Nyoka wapo katka makundi makuu mawili, kuna wenye sumu na wasio na sumu.
Nyoka wapo katka makundi makuu mawili, kuna wenye sumu na wasio na sumu. Ni vigumu kuwatofautisha wenye sumu na wasio na sumu kwani wakati mwengine wanafanana sifa. Wataalamu wameweka njia kadhaa za kuweza kuwajuwa weenye sumu. Nyoka mwenye sumu ana sifa zifuatazo
1.kichwa chake kipo katika pembe tatu
2.Rangi zake zinameremeta sana
3.Mboni ya Macho yao yamefanana na macho ya paka
4.Wanapoogelea kwenye maji miili yao inaelea juu
Tmbua kuwa sifa hizi hata nyoka wasio na sumu wamaweza kuwa nazo. Kuwa makini na kaa mbali na nyoka wa aina yeyote kama huna ujuzi na utambuzi huu. Mtu aliyengatwa na nyka mwenye sumu ataonyesha dalili zifuatazo:-
1.Uchovu
2.Kizunguzungu
3.Anaweza kuzimia
4.Kichefuchefu
5.Kuharisha
6.Kutapika
7.Mapigo ya moyo kuongezeka kwa kasi
8.Misuli kukosa uweze wa kutanuka na kusinyaa
9.Kuvimba eneo alipong’atwa.
Ukiona mtu ameng’atwa na nyoka na akaonyesha dalili hizi, wahi kuomba msaada ili awahishwe ituo cha afya kwa haraka. Hakikisha unampatia huduma ya kwanza ili kupunguza athari za kusambaa kwa sumu mwilini. Huduma ya kwanza kwa mtu aliyeng’atwa na nyoka inaweza kuwa kwa nama zifuata zo:-
1.mtulize mgonjwa nafsi yake, mpe maneno matamu na ya kutuliza. Hii itasaidia moyo kupunguza kazi ya kusambaza damu mwilini, hivyo sumu haita sambaa kwa kasi.
2.Muweke mgonjwa chini, na katu usimtembeze, mlaze chini kwa namna ambayo sehemu alipong’atwa itakuwa chini. Kwa mfano kama ameng’atwa mguuni, unaweza kumuwekea kitu kichwani akaegemea kwa mto ili sehemu ya mguuni iwe chini.
3.Ondoa mengo ya nyoka kwa uangalifu na katu usimishe eneo alilongatwa na nyoka.
4.Kama mgonjwa ana kizunguzungu, ama baridi mfunike kwa nguo ili kumuongezea joto
5.Chukuwa maelezo kuhusu aina ya nyoka, hii itasaidia wataalamu wa afya kujuwa tiba sahihi.
6.Osha eneo kwa kupitishia maji kwa juu na katu usisugue ama kuminya jeraha.
Usifanye vitu hivi:
1.Usinyonye sumu kwa mdomo wako
2.Usimpe mgonjwa chakula wala maji
3.Usimtembeze mgojwa
4.Usitumie barafu sehemu yenye jeraha
5.Usifunge kwenye jeraha eti kuzuia mzunguo wa damu.
Umeionaje Makala hii.. ?
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za vyakula vya vitamini
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa ovari kwenye mwili wa mwanamke. ovari ni sehemu ambapo mayai ya mwanamke hutunza, kwa hiyo kila mwanamke huwa na ovari ambayo husaidia kutunza mayai.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi huduma Kwa mgonjwa mwenye maambukizi kwenye kibofu Cha mkojo,ni huduma maalumu ya kumsaidia mgonjwa aliyepata maambukizi kwenye kibofu Cha mkojo.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu namna ambavyo mwili unapambana na maradhi
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi kazi ya chanjo za polio na kazi zake,hii ni chanjo ambayo unazuia maambukizi ya Virusi vinavyosababisha polio.
Soma Zaidi...Uke ni sehemu ambayo imo ndani ya mwili wa mwanamke, sehemu hii ufanya kazi mbalimbali hasa wakati wa kujamiiana, kubarehe na kujifungua kwa mama.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi umuhimu wa damu mwilini, Damu ni tisu pekee yenye majimaji ambayo hufanya kazi mbalimbali katika mwili wa binadamu.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea mambo ambayo hayawezi kuambukiza UKIMWI
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna ya kuwasaidia wagonjwa waliopata maambukizi kwenye milija na ovari, ni wagonjwa waliopata maambukizi kwenye milija na ovari.
Soma Zaidi...