Huduma kwa wenye Maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo
Posti hii inahusu zaidi namna ya kuwasaidia Watu wale ambao wana Maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo.
Huduma kwa wagonjwa wenye Maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo.
1.Kwanza kabisa Watu hawa huwa wanaharisha na kutapika kwa hiyo kitu cha kwanza ni kuhakikisha kurudisha maji yaliyopotea ili kuepuka hali ya kuishiwa maji mwilini.
2.Tunajua kuwa kutokana na Maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo mgonjwa anakuwa na maumivu kwa hiyo tunapaswa kumpatia mgonjwa dawa za kutuliza maumivu kama vile panadol, Asprin na dawa nyingine zinazofaa kwa kupunguza gharama.
3.Pia Mgonjwa anapaswa kupewa antibiotics ambazo usaidia kuzuia maambukizi, antibiotics hizo ni kama vile metronidazole ambazo ni nzuri sana katika kuzuia kuharisha kwa hiyo tunawapatia dawa hizo ili kuweza kuzuia maambukizi kama yapo.
4.Na pia tunapaswa kuangalia kiasi cha maji yanayoingia na kiasi cha maji yanayotoka ili kuweza kuepuka kupoteza kiasi cha maji kwenye mwili kwa kufanya hivyo tutaweza kugundua kama maji yapo ya kutosha au yamepungua.
5.Tunapaswa pia kuangalia vipimo vya mwili kama vile mapigo ya moyo, upumuaji, msukumo wa damu na upumuaji pia tunapaswa kuangalia kiwango cha joto la mwili kama limepanda au limeshuka na kuweza kuliweka sawa.
6.Tumapaswa kujua kuwa maambukizi ya kwenye tumbo na utumbo mdogo kunakuwepo na sababu kwa hiyo tunapaswa kujua chanzo na kuweza kutibu pia tutaweza kuzuia ili kuepuka na matatizo ya Maambukizi kwenye utumbo na utumbo mdogo.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Dua za Mitume na Manabii 👉2 Madrasa kiganjani 👉3 Kitabu cha Afya 👉4 Kitau cha Fiqh 👉5 Bongolite - Game zone - Play free game 👉6 ai web app
Post zinazofanana:
Tatizo la tezi koo
Posti hii inahusu zaidi tatizo la tezi koo, ni tatizo ambalo uwapata watu mbalimbali ambapo Usababisha koo kuvimba na mgonjwa huwa na maumivu mbalimbali na pengine mgonjwa upata kikohozi kwa sababu ya kuwepo kwa Maambukizi kwenye koo.
Soma Zaidi...Maumivu ya magoti.
Maumivu ya magoti ni malalamiko ya kawaida ambayo huathiri watu wa umri wote. Maumivu ya goti yanaweza kuwa matokeo ya jeraha, kama vile ligament iliyopasuka au cartilage iliyochanika.
Soma Zaidi...Maradhi ya Ini na dalili zake, na vipi utajikinga nayo
MAGONJWA YA INI NA DALILIZAKE, NA KUKABILIANA NAYO Ini ni katika viungo vikuu katika mwili wa binadamu.
Soma Zaidi...Namna ya kuzuia Ugonjwa wa ini
Posti hii inaelezea namna na jinsi ya kujikinga au kuzuia Ugonjwa wa ini.
Soma Zaidi...Mtu anaye umwaaa UTI anaweza kuona siku zake?
Kutokuona siku zake mwanamke ni ishara kuwa kuna shida kwenye umfumo wa uzazi. Wakati mwingine kutokuona siku ni ishara ya baraka ya kupata mtoto. Ijapokuwa kuna wengine wanadiriki kutoa mimba kwa sababu zisizo za msingi. Je unadhani UTI inaweza kusababi
Soma Zaidi...Mbinu za kuzuia na kuepukana na maradhi ya uti wa mgongo
Posti hii inahusu zaidi njia au mbinu mbalimbali ambazo zinaweza kutumika ili kuweza kuepukana na tatizo la ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo.
Soma Zaidi...