Huduma kwa mama mwenye mimba Inayotishia kutoka.

Post hii inahusu zaidi huduma ambayo Mama anapaswa kutolewa pindi mimba inapotishia kutoka huduma hii utolewa kulingana na Dalili tulizoziona zinazohusiana na mimba kutishia kutoka.

Huduma kwa mama mwenye dalili za mimba Inayotishia kutoka .

1. Kwanza kabisa tunapaswa kujikumbushia kidogo kuhusu mimba Inayotishia kutoka , mimba ya aina hii utokea pale ambapo mjamzito utokwa na damu kidogo kidogo zinaweza kuwa kama za hedhi ila zinaweza kuwa kidogo lakini ni za mwendelezo au za mara kwa mara na hazikati na pengine Mama anakuwa Hana maumivu hata kidogo au pengine maumivu yanakuwepo ila ni kwa kiasi kidogo sana kwa hiyo mama baada ya kuona hayo anapaswa kuwahi hospital Ili kupata matibabu na kuokoa mimba isitoke. Kwa mjamzito wa namna hii tunapaswa kumpatia huduma zifuatazo.

 

 

 

 

2. Kwa kwaida Mama akiwa katika hali hii mara nyingi huwa na wasiwasi kwa hiyo anapaswa kutiwa moyo na kumhakikishia usalama na kumwambia ni shida gani iliyompata pia mama anapaswa kulala kitandani kwa wiki Moja bila kutembea huko na huku bila sababu , mjamzito anashauliwa kulala kwa Sababu kama Kuna sehemu yoyote imeachia ni rahisi kabisa kujirudia na kuwa kawaida kabisa na pia mjamzito kama amefuata mashariti haya kitu cha kwanza kabisa damu ambazo zilikuwa zinatoka zinakoma na kama mjamzito amefuata mashariti anakuwa vizuri ndani ya wiki Moja ,na pia mama kama ameambiwa kulala anapaswa kuelezwa wazi kwa nini amelala na pia aambiwe wazi kwamba akikosea mashariti anaweza kupoteza mtoto.

 

 

 

 

3. Pia Mama anapaswa kushauliwa au kuambiwa kabisa kuachana na tendo la ndoa anapopatwa na tatizo la namna hii,

Mama anapaswa kuachana na tendo la ndoa kwa sababu inawezekana kwenye sehemu ya mlango wa kizazi Kuna sehemu iliyolegea kwa hiyo mama akiendelea kufanya tendo la ndoa anasababisha sehemu Ile kulegea na kuendelea kuleta matatizo zaidi au kwa wakati mwingine baba akitoa mbegu na mbegu hizo mara nyingi Zina kichocheo ambacho kikichanganyika na kichocheo cha uchungu cha mama uweza kuanzisha uchungu na kusababisha mlango wa kizazi kufunguka na mtoto anaweza kutoka, kwa hiyo Mama mwenye tatizo hili anapaswa kuacha tendo la ndoa mpaka hapo atakapomaliza kujifungua. Pia na baba anapaswa kuelezwa wazi hali ya mke wake.

 

 

 

 

 

4. Pia kwa Kipindi hiki kwa sababu mama anaweza kuwa na mawazo au kwa sababu ya kulala kwa mda mrefu anaweza kukosa usingizi na kuwa na kishawishi cha kutembea akiwa amejificha na kusababisha madhara zaidi kwa hiyo ni vizuri mjamzito akionekana na wasiwasi na kutotulia apewe dawa za usingizi, na pia pengine mimba inawezekana kutishia kutoka kwa sababu ya kukosekana kwa baadhi ya vichocheo ambavyo usaidia kukua kwa mimba kwa hiyo mama anapaswa kupewa vichocheo mbalimbali,kwa kitaamu huiitwa progesterone hasa hasa kama Kuna ushaidi kwamba imepungua kwenye mwili wa mama 

 

 

 

 

 

5. Ikitokea damu ikaacha kutoka hiyo ni dalili kubwa ya kwamba tatizo limepona na mama anaweza kuruhusiwa kwenda nyumbani lakina kwamashariti makubwa kati ya mtoa huduma za afya, mama na ndugu wa karibu hasa mme wake , kwa hiyo mama atapaswa kurudi klinic mara kwa mara Ili kuendelea kuangalia afya ya mama na mtoto, na kabla mama hajaondoka anapaswa kabisa kuangalia kama damu imeacha kutoka na watoa huduma wajihajikishie kwa sababu Kuna akina Mama ambao wamechoka kuishi hospital, na akina Mama wanapaswa kuwa wakweli na wawazi kuhusu afya zao na za watoto pia.

 

 

 

 

 

 

6. Pia tatizo likipona ni vizuri kutoa elimu ya kutosha kwa mama na ndugu Ili kuepuka Mila potofu ambazo zinaweza kuleta matatizo zaidi

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/11/12/Saturday - 03:45:19 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 4747

Post zifazofanana:-

ujuwe ugonjwa wa gout na athari zake mwilini
Post hii itakwenda kuzungumzia ugonjwa wa gout unaosababishwa na ongezeko la asidi mwilini. Soma Zaidi...

Huduma ya Kwanza kwa mtu aliyepatwa na shambulio la moyo
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyepatwa na shambulio la moyo Soma Zaidi...

Namna ya kutunza nywele za mgonjwa
Posti hii inahusu zaidi namna ya kutunza nywele za mgonjwa hasa kwa wagonjwa mahututi na wale wasiojiweza tunafanya hivyo ili tuweze kuwatoa kwenye hali ya usafi. Soma Zaidi...

Faida za kiafya za stafeli/soursop
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za stafeli ama soursop Soma Zaidi...

Njia za kuzuia Ugonjwa wa tauni.
Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali ambazo zinaweza kutumika ili kuweza kuepuka Ugonjwa wa raundi. Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kitunguu maji
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kitunguu maji Soma Zaidi...

Je utambuzi wa maambukizi ya ukimwi hupatikana mda gani pale mtu anapoambukizwa
Kuna ukimwi na HIV na kila kimoja kina dalili zake na muda wa kuonyesha hizo dalili. Soma Zaidi...

Msaada kwa wenye tonsils
Posti hii inahusu zaidi msaada kwa wenye tonsils, kwa wale wenye tonsils wanapaswa kufanya yafuatayo ili kuweza kupambana na ugonjwa huu. Soma Zaidi...

je maambukizi ya virus vya ukimwi yataonekana kwenye kupimo baada ya siku ngap??
Ni muda gani nitaanza kuona dalili za HIV na kilimo kitaonyesha kuwa nimeathirika? Soma Zaidi...

Ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo
Posti hii inahusu zaidi Ugonjwa wa uti wa mgongo, ni ugonjwa unaoshambulia sehemu inayofunika ubongo na pia sehemu ya spinal cord Soma Zaidi...

Aladini katika pango la utajiri
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

Mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili
Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili, hapa tunaona Jackie anajibu barua ya Julius kwa kusema yafuatayo. Soma Zaidi...