Huduma kwa walio na matatizo ya asili nyingi mwilini
Posti hii inahusu zaidi huduma kwa wale ambao tayari wameshakuwa na tatizo la asidi mwilini, ni njia ambazo unaweza kuzitumia ili kuweza kupunguza tatizo hili au Mgonjwa anapoendelea kupata matibabu.
Mambo ya kufanya kwa walio na tatizo la asidi mwilini.
1. Daima kula chakula kisichokuwa na ubaridi au na moto mwingi kwa hiyo kiwe cha kati na wakati wa kula chakula daima kula chakula kwa utaratibu na meza chakula kidogo kidogo hasa kwa wale wenye matatizo ya vidonda kooni.
2. Siku zote usitumie chakula kingi baada ya saa kumi na moja jioni na pia usile chakula na kulala mara tu baada ya kula daima subiri kidogo kabla ya kulala na kula vyakulal laini sana na mlo kidogo baada ya saa kumi na moja jioni.
3. Husilale chako baada ya kula,
Kwa kawaida ukimaliza kula Subiri kidogo na ndipo ulale na pia wakati wa kulala daima lala kwa upande usilale chali , ukilala chali unasababisha kiwango cha asidi kupanda juu na kuingia kooni hali inayoongeza kuwepo kwa tatizo.
4. Wakati wa kula kula kiasi kidogo na mara nyingi uwezavyo.
Hii ina maana kwamba siku zota kama umegundua una tatizo hili kula chakula kidogo kidogo na unaweza kutumia mda mwingi yaani kwa siku unaweza kula mala tano ila una kula chakula kidogo kidogo .
5. Jaribu kupunguza mfumo wa ulaji.
Hii ina maana kuepuka vyakula vya kukaanga, vyakula vyenye kemikali nyingi na vyakula ambavyo huwa na utamu kinywani ila havina faida yoyote mwilini daima siku zote kama una tatizo hili chemsha chakula chako kwa sababu vyakula vyenye kemikali nyingi na mafuta vina asidi nyingi.
6. Epuka nguo za kubana,
Kwa kawa watu wenye matatizo ya kuwepo na asidi mwilini wanapaswa kuepuka nguo za kubana na kuvaa nguo zilizo wazi ili kuweza kuwa huru na kuruhusu mzunguko wa damu mwilini juwa kawaida
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 kitabu cha Simulizi 👉2 ai web app 👉3 Kitau cha Fiqh 👉4 Bongolite - Game zone - Play free game 👉5 Kitabu cha Afya 👉6 Simulizi za Hadithi Audio
Post zinazofanana:
Kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi: Ni hatari?
Kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi, kitaalamu kama Menorrhagia, ni hali inayowapata wanawake wengi. Ingawa si kila mara ni ishara ya ugonjwa mbaya, damu nyingi kupita kiasi inaweza kusababisha upungufu wa damu mwilini (anemia) na kuathiri kwa kiasi kikubwa maisha ya kila siku. Makala hii inaelezea nini kinachozingatiwa kuwa "damu nyingi," sababu zake, na wakati muafaka wa kutafuta msaada wa kitaalamu.
Soma Zaidi...Dalilili za kukosa oksijeni
Posti hii inazungumzia kuhusiana na dalilili za kukosa oksijeni ambalo kitaalamu hujulikana Kama apnea.kukosa oksijeni ni tatizo ambapo kupumua kwako hukoma na kuanza unapolala.
Soma Zaidi...Namna ya kumsaidia mtoto mwenye UTI
Post hii inahusu zaidi namna ya kuwasaidia mtoto akiwa na ugonjwa wa UTI.
Soma Zaidi...Ugumba (Infertility): Je, tatizo huanzia wapi kwa mwanamume na mwanamke?
Ugumba hufafanuliwa kama hali ya kutoweza kupata ujauzito baada ya kushiriki tendo la ndoa mara kwa mara bila kutumia njia zozote za uzazi wa mpango kwa kipindi cha mwaka mmoja (au miezi sita kwa wanawake walio na umri wa zaidi ya miaka 35). Ni tatizo linalogusa pande zote mbili; takwimu zinaonyesha kuwa katika visa vya ugumba, karibu theluthi moja inatokana na mwanamume, theluthi moja inatokana na mwanamke, na theluthi iliyobaki ni mchanganyiko wa pande zote mbili au sababu zisizojulikana.
Soma Zaidi...Mate yanaweza kuambukiza ukimwi
Jibu ni hapana, matehayawezi kuambukiza HIV. Lakini swali unalotakiwa kulijibu je ni kwa nini mate hayaambukizi. Makala hii itakwend akukupa majibu haya
Soma Zaidi...