Huduma kwa mtoto mwenye Maambukizi kwenye mifupa
Posti hii inahusu zaidi msaada kwa mtoto mwenye Maambukizi kwenye mifupa, ni huduma anayopewa mtoto mwenye Maambukizi kwenye mifupa.
Huduma kwa mtoto mwenye Maambukizi kwenye mifupa.
1. Kwanza mtoto akigunduliwa kubwa na tatizo la Maambukizi kwenye mifupa anapaswa kupewa antibiotics ambayo inatibu ugonjwa huu ni vizuri mtoto kupewa antibiotics kwenye mfumo wa maji yaani drip kwa kufanya hivyo bakteria wanaosababisha Maambukizi wanaweza kupunguza au kuondolewa.
2. Jaribu kumweka mtoto kwenye mkao mzuri zaidi ili kuweza kupunguza kiwango cha maumivu, kwa sababu ya Maambukizi kuna sehemu ambazo zinakuwa na maumivu kupita sehemu nyingine kwa hiyo sehemu hizo zinabidi kugundulika na kuepuka kukaliwa au kukaliwa, kwa hiyo mtoto anapaswa kuwekwa kwenye sehemu nzuri.
3. Kwa kuwa mtoto anakuwa kwenye drip na anakuwa na maumivu kwa hiyo anapaswa kupimwa joto la mwili, msukumo wa damu, mapigo ya moyo ili kuona kama kuna mabadiliko, kama joto la mwili liko juu mtoto anapaswa kushushwa joto la mwili kwa kutumia baadhi ya Dawa na maumivu kama vile paracetamol ili kuepuka matatizo mengine ambayo usababishwa na joto la mwili kuwa juu kama vile degedege na kupungukiwa kwa damu.
4, Hakikisha kama kuna kidonda kidonda kwenye mfupa kilichotokana na Maambukizi kimesafishwa kwa kufanya hivyo tunaweza kupunguza maumivu na kuongeza kiwango cha kupona haraka na pia vitu vyote vya kusafishia kidonda vinapaswa kuwepo ili kukifanya kipone haraka.
5. Kwa mtoto hakikisha unaangalia kiasi cha kilichoingia na kiasi kilichotoka, kwa kuangalia kiasi kilichoingia angalia maji anayokunywa, chai au uji na vitu vyote vya aina ya kumiminika vilivyoungia mwilini na pia anapaswa kuangalia kiasi kilichotoka kwa kuangalia mkojo uliotolewa na jasho kama limetoka tunafanya hivi ili kuzuia kuishiwa kwa maji mwilini.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 kitabu cha Simulizi π2 ai web app π3 Kitabu cha Afya π4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina π5 Kitau cha Fiqh π6 Bongolite - Game zone - Play free game
Post zinazofanana:
Kuhusu HIV na UKIMWI
Somk hili linakwenda kukueleza kuhusu Mambo mbalimbali yahusuyo HIV na UKIMWI
Soma Zaidi...Homa ya manjano, dalili za homa ya manjano na namna ya kujikinga na homa ya manjano
HOMA YA MANJANO (yellow fever)Homa ya manjano ni maradhi yanayosababishwa na virusi na husambazwa na mbu.
Soma Zaidi...Sababu za Kuvimba kwa kope.
Post hii inazungumzia kuhusiana na Sababu zinazopelekea kuvimba kwa kope, kawaida huhusisha sehemu ya kope ambapo kope hukua na kuathiri kope zote mbili. Pia hutokea wakati tezi ndogo za mafuta ziko karibu na msingi wa kope huziba. Hii inasababisha kuw
Soma Zaidi...Maisha ya ndoa na afya ya uzazi baada ya kujifungua.
βKipindi cha baada ya kujifungua (postpartum period) ni awamu ya mabadiliko makubwa ya kimwili, kihisia, na kijamii kwa familia. Makala hii inachunguza kwa kina changamoto za kiafya ya uzazi, marejesho ya mahusiano ya ndoa, na mikakati ya kuboresha mawasiliano na afya ya akili. Lengo ni kuwapa wanandoa elimu ya kisayansi itakayowasaidia kuvuka kipindi hiki kwa ustawi wa familia nzima.
Soma Zaidi...Dalili kuu 7 za malaria na dawa ya kutibu malaria
Makala hii itazungumzia dalili za Malaria, athari za kuchelewa kutibu malaria, na matibabu ya malaria
Soma Zaidi...