picha

HUDUMA ZA KIAFYA KATIKA JAMII

Umuhimu wa huduma za kiafya katika jamii

Posti hii inahusu zaidi huduma za kiafya katika jamii ambapo tunaona huduma za afya ni kitu muhimu sana kwa mwanadamu .afya ni hali ya ukamilifu kimwili,kusajili,kijamii na kutokuwepo kwa maradhi .afya bora ni nguzo na rasilimali katika kuchangia maendeleo ya mtu binafsi .familia na taifa .huduma za afya katika jamii ni huduma za kiafya ambazo hupaswa kutolewa na serikali na asasi zisizokuwa za kiserikali ili kuimarisha afya za watu katika jamii .pia kuna huduma za afya ambazo hutolewa kwa makundi maalumu ya watu katika jamii .mfano watoto wadogo,mama wajawazito na watu wenye magonjwa sugu kama kisukari.Asasi zisizokuwa za kiserikali hujumuisha sekta binafsi na mashirika ya dini .huduma hizi hutolewa kwa kuzingatia mabadiliko endelevu katika sekta ya afya.

 

            ZIFUATAZO NI MAMBO MUHIMU KWA HUDUMA ZA AFYA.                                             

  1.kulingana na hapo juu tulipoeleza huduma za afya mwanadamu au jamii inabidi kuwa wanna huduma bora za afya ili waweze kilinda afya zao ili kuondokewa au kujikinga na magonjwa nyemelezi pia jamii au serikali inabidi kupunguza au kuondoa kabisa gharama za matibabu kwa watu walio na magonjwa sugu.ambayo nimeweza kuyaelezea hapo juu hii inapelekea mgonjwa hawa hawana uwezo wa kufanya kazi zao kwa ufasaha .hii itasaidia kupunguza idadi ya vifo vinavyotokana na magonjwa haya.

 

2. Kutokana na hilo kuna umuhimu wa kutoa mafunzo maalumu kwa mama wajawazito na mumewe .mafunzo haya huwandaa kisaikolojia na kihisia namna ya kukabiliana na changamoto za mimba zisizotarajiwa .pia inabidi wapewe ushauri kuhusu namna ya kutunza mimba.sambamba na ushauri ,wazazi tarajali hupata vipimo vya magonjwa ya ngono na UKIMWI .mfano wa magonjwa ya ngono ni kaswende na kisonono.

 

3.kutokana na hilo upo umuhimu mkubwa na kuwa na huduma hizi katika jamii kutokana na sababu mbalimbali.miongoni mwa sababu hizo ni kulinda na kuelimisha kundi la vijana dhidhi ya maambukizi ya magonjwa kama UKIMWI.ni ugonjwa unaowapata sana vijana ambapo wanapokuwa wanafanya ngono zembe bila kutumia kinga pia ugonjwa wa homa ya ini  ambapo kwa kitaalamu wanaita (hepatitis) pamoja na kifua kikuu huduma za afya ulifanya kundi hili ambalo ni nguvu kazi ya taifa liendelee na kuchangia maendeleo yao na taifa kwa ujumla sababu nyingine ni kutoa au kuwsaidia wazee wasiojiweza na kupata huduma za afya .Huduma za afya hutolewa kwa sababu wazee hawana uwezo wa kujihudumia 

 

4.pia kutokana na umuhimu  wa huduma za kiafya serikali ina bidi itoe elimu kuhusu afya ili wananchi waweze kujifunza na kutambua jinsi ya kutunza afya zao  pia inabidi iweke vitengo mbalimbali vinavyotoa huduma za afya katika jamii .mara nyingi vitengo hivo hupatikana hospitalini ,katika vizuo vya afya na zahanati .hats hivyo,bahadhi ya vitengo havipo hospitalini kutegemea haina ya kundi linalohudumiwa na huduma zinazotolewa katika jamii husika  .pia inabidi serikali iangalie utoaji wa chanjo na dawa kwa watoto wadogo ili kujikinga na magonjwa mbalimbali kama pepopunda ,polio,kifua kikuu ,ugonjwa  wa ini pamoja na ndui 

 

5.kuna umuhimu mwingine ambapo kuzuia ulemavu unaoweza kuwapata watoto wadogo kwahio inashauriwa mtoto akizaliwa lazima apatiwe afya bora malezi mazuri na mazunzo mazuri kwa mama yake ambapo usaidia kupunguza vifo ambavyo huwapata watoto katika umri mdogo .

 

6.kutokana na hilo pia kuna umuhimu wa kusaidia vijana walioathirika na dawa za kulevya huweza kurudi katika hali zao za kawaida .hili hutokana na tiba na unasihi wa kuwaongoza kurudi kwenye maisha ya kawaida .pia vijana inabidi wapewe elimu jinsi ya kuhimili mabadiliko ya kimaumbile wanayokabiliana nayo 

 

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2022/08/03/Wednesday - 10:21:40 pm Topic: Jifunze Main: Afya File: Download PDF Views 1315

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
πŸ‘‰1 Bongolite - Game zone - Play free game    πŸ‘‰2 Madrasa kiganjani    πŸ‘‰3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    πŸ‘‰4 web hosting    πŸ‘‰5 ai web app    πŸ‘‰6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina   

Post zinazofanana:

darasa la lishe

Jifunze mengi kuhusu afya na lishe, ujuwe utaratibu wa lishe

Soma Zaidi...
MAZINGIRZ

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...
darasa la lishe

Jifunze mengi kuhusu afya na lishe, ujuwe utaratibu wa lishe

Soma Zaidi...
NYANJA ZA AFYA

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...
SHUGHULI ZA KILA SIKU

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...
Kitabu cha Afya 04

Afya inaweza kuathiriwa na vitu vingi sana. Hapa tutaendelea kuona mabo zaidi yanayoathiri afya yako.

Soma Zaidi...
Dondoo za afya 21-40

Somo Hili linakwenda kukuletea dondoo mbalimbali za afya

Soma Zaidi...
Ukuaji wa mmea

Je wajua kwa nini mmea kama nyasi na miti hukua? Posti hii inahusuΒ  zaidi ukuaji wa mimea katika mazingira yetu kwa sababu watu hawatambui kwamba mimea .ni chanzo cha mahitaji kwa binadamu.

Soma Zaidi...
Kitabu Cha Magonjwa Sugu

Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet.

Soma Zaidi...
dondoo 100 za Afya

Basi tambua haya;- 61.

Soma Zaidi...