma ambazo wajawazito wanaweza kuzipata wakiwa na Dalli au tayari wana kifafa cha mimba.

Huduma kwa wanawake wenye kifafa cha mimba.

1. Kwanza kabisa Mama anapaswa kuhakikisha anahudhuria mahudhurio ya mara kwa mara ili kupima kiwango cha presha na pia kuangalia kiwango cha protini kwenye mkojo na pia kuzingatia mda wa kujifungua na ajitahidi kujifungulia hospitalini ili kuweza kuwa na uhakika wa huduma wakati wa kujifungua, akijifungua mitaani anaweza kupatwa na matatizo ambayo wahudumu wa pale wanaweza kushindwa kuyafanyia kazi na kulingana na tatizo.

 

2. Pia Mama anapaswa kupata mda wa kutosha kupumzika, pia huduma zota anapaswa kuzipata akiwa kitandani kwa hiyo akikaribia kujifungua aepukane na kutembea huku na huko bila sababu ya msingi na pia anapaswa kufundishwa jinsi ya kulala kwenye kitandani ili kuhakikisha kubwa damu inatembelea kwenye mfuko wa uzazi kwa kiwango cha kutosha pia kuhakikisha kubwa na miguu kama imevimba inatoka na kuwa kwenye hali ya kawaida.

 

3. Vile vile mkojo wa Mama unapaswa kuangaliwa kila mara ili kuweza kutambua kama kiwango cha protini kwenye mkojo kimepungua au kinaendelea kuongezeka na kuweza kutoa huduma za msingi ili kupunguza kiwango cha protini kwenye mkojo.

 

4. Kwa mama mjamzito kiwango cha vimiminika vinavyoingia na kutoka vinapaswa kupimwa, ikionekana kwamba  kiwango cha kimiminika kinachotoka ni kikubwa tunajua wazi figo linafanya kazi vizuri ila kama ni kidogo tunajua wazi kubwa kuna tatizo kwenye figo.

 

5. Kupima mara kwa mara kiasi cha presha kwa sababu ili kuweza kutambua kuwa kiwango kinaongezeka au kina pungua kupima mara nne kwa saa.

 

6. Kuendelea kuangalia tumbo mara kwa mara walau mara mbili kwa siku moja ili kuweza kuangalia kama kuna maumivu kwenye tumbo au kitu chochote kisicho cha kawaida.

 

7. Kuangalia mara kwa mara mapigo ya mtoto kama yapo sawa kwa sababu tatizo hili kama halijaangaliwa vizuri usababisha matatizo makubwa kwa mtoto

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea

Ndio     Hapana     Save post
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Uzazi Main: Post File: Download PDF Views 1568

Share On:

Facebook WhatsApp

Post zinazofanana:

Nguzo kuu za umama katika umri wa kupata watoto na kulea watoto

Posti hii inahusu zaidi nguzo kuu za umama katika umri wa kujifungua na kulea watoto, ni kipindi ambacho mama anakuwa analea watoto kwa kawaida kadri ya makadirio kipindi hiki uanza kati ya miaka kumi na mitano mpaka arobaini kwa walio wengi na kinaweza k

Soma Zaidi...
Fahamu siku za kubeba mimba na zisizo za kubeba mimba.

Posti hii inahusu zaidi siku za kubeba mimba na zisizo za kubeba mimba , tunapaswa kujua hivi Ili kuweza kupanga uzazi na kuepuka njia ambazo ni hatarishi kwa afya zetu.

Soma Zaidi...
Dalili za mimba kuanzia week mbili Hadi mwezi

Somo hili linakwenda kukueleza baadhi ya dalili za mimba kuanzia week mbili Hadi mwezi

Soma Zaidi...
Chanzo cha tatizo la mvurugiko wa hedhi.

Posti hii inahusu zaidi chanzo cha mvurugiko wa hedhi, Kuna kipindi hedhi uvurugika kabisa, pengine unaweza kupata hedhi mara mbili kwa mwezi au kukosa au pengine siku kuwa zaidi ya tano mpaka Saba au kuwa chache, hali hii utokea kwa sababu mbalimbali tut

Soma Zaidi...
Zijue sababu za kutobeba mimba

Posti hii inahusu zaidi sababu mbalimbali ambazo zinamfanya mama au dada kutobeba mimba. Kwa hiyo tutaziona hapo chini kama ifuatavyo.

Soma Zaidi...
Mimba iliyotungia nje, sababu zake na dalili zake. Nini kifanyike kuizuia?

Mimba hatari iliyotungia nje ya mji wa mimba, ni zipi dalili zake na ni kivipo mimba inatungia nje?

Soma Zaidi...
Tatizo la kutanuka kwa tezi dume.

Posti hii inahusu zaidi tatizo la kutanuka kwa tezi dume, ni tatizo ambalo linawakumba wanaume wengi kwa wakati huu kwa sababu ya kuwepo kwa maaambukizi kwenye tezi ambayo Usababishwa na vitu mbalimbali kama tulivyoona.

Soma Zaidi...
Changamoto za ujauzito

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu changamoto za ujauzito na dalili zake endelevu

Soma Zaidi...
Zijue Dalili za hatari kwa Mama mjamzito

Posti hii inahusu zaidi dalili za hatari kwa Mama mjamzito, ni Dalili ambazo ujitokeza kwa Mama mjamzito, hizi Dalili zisipofanyiwa kazi mapema zinaweza kuleta shida kwa Mama kwa hiyo jamii nzima inapaswa kujua Dalili hizi na kuchukua hatua endapo zitajio

Soma Zaidi...
mambo HATARI KWA UJAUZITO (MIMBA) mambo yanayopelekea kujauzito kuwa hatarini kutoka

Tofauti na mambo matano yaliyotajwa hapo juu kuwa yanapelekea ujauzito kutoka, kuna mambo mengine ambayo yanaweza kuuweka ujauzito kuwa hatarini.

Soma Zaidi...