Kung’atwa na nyuki kunaweza kukahitaji huduma ya kwanza kwa haraka kama mgonjwa ana aleji na nyuki.
Kung’atwa na nyuki kunaweza kukahitaji huduma ya kwanza kwa haraka kama mgonjwa ana aleji na nyuki. Utamjuaje kama ana aleji na nyuki?. ni pale utakapomuona aliyeng’atwa na nyuki akivimba mwili, na anaweza pia kupoteza fahamu. Pia hali hizi zinategemea ni kiasi gani cha nyuki wamemg’ata mtu.
Utakapomuona mtu ameng’atwa na nyuki usimkimbie, kwanza msaidie, kuhakikisha kuwa nyuki hawamng’ati tena. Unaweza kuchukuwa blanketi ama shuka uakmfunika vyema. Hakikisha na wewe umefunika pua, mgomo na masikio. Kama nyuki wanaendelea kuja mmwagie maji mgonjwa ili kupoteza harufu ya nyuki.
Hakikisha kabla hujaanza kutoa huduma ya kwanza, kwanza unaangalia hali ya aliyeng’atwa, kama hali ni ya kawaida na hahitaji kwenda hospitali. Kama anahitaji kwenda hospitali haraka wasiliana na kituo kilicho jirani ama tafuta msaada, kwa watu walio karibu. Hakikisha maamuzi haya hayaathiri hali ya mgonjwa. Ili kumpa huduma ya kwanza aliyeng’atwa na nyuki:-
1.kwa upole tumia kitu chenye wembamba kisha toa miiba ya nyuki kwenye ngozi ya mgonjwa. Katu usitukie kucha zako, maana zitaipasua miipa na sumu itaingia ndani na katu hutaweza kuitoa tena.
2.Unaweza kutuia kisu, ama kituchenye ncha, ila hakikisha kuwa miiba ya nyuki haikatiki kwa ndani. Kwa mfano unapotumia kiwembe kuna uwezekano mkubwa ukaikata miib kwa ndani.
3.Muweke mgonjwa mahali pa ubaridi kama inawezekana
4.Osha maeneo aliyong’atwa kwa sabuni na maji
5.Unaweza kutumia dawa za kutuliza maumivu.
6.Zipo dawa kama losheni (calamine lotion) ila ni maalumu kwa aliyeng’atwa na nyuki, kama zipo mgonjwa apakwe.
7.Hakikisha unamtuliza moyo mgonjwa.
8.Kama hali ni mbaya bado mgonjwa apelekwe kituo cha afya.
Umeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi namna ya kuchoma chanjo, ni njia ambazo utumika kutoa chanjo kwa watoto na watu wazima kwa utaratibu uliowekwa.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi ugonjwa wa kipindupindu ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria kwa kitaalamu huitwa vibrio cholera.
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kukabiliana na minyoo
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi umuhimu wa mate mdomoni, mate ni majimaji ambayo hukaa mdomoni na husaidia katika kazi mbalimbali mdomoni.
Soma Zaidi...Post inaenda kuzungumzia kuhusiana na upungufu wa damu mwilini ambapo tutaona SABABU na dalili zake lakin upungufu wa damu mwilini hujulikana Kama ANEMIA.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi watu ambao hawapaswi kupewa chanjo, hawa ni wale ambao wana hali tofauti na ikitokea wakapata chanjo wanaweza kupata madhara badala ya kuwasaidia.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi vipimo vya kuchunguza kama una kiwango kikubwa cha asidi au tindikali tumboni
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi madhara ya chakula kushindwa kumengenywa vizuri tumboni, haya ni madhara ambayo utokea kwa sababu ya chakula kushindwa kumengenywa vizuri tumboni.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi mabadiliko kwa wavulana wakati wa kubarehe, ni kipindi ambacho ni kutoka utotoni kwendea ujana.
Soma Zaidi...Jiamini A ni katika vitamini inayojulikana sana kuboresha na kuimarisha afya vya macho na uoni. Tafiti zinaonyesha kuwa kuna kundi kubwa la watoto wanaopata tayizobla kutokuona kutokana na ukosefu wa vitamini A vya kutosha.
Soma Zaidi...