Huduma kwa watu waliodhani wamepatwa na maambukizi.

Posti hii inahusu zaidi huduma ambazo utolewa kwa watu wanaodhani wamepatwa na maambukizi ya virus vya ukimwi.

Huduma kwa watu wanaodhani wamepatwa na maambukizi ya virus vya ukimwi.

1. Hii ni huduma ambayo utolewa kwa wale wanaodhani wamepatwa na maambukizi ya ukimwi, maambukizi unaweza kuyapata kupitia sehemu mbalimbali kwa mfano mtu kapata ajali na ana maambukizi na wewe unaenda kumsaidia na una kidonda na damu zinazagaa mwili mzima na ukihisi umepata unaweza kwenda hospital na kupata dawa hizo, unapaswa kujieleza kwa yaliyotokea au pengine umechomaa sindano iliyomchoma mgonywa wa ukimwi au umebakw yaani hali yoyote ambayo unahisi umepata maambukizi.

 

2. Kwanza kabisa ukihisi umepata ugonjwa huu usupaniki jisafishe vizuri kama ni damu iondoe na nenda kwenye kituo cha afya uwaeleze kilichotokea na watakusikiliza, kwanza watakupima kama una maambukizi kama hauna watakupatia dawa za mwezi mzima na utazimeza kwa mwezi huo baada ya mwezi au siku ishilini na nane utakwenda kupima kama uliambukizwa kama haujaambukizwa utaendelea na maisha kama kawaida ila kama uliambukizwa utaanzishiwa dawa 

 

3. Maambukizi yanaweza kutokea kwa sababu zifuatazo kwanza unapohisi umeambukizwa unapaswa kwenda hospital ndani ya masaa sabini na mbili ni sawa na siku tatu, au kwa wakati mwingine unaweza kupewa dawa na usizitumie ipasavyo unazitumia ukiwa unakunywa pombe,au Leo umetumia kesho unatumia au wakati mwingine kuziacha kabisa kwa kufanya hivyo huwezi kupona na wadudu wataendelea kufanya kazi vizuri.

 

4. Kwa hiyo tunapaswa kuzipenda na kuzidhamini afya zetu ikitokea ukahisi una maambukizi ni vizuri kuwahi hospital Ili kuweza kupata matibabu na hata ukijamiiana na mtu na una wasi wasi naye ni vizuri kwenda hospital kupata matibabu mapema Ili kuepuka hali ya kuendelea kuishi na maambukizi na tukipewa dawa tuzitumie ipasavyo.



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/05/22/Sunday - 07:58:23 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 973


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-