HUDUMA ZA MSINGI KWA MAMA MJAMZITO NA MTOTO.


image


Posti hii inahusu zaidi huduma muhimu anazopaswa kupewa mama mjamzito wakati akiwa na mimba, wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua yaani ndani ya masaa ishirini na manne, tunajua wazi kuwa Mama akiwa mjamzito anaweza kupata matatizo mbalimbali kwa hiyo anapaswa kupewa huduma muhimu kama ifuatavyo.


Huduma za msingi kwa mama mjamzito na mtoto.

1. Uzazi wa mpango.

Hivi ni huduma ya msingi kabisa ambayo Mama anapaswa kujua kabisa namba ya watoto anaowahitaji na ni namna gani wanapaswa kuachana kwa miaka, hali huu umsaidia Mama kupumzika kutoka kwenye nzao moja kwenda nyingine na kuwasaidia watoto kupata mda mzuri wa kukua, kupendwa, kupata malezi ya kutosha kwa mda mwafaka na kupata elimu ya kutosha. Kwa hiyo Mama anapaswa kuchagua njia ya uzazi wa mpango ambayo ni ya maana na faida kwake.

 

2. Usafi wakati wa ujauzito , kujifungua na wakati wa malezi ya mtoto.

Mama anapaswa kuwa msafi mda wote anapokuwa na mimba na kuandaa vifaa vyake kwa hali ya usafi wa hali ya juu kwa kufanya hivyo anazuia maambukizi bambayo yanaweza kuleta maendeleo kwa mtoto na kwa Mama mwenyewe, hali huu utokea kwa akina mama hasa wale wanojifungulia vijijini utumia viwembe vyenye kutu kukata kitovu na hatimaye kusababisha maambukizi kwa mtoto na hatimaye madhara makubwa yanayoweza kujitokeza. Kwa hiyo tunapaswa kuwahimiza akina  mama kujiandaa na kuwa na vifaa vizuri wakati wa kujifungua.

 

3. Kuzuia maambukizi kutoka kwa Mama kwenda kwa mtoto.

Hivi ni njia ambayo umsaidia mtoto kutopata maambukizi ya HIV au AIDS na kaswende kwa hiyo Mama anapoanza mahudhurio ya kwanza anapaswa kuja na mme wake ili kupima Maambukizi na kabla ya Mama kujifungua anapaswa kuja kupima maambukizi ili kama wazazi wana Maambukizi waweze kumkinga mtoto ili hasipatwe na wakati wa kujifungua kuwa makini ili kumzuia mtoto hasipatwe na Maambukizi, na pia huwasaidia wazazi wote way kujua afya zao endapo walikutwa na Maambukizi wanaanza dawa mara moja.

 

4. Pia wakati wa  ujauzito mama anapaswa kukingwa na Dalili za hatari.

Hizi ni Dalili ambazo ujionyesha kwa mama wakati akiwa na mimba na zisipotibiwa au kushughulikiwa mapema zinaweza kufanya mimba kutoka , Dalili hizo ni pamoja na kuvimba miguu kwa mama, kutokwa damu ukeni na uchafu ukeni, mtoto kushindwa kucheza akiwa tumboni, maumivu makali ya kichwa kwa mama mjamzito, Mama akisikia Dalili kama hizi anapaswa kuwahi mapema hospitali kwa ajili ya huduma zaidi, kwa hiyo mama anapaswa kujua wazi dalili za hatari na kuweza kuepukakana nazo au kwenda hospitali mara moja.

 

5. Kumtunza mama na Mtoto, baada ya Mama kumaliza kujifungua,

Hii ni huduma ambayo utolewa kwa Mama na mtoto ndani ya Masaa ishirini na nne, katika kipindi hiki Mama na mtoto upewa nafasi ya kupumzika ili kuweza kuangalia maendeleo yao au kuangalia kama kuna kitu chochote kinachoweza kubadilika lakini elimu utolewa kwa Mama namna ya kumlisha na kumtunza mtoto na chanjo mbalimbali utolewa kwa mtoto ili kumkinga na Magonjwa nyemelezi kwa mtoto, kama mtoto na Mama wanaendelea vizuri wanaweza kuruhusiwa kwenda nyumbani.

 

6. Kwa hiyo tunajua wazi ,Mama akiwa na mimba kuna mabadiliko mengi ambayo utokea kwa hiyo tunapaswa kuwapa kipau mbele na kuwasikiliza wajawazito na kuwapa chakula na dawa zinazofaa kwa hiyo tuachane na mila potofu na imani zisizofaa kwa akina Mama wajawazito.



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Hadiythi za alif lela u lela       ðŸ‘‰    2 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    3 Jifunze fiqh       ðŸ‘‰    4 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    5 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    6 Mafunzo ya html kwa kiswahili    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Signs and symptoms of pregnancy.
In fact there is a lot of signs and symptoms of pregnancy a mother experiences throughout pregnant. These signs may start to be revealed immediately after conception or in the first week after conception. A term pregnancy is traditionally calculated by midwives as 9 months and 7 days or 120 days or 40 weeks but they all mean one thing. These signs are divided into three trimesters three months per each trimester because a term pregnancy is having nine months. Soma Zaidi...

image Ulemavu wa ubongo na mfumo wa fahamu -multiple sclerosis
Posti hii inazungumzia kuhusiana na dadili na sababu zinazopelekea Ugonjwa wa ulemavu wa ubongo na mfumo wa fahamu ambao kitaalamu hujulikana Kama multiple sclerosis. Soma Zaidi...

image Namna ya kumsaidia mtoto mwenye degedege
Degedege ni ugonjwa unaoshambulia sana watoto chini ya miaka mitano,na uwaletea matatizo mengi pamoja na kuwepo kwa ulemavu na vifo vingi vinavyosababishwa na ugonjwa huu. Soma Zaidi...

image Faida na hasara za Kufunga kizazi kwa Wanaume
Posti hii inazungumzia Faida, hasara, na madhara ya Kufunga kizazi kwa Wanaume. Soma Zaidi...

image Namna ya kuzuia maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo
Posti hii inahusu zaidi namna ya kuzuia maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo, hizi ni njia ambazo zinapaswa kufuatwa ili kutokomeza kabisa maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo. Soma Zaidi...

image Mambo muhimu ambayo mama mjamzito anatakiwa kuzingatia.
Posti hii inazungumzia kuhusiana na Mambo ambayo mama mjamzito anatakiwa kuzingatia katika kipindi Cha ujauzito au mimba Soma Zaidi...

image Utajuwaje kama kidonda kupona
Posti hii inahusu zaidi juu ya kuhakiki kama kidonda kimepona kwa mgonjwa mwenye vidonda, kwanza kabisa tunajua kuwa vidonda uwanyima Watu raha na pengine kuwafanya wakate tamaa kama wapo hospitalini kwa hiyo tunapaswa kutumia njia zifuatazo ili kuweza kuhakikisha kama kidonda kimepona au la. Soma Zaidi...

image Sababu za ugonjwa wa mkojo kuwa na damu
Posti hii inaelezea sababu zinazosababisha mkojo kuwa na damu. Soma Zaidi...

image Mambo yanayosababisha kuharisha
Post hii inahusu zaidi ugonjwa wa kuharisha, kuharisha ni kitendo Cha kupitisha kinyesi Cha maji chenye damu au kisichokuwa na damu Soma Zaidi...

image Aina za saratani ( cancer)
Posti hii inahusu zaidi Aina za kansa, Kansa ni Aina ya ugonjwa unaosababishwa na kuzaliana kwa seli ambazo sio za kawaida. Soma Zaidi...