Huduma ya kanza kwa mgonjwa mwenye jeraha la kawaida kwenye ubongo
Posti hii inahusu zaidi huduma ya kwanza ya mgonjwa mwenye jeraha la kawaida kwenye ubongo, ni Tiba ambayo utolewa kulingana na dalili za jeraha la kawaida kwenye ubongo kama ifuayavyo.
Tiba ya mgonjwa wa jeraha la kawaida kwenye ubongo
1.Kuangalia kama Kuna sehemu yoyote ambayo mgonjwa ameumia kwa sehemu ya nje inayoonekana Moja kwa Moja kwa macho kama Kuna damu ambayo inatoka,au kama Kuna kidonda kinachoonekana au kama Kuna kitu chochote ambacho kimejishikisha kwenye sehemu yoyote ya kichwa, kama vipo jaribu kuviondoa na kama Kuna kutokwa na damu jaribu kuzuia damu isitoke kwa kufanya hivyo unapunguza maumivu kwa mgonjwa.
2.Kumpatia mgonjwa mda wa kupumzika.
Mgonjwa anapaswa kupumzika Ili aweze kurudisha mfumo wa ubongo kwenye nafasi yake au kwenye kazi yake ya kawaida kwa mfano mgonjwa wa jeraha la kawaida kwenye ubongo utapika, uona kizunguzungu, uhisi kichefuchefu,kuona kwa shida au maruweruwe hayo yote utokea kwa sababu ya mshutuko kwenye ubongo kwa hiyo mgonjwa akipata mda wa kutosha wa kupumzika anarudisha kila kitu kwenye hali ya kawaida. Kwa hiyo wahudumu wanapaswa kujulishwa hilo Ili kumpa mgonjwa mda wa kupumzika.
3. Mgonjwa anapaswa kupewa dawa za kupunguza maumivu.
Kwa sababu ya maumivu kwenye kichwa na sehemu mbalimbali za mwili mgonjwa anapaswa kupewa dawa ya maumivu , lakini sio kila dawa za maumivu zinafaa kwa mtu Mwenye jeraha la kawaida kwenye ubongo kwa Sababu nyingine nyingine zinasababisha uvujaji wa damu kuongezeka kama vile Asprini na Ibuprofen mgonjwa hapaswi kuzitumia lla Panadol au paracetamol ni nzuri, kwa hiyo wahudumu wa afya wanapaswa kujua hilo.
4.Mwamshe mgonjwa mara kwa mara na mwoji maswali Ili kuona kama amerudisha fahamu.
Mgonjwa anapaswa kuamshwa na kuulizwa maswali kama vile uko wapi?, Unaumwa wapi?, Unataka nini?, Unaumia wapi? Kwa kufanya hivyo unaweza kuona tatizo la Mgonjwa liko wapi kwa sababu wakati mwingine mgonjwa aliyepoteza fahamu huwa tunamhudumia tunavyojisikia na pengine huwa tunaongeza maumivu bila kujua Ila kwa kumuuliza mgonjwa unaweza kupata njia ya kumlaza au kumgeuza. Kwa hiyo ni vizuri kumwuliza mgonjwa Ili upatiwe urahisi wa kumhudumia.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 web hosting 👉2 Dua za Mitume na Manabii 👉3 kitabu cha Simulizi 👉4 Kitabu cha Afya 👉5 Madrasa kiganjani 👉6 Kitau cha Fiqh
Post zinazofanana:
Namna ya kumsaidia mtoto mwenye degedege
Degedege ni ugonjwa unaoshambulia sana watoto chini ya miaka mitano,na uwaletea matatizo mengi pamoja na kuwepo kwa ulemavu na vifo vingi vinavyosababishwa na ugonjwa huu.
Soma Zaidi...Faida za damu kwenye mwili
Post hii inahusu zaidi umuhimu wa damu mwilini, Damu ni tisu pekee yenye majimaji ambayo hufanya kazi mbalimbali katika mwili wa binadamu.
Soma Zaidi...Vyakula vya kuongeza nguvu za kiume
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu baadhi ya vyakula vinavyoongeza nguvu za kiume
Soma Zaidi...Namna ya kuchoma chanjo
Posti hii inahusu zaidi namna ya kuchoma chanjo, ni njia ambazo utumika kutoa chanjo kwa watoto na watu wazima kwa utaratibu uliowekwa.
Soma Zaidi...Huduma kwa mtoto mdogo anayeumwa
Mtoto mdogo ni mtoto chini ya miaka mitano, yaan kuanzia pale anapozaliwa mpaka anapafikisha miaka mitano
Soma Zaidi...Jinsi ya kutoa huduma ya kwanza kulingana na tatizo
Posti hii inahusu sana mambo ya huduma ya kwanza ambayo huduma ya kwanza inapatikana au inatolewa na mtu yeyote katika jamii .
Soma Zaidi...