image

Huduma kwa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi

Posti hii inahusu zaidi huduma ambazo wagonjwa wanaoishi na maambukizi ya virus vya ukimwi wanaweza kupata, huduma hii utolewa hasa kwa wale ambao wamejitokeza kupima afya zao na kujua wazi hali zao na kwa wale wanaofatilia huduma hii wanaweza kuishi vizu

Huduma kwa wanaoishi na maambukizi ya virus vya ukimwi.

1. Huduma ya kwanza ni kuwapa ushauri na kupima mara kwa mara afya zao Ili kuona wadudu wamafikia hatua gani na kuweza kutoa ushauri na elimu kuhusu namna ya matumizi ya dawa. Kwa sababu kwa wale wanaotumia dawa kila siku na kufuata mashart maendeleo yao ni mazuri mno na idadi ya virus upungua ingawa hawawezi kuisha Bali ufubaa.

 

2. Kuhakikisha wamekingwa na magonjwa nyemelezi, yaani magonjwa ambayo utokea pale kinga ya mwili inaposhuka , magonjwa hayo ni pamoja na kifua kikuuu ambapo dawa za kifua kikuuu utolewa kwa wagonjwa wetu na pia kuwapatia watoto vyakula mbalimbali Ili kuweza kuhakikisha kuwa wanakuwa na lishe ya kutosha yaani vyakula vya lishe utolewa kwa watoto wenye chini ya miaka mitano Ili kuepuka tatizo la kuwa na utapia mlo.

 

3. Kuzuia maamikimbi kutoka kwa Mama kwenda kwa mtoto wakati Mama akiwa Mjamzito.

Akina Mama wote wanapokwenda clinic au kwenye mahudhulio ni lazima kwanza kabisa kupima ukimwi Ili kuweza kugundua kama Mama ana maambukizi kama anayo ushauri utolewa Ili kuweza kuepuka maambukizi kutoka kwa Mama kwenda kwa mtoto wakati akiwa Mjamzito, wakati wa kujifungua na wakati mtoto ananyonya kwa kipindi chote Mama anakuwa karibu na wahudumu wa afya Ili kuhakikisha mtoto hasipate maambukizi.

 

4. Kutoa elimu kwa watu ni kuwaahamasisha kupima virus vya ukimwi.

Kuna vikundi mbalimbali ambavyo vimeandaliwa Ili kuweza kutoa elimu kwa jamii Ili kuhakikisha watu wapime pia na kutumia kinga Ili kuweza kupunguza kuendelea kuwepo kwa ugonjwa wa ukimwi na pia kuwaanzishia dawa wale wote waliopata maambukizi ya ukimwi,kwa kufanya hivyo jamii itaweza kuishi kwa matumaini .

 

5. Pamoja na kuwepo kwa ugonjwa huu hatari watu wanapaswa kujua kuwa matumizi ya dawa ni muhimu na kwa kufuata mashart kwa sababu Kuna watu wengi wameugua ugonjwa huu lakini bado wanaoishi na wanaendelea vizuri kwa hiyo tusiwakatishe tamaaa wagonjwa tuwajali na tusiwatenge kwa sababu na wenyewe Wana haki ya kuishi kama watu wengine.

            

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/05/22/Sunday - 07:12:46 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 540


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Ugonjwa wa Pumu, dalili zake na njia za kujilinda dhidi ya Pumu.
Pumu ni ugonjwa ambao huathiri sehemu ya kupitisha hewa kwenda kwenye mapafu ya binadamu kitaalamu huitwa bronchioles. Mtu mwenye pumu huwa na michubuko sugu mwilini kwenye mirija yake ya kupitisha hewa. Hali ambayo husababisha kuvimba kwa kuta za mirija Soma Zaidi...

Sababu za kumsafisha mgonjwa kinywa
Posti hii inahusu zaidi sababu za kumsafisha mgonjwa kinywa, Mgonjwa akiwa anaumwa na pia anakula chakula ni lazima asafishwe kinywa Ili kuweza kuepuka madhara mengine yanayoweza kujitokeza kwa sababu ya kuwepo kwa uchafu kinywani. Soma Zaidi...

fahamu kuhusu vitamini B na faida zake
makala hii inakwenda kukupa faida, kazi na athari za vitamini B mwilini. Nini hutokea endapo utakuwa na upungufu wa vitamini B mwilini? Soma Zaidi...

Sababu za michubuko kwa watoto wanaozaliwa
Post hii inahusu zaidi sababu za michubuko kwa watoto wanaozaliwa,ni sababu ambazo uweza kuchangia kuwepo kwa michubuko kwa watoto wanaozaliwa. Soma Zaidi...

HUDUMA YA KWANZA KWA MTU ALIYEZIMIA (CARDIOPULMONARYRESUSCITATION) AU CPR
Kuzimia ni hali ya kupoteza fahamu ambako kunaendana na kutokuhema. Soma Zaidi...

Faida za chanjo
Posti hii inahusu zaidi faida ya chanjo, tunajua wazi kuwa chanjo Ina faida kubwa kwenye mwili wa binadamu na vile vile kwenye jamii kama tutakavyoona hapo chini. Soma Zaidi...

Aina mbalimbali za maumivu ya mwili.
Posti hii inahusu zaidi aina mbalimbali ya maumivu ya mwili, Maumivu ya mwili utokea kwa aina mbalimbali kama ifuatavyo. Soma Zaidi...

Kazi ya chanjo ya kifua kikuu
Posti hii inahusu kazi ya chanjo ya kifua kikuu kwa kitaalamu huitwa BCG. Ni chanjo ambayo uzuia kifua kikuu na ukoma. Soma Zaidi...

Huduma ya Kwanza kwa aliyepatwa na presha ya kushuka
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyepatwa na presha ya kushuka Soma Zaidi...

Mambo yanayosababisha kupona kwa vidonda.
Posti hii inahusu mambo yanayochangia katika kupona kwa kidonda, ni mambo ambayo yapo kwa mgonjwa mwenyewe kama ifuayavyo. Soma Zaidi...

Namna ugonjwa wa herpes simplex unavyosambaa.
Posti hii inahusu zaidi namna ya ugonjwa wa vipele kwenye midomo na sehemu za siri unavyoweza kuenea kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Soma Zaidi...

Utaratibu wa lishe kwa watoto
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu utaratibu wa lishe kwa watoto Soma Zaidi...