image

Huduma ya Kwanza kwa mtu aliyepaliwa

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyepaliwa

.HUDUMA YA KWANZ AKWA ALIYEPALIWA AMA KUKWAMWA NA KUTU KOONI

Mtu aliyepaliwa ama kukwamwa na kitu kooni huwa anashindwa kuzungumza ama kupumua. Hali hii ikiendelea kwa muda inaweza kumsababishi amadhara makubwa hata kifo. Ubongo unaweza kufa ndani ya dakika chache sana kama ukikosa hewa ya oksijeni. Kama ukimkuta mtu amepaliwa ama kukamwa na kitu kooni na anashindwa kupumua unatakiwa umpe huduma ya kwanza:

 

Mtu anaweza kukwamwa ama kupaliwa na chakula, ama kitu kigumu kama kumeza pesa, jiwe barafu na kadhalika. Pia anaweza kupaliwa na maji, asali ama kimiminika chochote na kuzuia njia ya hewa. Hivyo kuathiri mfumo wa upumuaji.

 

Kama kupaliwa ni kwa kawaida amnapo mtu atakuwa na uwezo wa kukohoa, kulia, kuzungumza na kuhema, tambua kuwa anaweza kurudi katika hali ya kawaida hata bila ya kupata huduma ya kwanza. Ili kumsaidia mtu huyu kurudi haraka katika hali ya kawaida

1.Mwambie aendelee kuhohoa zaidi hii itasaidia kuondoa kilichokwama

2.Mwambe ajaribu kutema kicho kilichomkaba ama kilicho mkwama ama kusababisha kupaliwa

3.Katu usuthubutu kuingiza vidole vyeko kwenye koo lake eti kujaribu kukitoa kilicho mkaba

 

Kupaliwa kwa namna nyingine iliyo mbaya ni pale mtu anaposhindwa kusema, kukohoa, kulia ama kuhema. Bila ya huduma ya kwanza mtu huyu anaweza kuzimia na hatimaye kupoteza maisha. Huduma ya kwanza kwa mtu huyu ni:-

1.Muinamiche kifua chake kwa mbele, hii itasaidia kitu kilichomkaba kisiende ndani sana

2.Simama nyuma yake pembeni kidogo, weka mkono wako mmoja kwenye kifua chake na mgono wako mwingine anza kumpiga ngumi kwenye mgongo wake kati ya bega na bega, usawa na kifua kwa nyuma.

3.Angalia kama kilichomkaba kimeondoka

4.Kama hakijaondoka mpige tena kwa nguvu mapigo matano kama ni mtoto mminye kwa nguvu kwenye tumbo lake fanya hivi mara tano. Usifanye hivi kwa mtoto mdogo.

5.Kama hali inaendelea umpeleke kituo cha afya cha karibu.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1162


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Madhara ya ulevi
Poshi hii inahusu madhara ya ulevi.Utegemezi wa pombe kwa kawaida humaanisha kuwa mtu anatumia kiasi kikubwa cha pombe na kuna masuala kuhusu kupoteza udhibiti. Soma Zaidi...

Namna ya kumwosha Mgonjwa vidonda
Posti hii inahusu zaidi njia za kutumia unapotaka kumwosha Mgonjwa vidonda, ni njia muhimu ambazo ni lazima kuzipitia unapotaka kumwosha Mgonjwa vidonda. Soma Zaidi...

Jinsi macho yanavyoweza kuzungumza kuhusu afya yako ya kimwili na kiakili
Soma Zaidi...

Vipimo vya kuchunguza kama una asidi nyingi tumboni
Posti hii inahusu zaidi vipimo vya kuchunguza kama una kiwango kikubwa cha asidi au tindikali tumboni Soma Zaidi...

Kumsaidia mtu aliyeingiwa na uchafu au kitu chochote machoni
Posti hii inahusu hasa jinsi uchafu, wadudu na vitu vingine vinavyoweza kuingia machoni.macho ni mojawapo ya milango mitano ya fahamu ambapo kazi yake ni kuona. Soma Zaidi...

Kazi za vitamin B na makundi yake
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu kazi za vitamin B na makundi take Soma Zaidi...

HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEANGUKA KIFAFA
Kifafa kinaweza kumpata mtu muda wowte. Soma Zaidi...

Kwanini mbu hawezi kuambukiza ukimwi
Somo Hili linakwenda kukueleza sababu za kwanini mbu hawezi kuambukiza ukimwi Soma Zaidi...

Kuboresha afya
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu mambo yanayosaidia kuboresha afya Soma Zaidi...

Namna ya kutoa huduma ya kwanza
Huduma ya kwanza ni huduma anayopewa mgonjwa au mtu yeyote aliyepata ajali kabla ya kumpeleka hospitalini Soma Zaidi...

Mkojo mchafu na Rangi za mikojo na maana zake
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu Rangi za mkojo na maana zake na mkojo mchafu Soma Zaidi...

Hizi ni kazi za mapafu mwilini
Makala hii itakwenda kukufundisha kazi 5 za maafu mwilimi. Wengi tunajuwa tu kuwa mapafu yanafanya kazi ya kupumuwa. ila si hivyo tu yapo mengi zaidi. Soma Zaidi...