Huduma kwa mwenye maumivu ya tumbo la hedhi

Huduma kwa mwenye maumivu ya tumbo la hedhi

Posti hii inahusu msaada kwa mwenye maumivu ya tumbo la hedhi, hizi ni huduma ambazo utolewa kwa wale wenye maumivu ya tumbo la hedhi.

Huduma kwa mwenye maumivu ya tumbo la hedhi.

1.Kwanza kabisa tunapaswa kumfariji mgonjwa na kumpa pole tukijua kuwa sio yeye pekee yake ambaye amepatwa na ugonjwa huu bali ni tatizo la walio wengi na ni la mda maana utokea kwa siku chache na utoweka na kumhakikishia kuwa akibeba mimba hatapata tena tatizo hili 

 

2. Chukua maji ya moto weka kwenye chupa na weka kwenye tumbo lake na maumivu yatapungua na pengine utoweka kabisa na pengine kama hauna chupa chukua kitambaa chochote na weka kwenye maji ya moto ila sio sana kamua na weka kwenye tumbo hasa hasa sehemu ya maumivu na maumivu yatapungua au yataisha kabisa kwa kufanya hivyo mara kwa mara mgonjwa atapata nafuu.

 

3. Mpatie mgonjwa dawa za kupunguza maumivu kama vile asprin, panadol na dawa hizi zisitumike mara kwa mara zinaweza kusababisha vidonda vya tumbo kwa hiyo wanaovitumia kila mara wawe na tahadhari kubwa kwa sababu matumizi ya mara kwa mara uweza kuleta matatizo makubwa 

 

4. pia mgonjwa anaweza kupatiwa vidonge vya njia za uzazi wa mpango navyo usaidia kupunguza tatizo aina ya vidonge hivi uwa vina homoni ambavyo kwa kitaalamu huitwa combine contraceptive pill, huwa vina homoni zilizochanganywa kwa hiyo msiogope kwamba vina madhara ila upunguza maumivu ya tumbo.

 

5. Kwa sababu maumivu ya tumbo kama tulivyotangulia kusema kwamba uweza kusababishwa na kuwepo kwa uvimbe kwenye via vya uzazi kwa hiyo ikiwa uvimbe huo umeonekana ni vizuri kumwandaa mgonjwa kwa ajili ya upasuaji ili kuweza kuondoa uvimbe huo ambao unaweza kuleta madhara makubwa zaidi.

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Uzazi Main: Post File: Download PDF Views: 2903

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉2 ai web app     👉3 Dua za Mitume na Manabii     👉4 kitabu cha Simulizi     👉5 Kitabu cha Afya     👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    

Post zinazofanana:

Vyanzo vya kuharibika kwa mimba ya miezi kuanzia 0-3

Posti hii inahusu zaidi vyanzo vya kuharibika kwa mimba kuanzia miezi zero mpaka miezi mitatu, kwa sababu hii ni miezi ya kwanza kabisa Kuna sababu au vyanzo vya kuharibika kwa mimba katika kipindi hiki.

Soma Zaidi...
Namna ya kutibu kuharisha kwa mtoto ukiwa nyumbani.

Post hii inahusu zaidi njia za kutibu kuharisha kwa watoto wakiwa nyumbani, kwa sababu mara nyingine mtoto anaweza kuharisha si kwa sababu ya kuwepo kwa Maambukizi ila ni uchafu tu kwa hiyo njia muhimu zinazofaa kutibu mtoto ni pamoja na yafuatayo.

Soma Zaidi...
Fahamu kuhusu mapacha wanaofanana

Post hii inahusu zaidi watoto mapacha wanaofanana,ni watoto wanaozaliwa wakiwa wanaofanana kwa sura na hata group la damu huwa ni Moja.

Soma Zaidi...
Hatari ya kutokwa na damu wakati wa ujauzito

Posti hii inahusu zaidi hatari za kutokwa na damu wakati wa ujauzito, hali hii utokea wakati wa ujauzito ambapo Kuna baadhi ya wajawazito utokwa na damu jambo ambalo hatupaswi kutarajia kwa sababu tunafahamu kabisa mama akishapata ujauzito na damu zinakom

Soma Zaidi...
Namna ya kutunza uke

Posti hii inahusu zaidi namna ya kutunza uke, tunajua wazi kuna magonjwa mbalimbali yanayoweza kutokea iwapo uke hautaweza kutunzwa vizuri na pia uke ukitunzwa vizuri kuna faida ya kuepuka maradhi ya wanawake kwa njia ya kutunza uke.

Soma Zaidi...
Mimba iliyotunga nje

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu mimba iliyotunga nje na madhara yake kiafya

Soma Zaidi...